Nani mmiliki wa Habari Leo?

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
121,918
95,201
Wana jamvi amani iwe kwenu,

Kufuatia gazeti la Hahabri Leo kuamua kuandika habari zinazokibeba CCM na kuandika habari za kuviponda vyama vya Upinzani, naomba kujua mmiliki wa gazeti hilo, mishahara wanalipwa na fedha za nani?

Serikali kupitia shirika lake la Tanzania Standard Newspaper. Ndo wanachapisha na Daily News
 
Habari Leo, Daily News, TBC, Sunday News ni magazeti ya serikali, yanaendeshwa kwa kodi za wananchi. Ni jambo la ajabu kabisa kuwa vyombo hivyo vinatumika na CCM.

Mkuu nivema tujiandae kuvishitaki vyombo hivyo mahakamani kwa kutumia fedha za umma kwa kukitumikia ccm huku wakitumia rasilimali za taifa na jasho letu
 
Serikali kupitia shirika lake la Tanzania Standard Newspaper. Ndo wanachapisha na Daily News

Ni muda muafaka wa kuvishitaki vyombo hivyo kwa kutumia kodi za watanzania kuitumikia ccm na huo ni wizi na ufisadi
 
Nani mmiliki wa Tanzania daima??? Maana wanaandika habari za ukawa tuu
Hili gazeti ni Mali ya umma na sio mtu binafsi,Tanzania Daima na Mwanahalisi ni magazeti ya watu binafsi, unafananishaje na gazeti la umma? Mbona hujaulizwa kuhusu raia Mwema au jambo Leo la Juma mpito?
 
Hili gazeti ni Mali ya umma na sio mtu binafsi, Tanzania Daima na Mwanahalisi ni magazeti ya watu binafsi unafananishaje na gazeti la umma? Mbona hujaulizwa kuhusu raia Mwema au jambo Leo la Juma mpito?

Kweli mkuu naona kuna watu wanakosa nini wapost
 
Nani mmiliki wa Tanzania daima??? Maana wanaandika habari za ukawa tuu

Hi nyie wenzetu uelewa wenu hua ukoje!? Magazeti yanayoshabikia ccm yapo mengi, Raiamwema, raia Tanzania, Dira nk. Mleta huja si kwamba hajayaona hayo, ameyaona but hayo ni magazeti ya watu. Hata Uhuru likifanya hivyo hakuna atakae uliza cause ni gazeti la ccm lakini sio Habari leo, Daily news na Sunday news, hata TBC haipaswi kufanya hayo inayoyafanya kwasababu hivi ni vyombo vya umma; unataka kunambia we hulioni hilo!? Mwanahalisi linamilikiwa na Sead Kubenea, mgombea ubunge kwa Chadema pale Ubungo, Tanzania daima linamilikiwa na familia ya Mbowe ambaye ndiye mwenyekiti wa Chadema, ulitegemea iwaje!? Ndio maana UKAWA wanasema kipaumbele chao cha kwanza ni Elimu, uelewa wa kupambanua mambo wa Watanzania wengi uko chini sana.

Jana nimerudi toka kazini napata habari kwamba jirani yangu ananitambia kwamba atanizomea sana UKAWA ikishindwa uchaguzi (hua tunatanian anae sana tu) nikamwambia mimi hata nikiumwa ugonjwa wowote pamoja na familia yangu hua hatutibiwi na hospitali za serikali, mwajiri wangu anachukua jukumu hilo, na wewe je!? Ukweli watu wengi wanadhani kushabikia vyama hivi kwenye hu uchaguzi ni kama kushabikia YANGA na SIMBA, yote hi ni kwasababu ya ELIMU. Unaweza kusona but namna yako ya kupambanua mambo ikawa chini sana. Sorry kwa maneno yangu mengi, nasikia kugadhabika kwasababu mtu mwenye uwezo wa kutumia internet naye hajui kutofautisha magazeti ya serikali na magazeti ya watu binafsi.
 
Nani mmiliki wa Tanzania daima??? Maana wanaandika habari za ukawa tuu

Binti ongeza bidii katika kozi yako ya pre form one,huku unapokimbilia si mahali sahihi kwako.Mleta mada kauliza uhalali wa Gazeti la Serikali linaloendeshwa kwa kodi zetu kugeuka na kuwa vuvuzera la chama tawala,na hili nalo umeshindwa kuling'amua ewe kizazi cha BRN zao la Mitihani ya multiplechoice?Umedhihirisha huna unachofahamu,umebaki na akili za "kushedi"OMR tu ktika Mitihani yenu ya kuchagua toka swali 1-50,huna thamani yoyote katika Taifa.Bora ufe tu.
 
Back
Top Bottom