Nani kati ya hawa wanasiasa Chadema anafaa kuwa Raisi wa Tanzania?

Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Jun 9, 2011
6,808
6,500
Kadri siku sinazokwenda inajidhihilisha kuwa ni Vyama Vitatu tu ambavyo vina uewezekano usiopingika wa kutoa Raisi wa awamu ya tano Tanzania (CCM, CHADEMA NA CUF).

Nisingependa kuongelea Wagombea Uraisi binafsi mpaka hapo katiba mpya itakapo litambua hilo. Kwa kuanzia na hii toli (thread), ningependa mchangiaji utoe mawazo yako ya nani anafaa kati ya hawa Wanasiasa wa CHADEMA na sababu zipi zinakufanya ufikilie kama ana uwezo kisiasa wa kuwashinda wagombea wa vyama vingine ya siasa.

Pia kama unafikilia katika orodha hii kuna Mwanasiasa sikumtaja, tafadhali bandika jina lake na utoe sababu lakini kumbuka katiba ya Tanzania, Ibara ya 39, Ibara ndogo ya (1), kifungu kidogo (a-e ). Mwanasiasa lazima awe na umri si chini ya miaka 40 na haisemi lolote juu ya kiwango gani cha elimu, kwa maana hii, elimu siyo kigezo kinachomzuia Mtanzania kugombea nafasi ya Uraisi.

Nitatoa majina pia ya Wanasiasa wa vyama vya CCM na CUF katika toli(thread) nyingine ili wana janvi tuchangie.

Ikumbukwe dhumuni langu kuu siyo kupiga kura za maoni au kutoa kashfa zisizo zibitishwa bali ni kuchangia mawazo kuona ni jinsi gani sisi kama wananchi wa kawaida tungependelea awe kiongozi wetu wa Taifa.
Nitakuwa ninakusanya maoni kila baada ya saa sita usiku na kuona ni Mwanasiasa yupi wanamtandao mnafikilia zaidi kama awe ni kiongozi wa Taifa.

Janvi ni lako, litawaliwe na nguvu za hoja na sio hoja za nguvu.

Changia...

Freeman Aikaeli Mbowe-Mwenyekiti
Dk. Willibrod Peter Slaa-Katibu
Tundu Lissu-Mbunge(Singida Mashariki)
Philemon Kiwelu Ndesamburo-Mbunge(Moshi Mjini)
Prof. Kulikoyela Kanalwanda Kahigi-Mbunge(Bukombe)
Simon Peter Msigwa-Mbunge(Iringa Mjini)
Mabere Marando-Mjumbe wa Kamati kuu
John Magale Shibuda-Mbunge(Maswa Mashariki)
Joseph Roman Selasini-Mbuge(Rombo)
Mustapha Boay Akunaay-Mbunge(Mbulu)
Said Amour Arfi-Mbunge(Mpanda Mjini)
Prof. Mwesiga Baregu-mshauri wa kisiasa

Update: 3th July

Katika watu waliochangia mpaka usiku wa leo, Freeman Aikaeli Mbowe na Dr. Willibrod Peter Slaa wanafungana katika idadi ya watu waliopendekeza wawe Raisi wa awamu ya tano wakifuatiwa na Tindu Lissu, Peter Msigwa na John Shibuda

Jamvi bado liko wazi
 
Mkuu nadhani kwa sasa tuhangaikie tukio la Dr Ulimboka na mgomo wa madaktari. Mambo ya ugombea Urais kwa sasa hayana nafasi. Rais wa awamu ya 5 anajulikana ni Dr Wilbroad Slaa.Ya nini kupoteza muda kujadili hapa?
 
Sisi Rais wetu tayari tunaye mioyoni mwetu tunasubiri tu ifike 2015, wewe mtizamo wako ni upi kama mtz?
 
Mkuu nadhani kwa sasa tuhangaikie tukio la Dr Ulimboka na mgomo wa madaktari.Mambo ya ugombea Urais kwa sasa hayana nafasi.
Rais wa awamu ya 5 anajulikana ni Dr Wilbroad Slaa.Ya nini kupoteza muda kujadili hapa?

Mungu wangu wa Israel amlinde Rais wangu Dr. Slaa. Amen
 
Mkuu nadhani kwa sasa tuhangaikie tukio la Dr Ulimboka na mgomo wa madaktari.Mambo ya ugombea Urais kwa sasa hayana nafasi.
Rais wa awamu ya 5 anajulikana ni Dr Wilbroad Slaa.Ya nini kupoteza muda kujadili hapa?

Ndio anajulikana Rais kivuli wa Tanzania.
 
Sisi rais wetu tayari tunaye mioyoni mwetu tunasubiri tu ifike 2015

wewe mtizamo wako ni upi kama mtz?

Mtazamo wangu ninadhani Freeman Aikaeli Mbowe anafaa na ameonyesha uelevu na upeo mkubwa katika siasa ukilinganisha na kipindi alichogombea hii nafasi ya Uraisi.
 
Anayefaa kuwa Rais ni Prof Lipumba pekee kwa hali tuliyofikia hivi sasa, ukimkataa unasukumwa na UDINI NA UKASKAZINI.
 
Tuache ushabiki wa vyama na viongozi wao, kwani mstakabali wa nchi yetu upo kwa YEHOVA!
 
Kwangu mimi zitto kabwe anafaa. sina hakika kama 2015 atakuwa ametimiza miaka 40. Mwenye elimu na umri wake anijuze
 
Hebu tupe maendeleo ya dokta huko majuu!


Vyombo vya habari vya nchi za Magharibi huwa havizungumzii lolote kuhusu siasa za Africa achalia mbali siasa za Tanzania. Kuiona habari yoyote ya Tanzania mpaka jambo fulani la kihistoria au la kutisha litokee., ie Mauaji ya ajabu au raia wao apate tatizo akiwa Africa(Tanzania).
 
Freeman Mbowe watanzania tukimwanini naamini anatufaa sana kwani ameonyesha utulivu na ubunifu katika kutatua na kutoamwongozo wa nchi yetu.
 
Back
Top Bottom