Nani kafumaniwa

usikilize moyo wako,kwani wewe ndio unaeweza kutoa msamaha,na ndio ulieona kwamacho yako vitendo alivyovifanya, kama umeona anastahili kusamehewa sawa ....
hana ubavu wa kuacha......angekuwa na uamuzi huo saaa hizi ingekuwa siku nyingiiiiiiiii kila mtu kivyake.
 
kama alivyosema arabianfalcon usikilize moyo wako.

Kumuacha ama kuendelea ni jibu ambalo unalifeel mwenyewe kwenye moyo na mifupa
 
kitu gani kilikufanya hadi ukapatwa na machale ukaamua kurudi pale club? humwamini mtu wako??

Wakati ananipigia simu kunitakia usiku mwena alionyesha wasiasi fulani hivi. Nina mazoea ya kwenda kwake ila huwa namtaarifu kuwa nakuja. sasa aliponipigia simu kujua kama naenda nikamwambia siendi. Nilibana pale club kusubili muda upite ili nim-suprise kwenda, kumbe ndo Mungu ananiongoza kuona niliyoyaona.
 
Tatizo la vijana (wachangiaji wengi kwenye hii post), mnajaribu ku-over-act badala ya kufikiria kwa ukaribu zaidi...

Huyu in MCHUMBA (probably - mke mtarajiwa): Huyu binti siyo MKE wa Chimps: Huyu anayo maisha na matarajio yake kama alivyo Chimps: Huyu binti anao uhuru wa kwenda kokote atakako na kujumuika na marafiki zake bile Chimps kuwapo (hawana mkataba hawa wawili so far):::

Kama ilivyo kwa Chimps: akishampatia "lift" na kumfikisha kwake, na yeye Chimps anapitia Rose Garden, Corner Bar, au kwingineko nakujumuika na marafiki zake (bila kumhusisha huyu binti - ni uhakika na hilo):::

Kwahiyo "at this stage" hakuna ambaye "anammiliki" mwenzake - Kumlipia Kodi, Kumsomesha, e.t.c ni mambo unayotenda kwa sababu unamjali (siyo kumpenda - although inawezekana) kama rafiki yako wa karibu na siyo kama "MKE" wako... Wengi tuliochumbia muda mrefu - tulilipa sana KODI, Tulisomesha mpaka ndugu za wachumba, e.t.c - Na wengine hatukuweza kuwa nao kwa sababu mbalimbali - BUT - hatukujilaumu, kwa maana hatukuwa tunatenda hayo kama "UWEKEZAJI"...

Ushauri: Ukimkuta "MCHUMBA" wako mahali (kwenye starehe) bila ya kuwa mmetaarifiana kabla, the best thing you can do ni kusalimiana (possibly na kutamblishana kama anayo kampani yake) basi... Baada ya hapo kila mtu anachukua "time"... Kama "nafasi ipo" mnaweza kujumuika pamoja katika kustarehehe, otherwise, peaneni nafsi ili mpate kufahamiana vizuri!
 
Hiyo kaka ni ajali tu sasa ajali ikitokea wapo wanaosema wamelogwa na wapo wanaosema ni uzembe na haufai kunyamaziwa, ila ajali ni ajali kwa kila mtu iwe umelogwa au bahati mbaya. Samehe tu kwa roho nyeupe wewe jiaminishe kuwa wale ni kaka zake ili usipate shida kimawazo.
 
Pole ndugu yangu umeshaonyeshwa mapema makucha yake alio yaficha na hiyo ndio tabia yake kubwa alikuwa amejivisha ngozi ya kondoo kumbe ndani ni chui. Ukitaka kumjua tabia yake zaidi jifanye umesahau then siku unaibuka kwake hata saa 7 usiku utajionea mengi zaidi ila usiende na kale kamguu ka Ismail Rage maana tutakupoteza humujamvini.

But shukuru Mungu kwa kila jambo amekuonyesha hili atafungua jingine zuri zaidi
 
Kama unataka kugeuka kaburi wakati siku si zako endelea nae!


Ni saa kumi na mbili jioni natoka kazini, nampita demu wangu ili nimpeleke kwake na mimi nirudi zangu kwangu.
Mara ananiambia nimpitishe mahala kuna club fulani karibu na kwake akachukue mzigo wake fulani kwa rafiki yake. Nafanya hivyo na tulipofika nje ya hiyo club nikapokea simu inayonilazimu nirudi ofisini. Hivyo tukakubaliane achukue mzigo na aende nyumbani maana mimi narudi ofisini. Nimekaa ofisini mpaka saa mbili usiku, akanipigia simu kuwa ameshalala na akanitakia usiku mwema. Nami nikamweleza kwamba ndo naelekea kwangu. Ila machale yakanicheza ikabidi nipite kwenye ile club, nika-paki gari mbali kidogo, nikaingia ndani ya hiyo club nikaagiza maji na kijichimbia kenye kona fulani ina kagiza.
Mtumeeeeee!!!, baada ya dakika kumi hivi sikuamini macho yangu kumuona demu huyohuyo anaingia akiwa ametinga pedo laini, mapaja yote nje. Akaenda kukaa meza moja walikaa mabrother men na baadhi ya mademu. Kilicho niuma ni brother men mmoja kumpokea kwa busu, wakakaa then demu akawaamemkumbatia huyo brother. kweli roho iliuma kinoma. Nikawaacha waendelee na mishemishe zao, mara wanyanyuke wasindikizane nje, waende kwenye gari kutafuta koti na mengine.
Ulipopigwa mziki wa hakunaga, meza yao wote alinyanyuka na kuanza kusakata rumba. At around saa nne na robo wakawa wameshakolea kilevi. sasa wakati anasakata rumba gafla demu kaniona nikiwa kona nimekaa nami namuangalia. Nguvu ya kucheza iliisha, akaangalia chini kwa aibu, akaja kunifuata. kuja tu nikamzuia asinifuate aendelee na starehe maana mimi sijamuita. then mimi nikaondoka zangu.
sasa najiuliza maswali yasiyo na majibu
1. Kuna haja ya kuendelea naye
2. ananiambia wale ni kaka zake, je kaka kwa staili ile, na alitegemea kulala wapi maana nyumba anayoishi geti linafungwa saa nne kamili.
3. nilikuwa namlipia masomo ya kuendeleza shule yake, je niendelee au ndo mwisho??
4. nyumba anayoishi nailipia mimi maana mimi kwangu nakaa na wadogo zangu na hatujaanza kuishi pamoja, je nitaendelea kulipa


Naomba ushauri,

Chimps
 
Usiku mwema mm nalala, alafu unamkuta Club, then anakwambia kaka zake. Je ni dhambi kutoka na kaka zake? kwa nn asikuambie ukweli? Ukiukubali uongo siku za kwanza wakati wa urafiki, basi uwe tayari kudanganywa siku zote hata mtakapooana. Maswala ya mapenzi ni ya wawili, pima mwenyewe maana wewe ndiye uliona kila kinachoendelea. Kama ni kaka kweli ama anakuzingua. Fanya maamuzi yaliyo sahihi ambayo hayatakuumiza huko mbele ya safari.
 
hapo hakuna kitu mkuu,kimbia upesi sana, wewe unaingia gharama wenzio wanatafuna buure!
 
da kaka una bahati sana ulimfumania live,wengine wanabaki kuhisi tu....sepa fasta unaweza letewa magonjwa ukajuta....demu unatakiwa umsomeshe ukishaoa,statistics are not favourable kwa wale wanaosomesha kwenye uchumba
 
Kimbia utakufa siku si zako kahaba huyo..gold digger na nafahamu tayari umepunguza imani kwake la muhimu chapa lapa angalia maisha yako
 
Back
Top Bottom