Nani mvumilivu kati ya mwanaume na mwanamkeke?

lolz
frankly speaking madume hatuvumilii hata chembe.....mimi binafsi namiliki password ya email zake,from thursday mpaka j3 simu zote zinazoingia kwake nime divert kwangu.....hana password zangu na n.k...
hii sio mfumo dume ni jinsi gani ninavyomjali na anapenda kweli kweli

Huyu ni mke au galfriend?
Kama ni mke basi umefanikiwa kumgeuza mwanasesere - hongera!
Kama ni gf basi iko siku utashangaa atakavyokuponyoka!
 
naamini suala hapa si uvumilivu bali ni jinsi jinsia hizi mbili
zinavyo-react wakati wa misukosuko ya ndoa. wanaume ni
wawazi na hawafichi hasira zao pale wanapogundua/kuhisi
mwenzi ametoa tunda nje. hatua wanazochukua mara nyingi
ni za papo kwa hapo na zinachangiwa zaidi na jazba kuliko mkakati.

kwa upande mwingine wanawake wao wanauwezo mkubwa wa
kuficha hasira zao na mara nyingi hatua wanazochokuwa ni za
kudhamiria na zenye kuandaliwa na mikakati imara. hapo ndio
kwenye usiri wao. kuto-react papo kwa hapo sio kipimo cha
uvumilivu wala kwamba usamehevu, la hasha, bali ni ishara ya
nia yao ya kujibu mapigo tena kuhakikisha mapigo hayo yatamuumiza
mwenzi kuliko alivyoumia yeye.

hata hivyo katika jinsia zote hizi kuna tofauti hivyo basi hayo niliyoyaeleza
hapo juu yanahusisha wengi na sio wote
 
...Interesting; Wazo la kuwa na KIPOOZEO lingekusaidiaje kwenye shida ulizokuwa nazo?


kama binaadamu wa kawaida/kamili nahitaji mapenzi, hakuwa kwa ajili ya kunisaidia/kunitatulia shida nilizo kuwa nazo.
 
Du ! mwanamke ni mvumilivu pia ni mwepesi kusamehe na kusahau,lakini kwa mwanaume hatuna uvumilivu katika jambo hili ni wagumu wa kusamehe,maana kila picha hiyo inapokuja unaji8sikia moyo kwenda mbio isivyokawaida na hii haijalishi umri wa mtu wala imani ya mtu ukweli inataka moyo.
 
Nimeshuhudia kuona mara nyingi katika mahusiano Mwanaume akiwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanamke mwingine, huwa mwenzi wake anaweza msamehe ila kwa sisi wanaume ukigundua mwanamke wako anauhusiano wa kimapenzi na mwanaume mwingine ni fujo,wengine mangumi,visu...mbaya zaidi kama ni ndoa unatoa talaka fasta .....HII NI SAWA JAMANI....NANI MVUMILIVU?
Wanawake wavumilivu
 
Back
Top Bottom