Nani mwenye dhambi? Nani mwenye dhawabu?

Nicas Mtei

JF-Expert Member
Dec 21, 2010
11,556
7,085
Askofu aliendesha harambee
kuchangia ujenzi wa kanisa. Wakristo
wakatoa Tshs75,050 tu. Ghafla
majambaz wakateka kanisa na
kuamrisha kila mtu atoe alichonacho!
Wakakusanya Tshs 8,945,800 kisha majambazi wakamkabidh askofu fedha
hizo zote ili aendeleze ujenzi. Je
majambazi wana dhambi au wakristo
wanathawabu? Toa maoni yako.
 
Mandhar uliyotoa inachekesha na kusikitisha..Wakristo, kwa hiari yao walitoa kulingana na uwezo wao. Majambazi walipoingia, uhuru na hiari ya wakristo vilitoweka. Ingawa fedha walizokusanya majambazi zilikabidhiwa kwa kiongozi wa dini, fedha hiyo ilikusanywa kimakosa. Kwa majambazi ni dhambi juu na wakristo ni poa.
 
Hapo kosa lipo kwa majambazi, katika kuchangia ni sadaka na sadaka kwa mujibu wa Imani yangu hutakiwi kuitoa kwa kulazimishwa wala kujilazimisha bali unaweza kutoa chochote ulichonacho bila ya kuangaliwa uwezo wa mtu tofauti na zakat ambayo hutolewa kwa kiwango maalum kulingana na mali mtu aliyokua nayo.
 
hao hawakuwa majambazi watakuwa maaskofu wa kisasa hao! maana sifa za majambazi sio hizi, jambazi ni chukua ukibisha chinja ua tupa kule na hampati kitu
 
Back
Top Bottom