Nani kama Mama Vs Nani kama Baba

Wote ni walezi wa familia lakini ilionekana ivo sababu mama ndiye aliyekuwa karibu na watoto, sikuzote na baba alikuwa mtafutaji chochote kihusucho familia na malezi ya watoto mama ndiye aliyehusika sana na ndio maana hata mtoto alipoharibika mama ndiye aliyelumiwa bila kujali alipitia mangapi.
baba alikuwa wa kuhakikisha chakula kipo,ada na mahitaji mengine na hata akipotea wiki nzima yeye anachojua aikute familia inaendelea vizuri na kwa baadhi majukumu yalikuwa tofauti wote watafutaji na bado mama alihitajika kuwa karibu ili watoto wakue katika misingi ipasayo.

Lakini siku izi maisha yamebadilika na huu msemo nguvu yake unaelekea kwisha imebaki mazoea tu ya maneno tuliyozoea kusema.

Najua sana maana ya kulea kwa sababu nafanya hivyo kila siku.
 
Hapo sasa umeongea la msingi. Uwe na wikendi njema.
 
now days utandawazi umewasaidia kina baba kujitambua na kugundua kuwa nao wana umuhimu kwenye malezi ya watoto wao
 
My people, you can't be serious! Yaani kila mwanaume anaweza kuwa baba? Kila mtu anaweza kuvaa uhusika wa baba mzazi kwa mtoto? Hakuna kama MAMA, hakuna kama BABA. Their roles to children are irreplaceable. Majukumu ya mzazi wa kiume/kike huwezi kuyakasimu kwa mtu yeyote. Kuna wakati mtoto anafanya ukorofi na ukaidi kiasi kwamba kama anayemlea si mzazi wake anaweza akadhani mtoto anamdharau kwakuwa siyo mzazi wake, na hatimaye kupunguza upendo kwa mtoto. Hivi mnajua mtoto anaanza kukua na kujengeka kisaikolojia akiwa tumboni kwa mama yake? Mwanamke mjamzito asipokuwa treated vizuri na mume wake, mtoto tumboni anaathirika, hii inaonyesha kina baba tuna umuhimu mkubwa sana hata wakati wa ujauzito.

Wanaume wenzangu nadhani mmewahi ku-date wasichana wenye 'dad issues', ni wasumbufu balaa. Wengi wanakuwa diehard feminists. She will blame you for every mistake her dad did decades ago. Hii inaonyesha majukumu ya baba mzazi ni muhimu.

Kuna wakina baba wenye kasoro zao (kutelekeza familia, kukataa watoto, nk) na kina mama(kutesa watoto,kuzaa na kutupa watoto, kutelekeza) wenye kasoro vilevile.Kusema mama ni muhimu kuliko baba ni sawa na kusema kuku alitangulia ndo likafuata yai. Ni kitendawili. Naamini mtoto yeyote aliyelelewa na single parent, kuna kitu anapungukiwa, hata kwa kiasi kidogo.

Ukweli ni kwamba mtoto anakamilika akipata malezi mazuri ya baba na mama. Baba yangu uko juu, hakuna kama wewe, umenipa dira ya maisha. You have taught me how to be a man. Mama hakuna kama wewe, umenifundisha upendo na kuwaheshimu wanawake.

Mimi Wazazi wangu wote ni mashujaa wangu na nawapenda wote sawa sawa kwani walishiriki kikamilifu katika malezi yangu tangu nikiwa sina akili mpaka pale nilipopata akili ya kutambua juhudi za wazazi wangu katika malezi. Nilizithamini sana juhudi zao kubwa za malezi ili kuhakikisha kwamba nakuwa raia mwema na pia very productive katika jamii ya Walimwengu. Sasa nimekuwa mtu mzima nikikumbukua miaka ya nyuma zile juhudi zao kubwa za kila siku iendayo kwa Mungu sina cha kusema zaidi ya kuwapa shukrani zangu nyingi sana. Kwani mafanikio yangu yote kimaisha yasingewezekana bila juhudi zao kubwa sana. Kwa hiyo kwangu mimi naomba tu niseme NANI KAMA WAZAZI!
 
Sasa hapa wajameni,

hii issue ya hakuna kama mama au baba inategemea na malezi, mazingira pamoja na utamaduni mtu aliokulia

kwa maelezo ya wengi hapa, umuhimu wa mzazi mmojawapo unategemea na perception ya mtu mwenyewe dhidi ya mzazi. Obviously, kwa mtu aliyelelewa vizuri na baba kuliko mama and vice versa atakuwa anamwona mmojawapo kuwa ni muhimu zaidi ya mwingine

Nikimbilie kusema kuwa "nani kama mama" ilikuja katika muktadha wa nafasi ya mama katika kuzaa na kubeba mimba, yakionekana ni majukumu adhimu kabisa kwa mwanamke.

Lakini kadiri siku zinavoenda, na walivokwisha kusema wengine, mwanamke huyu huyu ameyabemenda haya majukumu (kama kutoa mimba, kutupa vichanga, kutokunyonyesha ipasavyo nk) na hivyo kuondoa ile stahiki ya kuitwa 'nani kama mama'

Pia tukubaliane na ukweli kwamba kwa tamaduni zetu majukumu yametenganishwa vizuri kwamba mama afanye nini na baba afanye nini katika mazingira ya kawaida

Hivyo basi, kusema kuwa NANI KAMA MAMA au NANI KAMA BABA sio sahihi wote wana umuhimu wao wa kipekee.
 
Baba anamfanya mama asimame aweze kulea watoto kwa ukaribu.......pia baba analea watoto....
Katika sumaku....ni ncha ipi muhimu zaidi?
Kama ilivyo hakuna kama mama...na hakuna kama baba....
ODM hebu funga hii kitu..
 
Kwa upande wangu mama na baba hakuna aliyejuu ya mwenzie kiupendo ktk moyo wangu ksb ,
natambua umuhimu wao,upendo wao,mafundisho yao wote wawili ktk malezi yangu,
kila mmojawao ana umuhimu mkubwa sana sana kwangu, kwa hiyo
msemo wa nani kama mama nautambua na kuuthamini sana,lakin pia
nani kama baba ni muhimu sana kwangu, na siamini kama mwanaume yoyote anaweza kuwa baba yangu,
baba yangu hana na hatatokea mbadala wake, atabaki kuwa baba yangu,
na naamini kuwa baba yangu ni baba bora zaid kuliko wote hapa duniani,
pia mama yangu ni mama bora zaidi kuliko mama wote hapa duniani.
Pasipo baba yangu mimi nisingekuwepo leo,vivyohivyo pasipo mama yangu mimi nisingekuwepo leo.
Nawapenda sana wazazi wangu wote wawili ,nawapenda zaidi ya nitamkavyo kuwa nawapenda.
 
mimi wazazi wangu wote ni mashujaa wangu na nawapenda wote sawa sawa kwani walishiriki kikamilifu katika malezi yangu tangu nikiwa sina akili mpaka pale nilipopata akili ya kutambua juhudi za wazazi wangu katika malezi. Nilizithamini sana juhudi zao kubwa za malezi ili kuhakikisha kwamba nakuwa raia mwema na pia very productive katika jamii ya walimwengu. Sasa nimekuwa mtu mzima nikikumbukua miaka ya nyuma zile juhudi zao kubwa za kila siku iendayo kwa mungu sina cha kusema zaidi ya kuwapa shukrani zangu nyingi sana. Kwani mafanikio yangu yote kimaisha yasingewezekana bila juhudi zao kubwa sana. Kwa hiyo kwangu mimi naomba tu niseme nani kama wazazi!

nakuunga mkono 100% hapo kwenye blue.
Asante sana.
 
"Hakuna kama mama". Huu ni ubaguzi binafsi kwa wamama dhidi ya wababa. Then haishii hapo kwani hata hao wamama huendelea kubaguwana wenyewe kwa wenyewe, ndio unasikia "Mama wa kambo si mama".
Kwanza kabla/baada ya kusema "nani kama mama au nani kama baba" weka neno "INATEGEMEANA MTU NA MTU". Kwa maana ya kuwa siyo wote wanawakubali mama/baba kuliko wanavyowakubali baba/mama.
Na sidhani kama kuna mtu atanipinga nikisema kuwa mapenzi ya mtoto wa kiume zaidi yapo kwa mama kuliko kwa baba. Na mapenzi ya mtoto wa kike zaidi yapo kwa baba kuliko kwa mama. (Na nikisema mtoto hata kama una mvi bado wewe ni mtoto mbele ya baba na mama yako, ila nisifikiriwe kuwa naongelea mtoto kwa maana ya aliyeko primary saivi).
baba = mama
 
Hii inategema nani ameonyesha upendo/malezi ukaribu na watoto

mfano mie ninasema nani kama mama kwa vile natambua /mapendo na
uwepo wa mama yangu toka nilipokuwa mdogo mpka sasa katika maisha yangu
sikuwahi kupata malezi/mapenzi yoyote kutoka kwa baba yangu, baba alitutelekeza tukiwa wadogo kwenda kuoa mke mwingine kule waliwapenda sana watoto wake
hata nilipokutana nao waliniambia wanampenda baba kuliko mama yao.
lakini kwa upanda wangu siwezi kamwe kusema nani kama baba sina hata
chembe ya mapenzi kwake

Umuhimu wa Baba unadhihirika zaidi kwenye familia za "wajane".
Najua ujane ni hali ya pande zote, lakini katika hali halisi imekuwa kama wajane ni wakina mama tu!
Mwezi uliopita kanisani kwetu tulizindua mfuko wa ustawi wa jamii, ambao utashughulika na wajane na yatima.
Hivyo ilibidi wajane wote wajiorodheshe, wajane wote waliojitokeza ni wakina mama tu.
Hapa ndio mchango wangu ulipo, kwamba kwenye familia za namna hii, ukweli utaendelea kuwa "HAMNA KAMA BABA"
 
Back
Top Bottom