Nani muislam? wote kimya!!!!

Mtego wa Noti

JF-Expert Member
Nov 27, 2010
2,591
1,599
Jamaa kajitoma mskitini ghafla, huku majasho
yanamtoka!
Mkononi kashika panga kali, Akauliza,"nani muislamu hapa,"
watu
kimya. Karudia tena kimya "nani muislam hapa".
Ghafla kamnyakuwa
jamaa alikuwa karibu na mlangoni akaondoka nae!
Kufika nje akamwambia,
"Samahani mkuu wangu najua nimekusumbua, naomba
unisaidie kuchinja mbuzi"
jamaa akachinja yule mbuzi, alipomaliza
akasema yeye hawezi kumchuna
mbuzi.

Jamaa akiwa na panga lenye damu akarudi tena msikitini!
"jamani
nauliza humu nani muislamu?" jamaa wakamnyooshea kidole imamu wa
siku
ile.
Imam akaanza kujitetea!" aah jamani mi kuswalisha siku 2 tu
ndo
nimekuwa muislamu sana?,hapana mimi si muislam ila nilikuwa
najifunza
mila za dini hii tu."
jamaa akasema "naomba uondoe hofu naomba
ukanisaidie kuchuna mbuzi nje!"
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom