Nani kama housegirl sio nani kama mama

mhugo hantish

Senior Member
Apr 21, 2015
135
33
J
691a742096622840e5172d703652975f.jpg

Habari ndugu wadau? Napenda kuileta mada yenye kichwa husika hapo juu. Siku hizi wazazi wengi wameanza kuwasahau wana wao na kusahau majukumu yao. Hali hii imepelekea kuwafanya watoto walio wengi kukua vibaya na kuyakosa malezi ya mama mzazi licha ya uwepo wa asilimia kadhaa ya watoto wanao lelewa vizuri ukilinganisha na hapo kale. Leo hii mtoto akizaliwa tu anaachwa na house girl. Mama anakua na majukumu mengine ya kikazi na utafutaji hasa kwa kipindi hiki ambacho uchumi umepanda ngazi. Kwa jinsi hiyo mtoto hujikuta kuyakosa malezi ya mama hata afikiapo umri wa kujitambua.
Sasa hebu tuangalie hapa. Sahizi idadi ya mahouse girls inapungua na idadi ya wasomi inaongezeka. Hii inamaana kua kila mzazi anamlea mtoto akimuandaa Kuwa msomi na si mlea watoto. Je, baada ya karne moja nchi hii itakua na walea watoto? Na kama jibu ni hapana tutawatunzaje watoto wetu watakao zaliwa hiyo karne?
Kuna hatari ya kuwasababishia wanetu lishe hafifu/afya duni.

Nina mengi ya kusema ila niishie hapa kwa leo.
 
Tutawaajiri bibi na mama zetu (kiumri) kama wanavyofanya mataifa mengine.
TZ kuna ajira nyingi sana za watoto hasa majumbani.
 
usiwe unaangalia mambo kwa jicho moja ,ulaya na malekani wameendelea lakini kuna mahouse gal
kilichopo ni kuwa kazi hiyo itapata dili sana na itakuwa na mshahara mkubwa kwani itafanywa na watu waliomaliza form four na wakafeli
 
usiwe unaangalia mambo kwa jicho moja ,ulaya na malekani wameendelea lakini kuna mahouse gal
kilichopo ni kuwa kazi hiyo itapata dili sana na itakuwa na mshahara mkubwa kwani itafanywa na watu waliomaliza form four na wakafeli
Ma house girl wengi wa ulaya wamekuwa imported kutoka mataifa ya Asia kama india, Nepal na kwingine. Labda na sisi pia tuta import kutoka kwa mataifa mengine. Ila uhakika ni kuwa itafika mahali hii kazi itaheshimika na itakuwa na mshahara mkubwa kitu ambacho wengi hawataweza kutokana na vipato vyao. Kwakweli maisha yamekuwa sio rafiki kwa watoto wetu, jukumu la msingi waliloumbiwa wanawake limeachwa mikononi mwa house girls, wao sasa wanatekeleza jukumu la wanaume la kuhakikisha wanaleta mkate wa kila siku nyumbani.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom