Nani mwizi nani mla rushwa?

Mjomba wa taifa

JF-Expert Member
Apr 20, 2012
231
161
Inahitaji nguvu ya ziada kuweza kung'amua baina ya wizi na rushwa. Makosa yote haya kwa mujibu wa sheria ni makosa ya Jinai. Kwa maana rahisi kabisa mwizi ni yule anaechukua kwa uficho mali au kitu pasipo ridhaa ya mmiliki husika. Rushwa ni kitendo cha kutoa/kupokea hongo kwa lengo la kupindisha taratibu zilizowekwa ili kurahisisha kusudio la mtoaji. Kisheria mtoaji na mpokeaji wote ni wahalifu.

Hivi karibuni baadhi ya mawaziri wameondolewa katika baraza la mawaziri kwa tuhuma za wizi na matumizi mabaya ya mali ya umma. Kwangu mimi mawaziri hawa sio walarushwa bali ni wezi. Kwa taratibu za kisheria wala rushwa huchunguzwa na TAKUKURU na wezi hukamatwa na POLISI.

Sasa basi, kama hivyo ndivyo kwanini mawaziri hawa wasikamatwe na Polisi wakapelekwa mahakamani ili sheria zichukue mkondo wake. Kama wanachunguzwa kwa makosa ya rushwa, ni nani mpokeaji? na ni nani mtoaji?

Tufikie hatua makosa ya wizi yasichanganywe na rushwa ili tusipotoshe maovu ya Mafisadi. Tusije tukahadaiwa hata wakwapuaji tukawaita wala rushwa.
 
seria ipi inayokataza polisi kukamata mla rushwa?? Takukuru wanachunguza pale ambapo hakuna uhakika ila kama kuna uhakika pasi shaka yoyote wala rushwa wanakamatwa na kupelekwa mahakamani!!
 
Back
Top Bottom