Nani mwenye makosa

Columbus

JF-Expert Member
Nov 5, 2010
2,002
648
Nilipata simulizi hii kutoka kwa rafiki yangu.

Polisi watatu waliokuwa lindoni usiku wa manane walilikamata gari moja lililokuwa na mali ya wizi, baada ya kulisimamisha mwenye mali alishuka na kuwafuata wale polisi. Mwenye mali alikiri na alikuwa tayari kuwapatia gawio la shilingi milioni sita huku akidai kuwa ule mzigo wote ulikuwa na thamani ya shilingi milioni kumi na mbili. Baada ya malumbano ya muda hatimaye polisi wawili wenye vyeo vya corporal walikubali wachukue hizo fedha wagawane wote watatu ili wamuachie, lakini yule askari mwingine mwenye cheo kikubwa zaidi alionyesha kutokubaliana na wazo hilo na kutaka suala hilo lifikishwe kituoni.

Katika hali ya sintofahamu wale polisi wawili waliamua kuchukua zile pesa na kumruhusu yule mwenye mzigo wa wizi kuondoka na mzigo wake. Wale polisi wawili waendelea kumbembeleza yule polisi mwenzao wagawane kiasi cha shilingi milioni mbili mbili kila mmoja lakini yule polisi mwenye cheo cha juu kidogo alikataa na aliwanunia wale polisi wenzake na kuwahakikishia kuwa suala lile atalifikisha kwa mkuu wao wa kituo.

Kadri muda ulivyokuwa unaendelea yule polisi wa cheo zaidi ya wenzie aliendelea kusisitiza kuwa cha moto watakiona mara kutakapopambazuka atakapolifikisha suala lile mbele ya mkuu wao. Wale polisi wawili waliamua kumuongezea shilini milioni moja zaidi lakini alikataa katakata. Katika historia yao huko nyuma ilionyesha kuwa yule polisi aliyekuwa akikataa fedha alikuwa na tabia ya ubinafsi ya kutaka fedha zote apewe yeye ambapo wale wenzie hawakuwa tayari kwa hilo.

Ilipofika asubuhi saa za kazi wale polisi waliopokea zile fedha waliamua kumuona mkuu wa kituo mapema kabla ya yule mwenzao aliyezikataa zile pesa na kumueleza hali halisi iliyotokea kule lindoni. Wote kwa pamoja waliamua kumpatia bosi wao gawio la shilingi milioni mbili ambapo bosi alifurahi sana. Baada ya hao askari wawili kutoka ofisini kwa bosi yule askari aliyekataa kupokea zile pesa aliingia na kumsimulia yule bosi yale yaliyotokea lindoni. Aliendelea kumueleza bosi kuwa tabia ya kuchua rushwa kwa wahalifu itabidi ikemewe kwa nguvu zote katika jeshi la polisi na kwamba suala lile atalifikisha pia kwenye vikao vyao vya kila mwezi.Yule bosi alionyesha kukasirishwa sana na tukio hilo la kuchukua rushwa toka kwa wahalifu na kuahidi atawaita wale askari wawili na kuwashuhulikia ipasavyo.

Mara baada ya yule askari aliyekataa pesa kutoka ofisini yule bosi aliwaita wale askari wawili na kuwaeleza nia ya yule mwenzao ya kulipeleka lile sula mbele. Yule bosi aliwaagiza kuwa siku ya pili watakapoenda lindoni wahakikishe ya kuwa yule askari mwenzao harudi kituoni akiwa hai. Na kweli siku iliyofuata wakiwa lindoni majira ya saa nane na nusu usiku walimpiga risasi ya kichwa yule mwenzao na kumuua pale pale kwa kisingizio kwamba alipigwa risasi na majambazi waliokuwa kwenye gari iliyokuwa ikipita kwa kasi mbele yao.


Mwisho: Je katika hadithi hii tunajifunza nini? nani alifanya kosa na ni kosa gani? nawasilisha.








 
Kwani hujui rushwa na mauaji ni makosa kisheria?...
 
Hao jamaa hawaishi vituko,kuna siku niko Check Point jirani na mapambano kama saa sita usiku,basi jamaa wakaja na mikwara kibao eti muda wa kufunga baa umefika nikanunua kreti mbili za Safari nikamwambia muhudumu aziweke kwenye parking pembeni ya Baa,basi waliondoka mmoja mmoja kuzifuata.Kwa hiyo hata kwa kesi hii unayouliza naweza sema kuwa hakuna mwenye kosa ila ni tabia yaoo//
 
Wakubwa hapo juu,una mtoto mgonjwa sana na umefanikiwa kumfikisha hospitali ila dokta anataka kitu kidogo ili amuhudumie mgonjwa wako,wewe misimamo yako hairuhusu katika kuvutana huko mtoto amekufa?kwa hyo nikupongeza kwa kutopokea rushwa na mtoto kufa?
 
Wa kulaumiwa ni mkuu wao aliyetoa amri ya huyo bwana kuuawa.
 
Mijitu mingine bana, sa amekataa million 2 kwani ye mshahara wake ni kiasi gani mpaka aone mil 2 ndogo
 
Back
Top Bottom