Elections 2010 Nani kuiwakilisha CHADEMA 2010?

Luteni

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
2,274
301
WAKATI vyama mbalimbali vikijitokeza kuwania nafasi ya Urais, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema hakina papara ya kumtangaza mgombea wa nafasi hiyo mapema kwa kuhofia kuchafuliwa. Kaimu Katibu Mkuu CHADEMA Taifa, Victor Kimesera, ameliambia gazeti hili.

Amesema malengo ya chama hicho si kukurupuka na kumtangaza mapema mgombea, kwanza ni kujipanga ili kuweza kuongeza idadi ya majimbo na madiwani ambao wataweza kuwa nguvu ya kupambana na chama tawala.

“Matarajio yetu ni kuongeza nguvu bungeni angalau kufikia robo tatu ya wabunge wote,” amesema.

Kimesera amesema kabla ya kuweka wazi jina la mgombea urais, watatangaza majina ya wagombea ubunge na udiwani Agosti 9 na 10, mwaka huu. Amesema ifikapo Agosti 12, mwaka huu wanatarajia kumtangaza mgombea wao wa Urais.

Akifafanua kilichosababisha kuchelewa kuweka hadharani majina ya wagombea hao, amesema si kweli kuwa CHADEMA inasuasua kumtangaza mgombea kama ilivyovumishwa bali wanaendelea kupokea maombi ya wanachama ya kuwania nafasi mbalimbali, na hiyo imetokana na kujitokeza kwa wagombea zaidi ya mmoja katika nafasi moja.

“Hata hivyo, kuna hasara na faida ya kuwahi kumtangaza mgombea, lakini kwa upande wetu tumeona hasara ni kubwa kuliko faida kwani anaweza kufuatwa na wapinzani wake na hatimaye kumchafua,” amedai.

Akifafanua juu ya mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, kugombea ubunge badala ya nafasi ya urais, amesema wameamua kufuata mfumo wa mataifa makubwa duniani kwa kumteua mgombea ambaye sio mwenyekiti wa chama.

HABARI NDIYO HIYO
 
Luteni,

Ni kweli kwamba mnasubiri makapi ya CCM? Kuna tetesi hapa kwamba mgombea wenu wa urais atatoka miongoni mwa wabunge wa CCM.
 
Hivi inakuwaje wagombea wa nafasi ya urais mara zote ni wenyeviti wa vyama!?
 
Luteni,

Ni kweli kwamba mnasubiri makapi ya CCM? Kuna tetesi hapa kwamba mgombea wenu wa urais atatoka miongoni mwa wabunge wa CCM.
Tunayataka hayo hayo makapi kwani wao sio watanzania hata Dr. Slaa alikuwa makapi ya CCM, ukimkataa wewe wenzako wanamsubiri kwa hamu.
 
CHADEMA tuwape nafasi, tumsubiri watakayemleta tumhukumu kwa matendo yake na utendaji wake
 
mmh.. hawa CHADEMA nao... they better put someone decent wasilete vituko kama TLP wanatuletea some pastor eti awe Rais..wtf!
 
Success and failure are not measured by ends but by means or processes towards envisaged ends.
 
Mwaka huu utakuja na wengi tu na kuchokonoa kwa wengi, TULIA Abh.....or MS Chadema hawajasema


Hacha siasa zako za maji****** Taka umewaka picha ya kwanza ukaangalia upepo Now naona umekuja na prof Berugu baada ya kubadilisha ya kwanza
 
UKIWEZA JINYONGE, UKICHUKIA CHUKIA , UKILIA LIA. LKN HAMNA AWEZAE KUYAPANGUA YA MUUMBA WETU
"JK TU 2010"

Kwani inahusu?

Kumbuka pia "No one is irreplaceable"
 
Malaria sugu unachosha na unakera. Halafu leo umepitiwa kidogo mpaka saa hizi hujamsifia JK.
 
Prof. Baregu ni mtu makini, mwana mapinduzi na anafaa sana kuwa Rais. Tatizo ni kuwa hajajulikana kitaifa kwenye national politics. Bora agombee ubunge akae ndani ya Bunge at least 5 years ajenge jina halafu ndiyo agombee Urais. Chadema inaweza pia kumpa ubunge wa viti maalumu ili alete changamoto ndani ya Bunge.
Kwa mtaji huu bora Chadema imuunge mkono Prof. Lipumba wa CUF.
 
Safari hii vyama vinaweka mgombea mmoja tu ili kuiweka sawa Tanzania ,ikiwa hamna habari na mmefichwa kulijua hilo ,basi nawamegea.

Ili kuondokana na usumbufu wa CCM kujitwalia madaraka kirahisi na kuiendesha nchi kivuvuzela ,vyama vya siasa vimeamua au vitaamua kumuweka mgombea Uraisi kutoka Chama fulani kimoja ,nimepata tetesi kuwa kutakuwepo na ugawaji wa madaraka kwa serikali hiyo kuwapa vyama vingine iwapo ushindi utapatikana,siwezi kusema zaidi kwa sababu si msemaji wa tukio hilo.
 
Baregu: Natafakari kugombea urais

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (Saut) cha jijini Mwanza, Profesa Mwesiga Baregu, amesema anatafakari juuya nia ya kutaka kugombea kiti cha urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.

Akizungumza na Nipashe jana, Profesa Baregu alisema anayo nia ya kufanya hivyo na kwamba muda utakapofika ataweka bayana mambo yote kwa kuwa anazo sifa za kupigania kiti hicho.

“Sifa zote ninazo na muda ukifika nitafanya hivyo kupitia chama changu na endapo kitanipitisha, nitasimama na kugombea na wagombea wengine kutoka vyama vingine vya siasa,” alisema Profesa Baregu.

Chadema mwezi Mei mwaka huu kilitangaza ratiba ya wananchama wake kuchukua na kurejesha fomu katika nafasi za udiwani, ubunge na urais.

Kwa mujibu wa ratiba hiyo, wagombea urais walitakiwa kuchukua fomu kuanzia Mei hadi Agosti na kuwa wamezirejesha ifikapo Agosti 9, mwaka huu.

Katika chaguzi za mwaka 1995 na 2000, Chadema hakikusimamisha mgombea urais hadi mwaka 2005 kilipomsimamisha Mwenyekiti wake wa Taifa, Freeman Mbowe.

Hata hivyo, safari hii Mbowe amesema hatagombea nafasi hiyo na badala yake atakwenda kugombea Ubunge katika jimbo la Hai, mkoani Kilimanjaro.

Profesa Baregu aliliambia Nipashe kuwa hatarajii kuchuana katika nafasi ya ubunge katika jimbo lolote na kwamba sehemu anayoona anaimudu ni kwenye urais.

Alisema ikiwa atafanikiwa kuchaguliwa kuwa kiongozi wa nchi hii, atatekeleza mambo mbalimbali ikiwemo kukuza uchumi na kuondoa umaskini kwa Watanzania.

Kwa mujibu wa ratiba ya Chadema kuhusiana na mchakato wa uteuzi wa mgombea urais baada ya wagombea kuzirejesha fomu hizo Agosti 9, mkutano mkuu utakaa Agost 10 ili kupitisha jina la mgombea wake.
 
Back
Top Bottom