Nani kugombea urais 2015 Tanzania kupitia CCM?

DR Salim A Salim kugombea,naomba kutoa hoja!Wanaoafiki waseme ndiyooooooooo!
Siyooooooooooo! Salim hatagombea tena since JK amfanyie rafu 2005 na refa kutoiona ile rafu aliishajiuzulu mchezo wa kugombea ile nyumba ya magogoni.
 
Maana kusema ukweli mpaka hivi sasa hatuoni mtu yeyote wala dalili yeyote kama ilivyokua wakati kikwete akitarajiwa kuingia na jinsi mambo yalivyo tight,sijui nani atafaa?
kama unajua tafadhali niambie

Haa mkubwa kwani Raisi 2015 atatoka CCM tena sidhani kwa misingi gani?.
 
Tukiwa tunafanya maandalizi ya kupata Rais 2015 unahisi nani anafaa kati ya hawa kuwa Rais.

1. Edward Lowassa
2. John Pombe Magufuli
3. Wilbroad Slaa
4. Asha Rose Migiro
5. Freeman Mbowe
6.Ibrahim Lipumba
7. January Makamba
8. Bernard Membe
9. Mizengo Peter Pinda
10. Dovutwa Dovutwa
 
tukiwa tunafanya maandalizi ya kupata rais 2015 unahisi nani anafaa kati ya hawa kuwa rais.

1. Edward lowassa
2. John pombe magufuli
3. Wilbroad slaa
4. Asha rose migiro
5. Freeman mbowe
6.ibrahim lipumba
7. January makamba
8. Bernard membe
9. Mizengo peter pinda
10. Dovutwa dovutwa
kwanza toa magamba ili tuuone mti vizuri maana umeuliza swali ambalo limechanganyika na uchafu kwa hiyo toa magamba swali litaonekana vizuri
 
Wajanja hao na wanajua siasa mchezo mchafu. Kama walivyotudanganya na handsome 2005 wanaweza wakamweka Magufuli au mama Tibaijuka kutuaminisha tena kumbe wao watakuwa wanafunika makosa yao waliyoyafanya nyuma.
 
Tufanye kazi kwanza..si wakati muafaka sasa kufikiria urais 2015 wakati nchi ina matatizo lukuki hususan kuporomoka kwa thaman ya tsh ova dola,kupanda mafuta,umeme usio wa uhakika,bei kubwa za bidhaa madukani.
 
Kwa hali inavyozidi kubadilika kila kukicha sioni wa kumzuia Edward N Lowassa kugombea Urais kupitia CCM. Ila tu ni kwamba CCM itamegeka tu manake sioni Mzee 6 na kundi lake wakikubali na kuunga mkono ENL, nadhani watajiengua na kuelekea CCK kama si CDM!!
 
Back
Top Bottom