"Nani MUISLAM hapa??"

LiverpoolFC

JF-Expert Member
Apr 12, 2011
11,348
3,219
Jamaa aliingia Msikitini na panga mkononi na kuuliza:

"Ni nani Muislam hapa?" Wote waliokuwa msikitini wakanyamaza kimya.
Akarudia kuuliza tena: "Nani Muislam hapa?" Vile vile hakujibiwa waumini wote kimya.

Jamaa alitoka nje na kumchukua mmoja wa waumini kumwomba amchinjie mbuzi. Halafu alirudi tena msikitini na panga lake lenye damu mkononi na kuuliza tena: Nani Muislam hapa?

Waumini walimuonesha kidole Imamu kuwa ndiye Muislam,Imamu alijitetea kwa kusema:
Jamani Mi kuswalisha siku mbili ndiyo mniite Muislam? Mi hapa najifunza tu!"
Jamaa aliyekuwa ameshikilia panga alisema: Jamani mbona hivyo,Mi nilikuwa nataka Muislam mmoja anisaidie kuchuna mbuzi na kuja kuigawa msikitini." Waumini walibakia vinywa wazi.

Mmmh! Kweli maisha matamu.
 
hahaha!!!
Imani dhaifu!!!!!!loh!!!
sasa na huyo mwenye Panga nae kadhamiria kutisha watu, unamtafuta aliye Muislamu ndani ya Msikiti jamani!
 
Du nimeiroma nikiwa kwenye daladala acha nicheke abiria wamebaki kunishangaa tu! Ya ukweli mkuu
 
Jamaa aliingia Msikitini na panga mkononi na kuuliza:

"Ni nani Muislam hapa?" Wote waliokuwa msikitini wakanyamaza kimya.
Akarudia kuuliza tena: "Nani Muislam hapa?" Vile vile hakujibiwa waumini wote kimya.

Jamaa alitoka nje na kumchukua mmoja wa waumini kumwomba amchinjie mbuzi. Halafu alirudi tena msikitini na panga lake lenye damu mkononi na kuuliza tena: Nani Muislam hapa?

Waumini walimuonesha kidole Imamu kuwa ndiye Muislam,Imamu alijitetea kwa kusema:
Jamani Mi kuswalisha siku mbili ndiyo mniite Muislam? Mi hapa najifunza tu!"
Jamaa aliyekuwa ameshikilia panga alisema: Jamani mbona hivyo,Mi nilikuwa nataka Muislam mmoja anisaidie kuchuna mbuzi na kuja kuigawa msikitini." Waumini walibakia vinywa wazi.

Mmmh! Kweli maisha matamu.

Kwaa kwaa kwaa, tehetehe, umetisha jomba...Kwenda peponi c kazi rahisi.
 
Back
Top Bottom