Nani kafanyia taifa makubwa kati ya awa?

nyie hamjui kuwa kikwete ni potezapoteza...anataka watu wasahau matatizo aliyoyasababisha kwa udhaifu wake kiuongozi. Anatafuta coverage mpya. Bado haamini kuwa watz hawadanganyiki kirahisi hivyo.

Duh unakoelekea sasa! Kumbe tunapigwa changa la macho sio?
 
umewataja remmy na moshi kwa mtazamo wako lakin wapo wanaomuona kanumba kama shujaa. Ofcoz kwa upande wa umaarufu kwa jamii nzima kanumba ni zaid ya hao uliowataja anajulikana kwa lika zote lakin nenda kakaulize kanafunzi ka darasa la pili kama kanamfahamu tx moshi au dr. Remmy.

Hapo kwenye red... Jumapili nilikuwa kwenye Daladala moja mzee mmoja ambaye naye alikuwa abiria kama mimi alizua kicheko kidogo baada ya kuuliza abiria wenzake kuwa anasikia kanumba kafa ndo yupi yule mnene au mwembamba?... sasa sijui anarelate vyovyote na hapo kwenye red?
 
Hapo kwenye red... Jumapili nilikuwa kwenye Daladala moja mzee mmoja ambaye naye alikuwa abiria kama mimi alizua kicheko kidogo baada ya kuuliza abiria wenzake kuwa anasikia kanumba kafa ndo yupi yule mnene au mwembamba?... sasa sijui anarelate vyovyote na hapo kwenye red?

Jamaa anataka kutuingiza chaka, anataka kutuaminisha kuwa KANUMBA anajulikana na kila mtu wakati siyo.
 
serikali imeniboa mpaka basi! au ndo mambo ya freemasons at work?

Hawa woote wanacheza, kuna Marehemu Mzee Kipara wa Kigamboni, aliumwa mpaka akafa bila msaada wa serikali wala ajuza yeyote zaidi ya michango ya wasamaria wema. Hii nchi inaongozwa kwa hisia. Na ndio maana bwanamkubwa alienda South Africa huku tunafukutwa na giza na Jairo na akaenda Davos tukiwa na mgomo wa madaktari, lkn kwa kifo cha muigizaji, safari zake za kutalii zilikatishwa.
 
Kila fani ina kinara wake na anayechukuliwa kama shujaa, ukitaka kuitendea haki hoja yako mlinganishe marehemu na waigizaji walotangulia mbele ya haki. Kumlinganisha na wasanii wa fani nyingine mizani inagoma. Achilia mbali mapungufu ya kibidamu the guy deserve the name "the great" kwa tz. Nani zaidi yake?

Okeeeeey! Kwa hiyo huyu ndio alikuwa kinara wa kubandua vibinti U20?

He was Great and Guilty
 
kuna waanzilishi wa hii sana na hawajazikwa ivyo! mzee jongo?

Mkuu kuna kitu kinaitwa mvuto kwa jamii na mwamko wa tasnia yenyewe kwa nyakati hizi. Wakina mzee Jongo walifanya kazi kubwa ila tasnia yenyewe haikuwa na mvuto kama sasa. Pia Kanumba alipendwa sana na rika la watoto na vijana na wakina mama. Inawezekana wewe sio mpenzi wa hizo bongo movies lakini kuna watu wanazinunua kama karanga na kwa kuwa lugha ya kigeni (english) ni tatizo hizo za kiswahili ndo zinakuwa na mvuto zaidi.

japo unasema serikali inapendelea, lakini hata serikali yenyewe imechemka kuuandaa hapo leaders kwa wingi wa watu waliokuja na ambao hawakuletwa kwa na mafuso kama mikutano ya vyama flani. Watu walikuja wenyewe kiroho safi, na sijui unawazungumziaje hawa?

Japo kuna watu wanasema ni style ya Free masons lakini ni ngumu kudhibitisha hilo maana hawa watu huwa hawajisemi na mwenye kutoa uhakika wa hili lazima na yeye awe member kwa hiyo tunabaki kuamini kuwa Kanumba kazikwa na watu wa kawaida.

Suala la Lulu kuwa under 18 ni vigumu kumlaumu marehemu maana kwenye mapenzi ya siku hizi (sikiliza wimbo wa Single Boy- Alikiba ft Lady Jaydee) kuulizana umri ni ngumu sana na huyo dogo ameanza mambo ya mahaba kwa mda mrefu sana na wote tunajua.

In short, Kanumba alipendwa sana na hata kama serikali isingesaidia kuna watu wangekufa pale uwanjani au makaburini
 
Hawa woote wanacheza, kuna Marehemu Mzee Kipara wa Kigamboni, aliumwa mpaka akafa bila msaada wa serikali wala ajuza yeyote zaidi ya michango ya wasamaria wema. Hii nchi inaongozwa kwa hisia. Na ndio maana bwanamkubwa alienda South Africa huku tunafukutwa na giza na Jairo na akaenda Davos tukiwa na mgomo wa madaktari, lkn kwa kifo cha muigizaji, safari zake za kutalii zilikatishwa.

Masikini Mzee Kipara! Umenikumbusha mbali sana
 
Dkt Remmy Ongala aliwai kutoa nyimbo inayoitwa DUDE KWA SOKSI ambapo dhima ya nyimbo hii ilikua ni kuhamasisha matumizi ya Condom lakini cha kushangaza serikali iliipiga vita na kuifungia nyimbo ile, sasa chakushangaza leo hii matangazo ya Condom yanatolewa mpaka chekechea.
Kama ni kuitangza TZ nje ya mipaka yetu, Remmy Ongala alisumbuliwa kwa swala la uraiya lakini ni Msanii wa kwanza kufanya kazi TZ na kupata tuzo za kimataifa zilizoitangaza TZ.
 
Sikatai umaarufu, nataka kujua kalifanyia nini taifa mpa azikwe kitaifa?

Mojawapo ya kitu alicholifanyia taifa ni pamoja na kuongeza ajira maana kazi zake zimetengeneza ajira nyingi sana na pato la taifa limeongezeka kupitia kazi zake, lakini pia tourism sector kwa kiasi fulani ameweza kuitangaza Tanzania hata bila kupewa malipo ya advertising agent, yote hayo ukiyaangalia kwa umakini utagundua kuwa Kanumba amefanya mengi kwa TZ.
 
Dr remmy Ongara, Kanumba na Tx William Moshi? kwa upande wangu Dr remmy na Tx Moshi wamefanya makubwa kuliko Kanumba na wangefanyiwa kama Kanumba, maana sijaona cha ajabu alichofanya kuwazidi hawa jamaa! Serikali ina upendeleo! sijafuraishwa na ubaguzi wa Serikali. Remmy na Tx wametunga nyimbo nyingi za kufundisha na kuelimisha jamii ambazo zinasikilizwa na kila rika mpaka sasa, Je Kanumba kafanya nini mpaka Serikali kugharamia msiba wake na tena rais kuhairisha safari yake kisa Kanumba! kweli kuna mantiki? Tv zinashindwa kuonyesha matukio muhimu ya kitaifa na ya kujenga nchi, chakushangaza hata TBC wanakatisha bunge wanatuletea mazishi ya KANUMBA! kweli tanzania ni zaidi uijuavyo! Sipendi ifike atua niichukie Serikali. Ebu badilikeni jamani na fanyeni vitu vya Msingi, Watoto wanakaa chini, hospital hazina madawa, wafanyakazi wanalipwa mishahara midogo, umeme tabu hata kulipa IPTL ni shida then mnatumia Kodi za wananchi kuendeshea msiba wa KANUMBA! Au Serikali imelogwa? Bila marehem MZEE KIPARA nani angemjua KANUMBA. Mbona mzee kipara tena mwanzilishi wa maigizo hakufanyiwa hivyo?

Chezea freemason wewe!!
 
Freemasons ndio wanaocontrol media wao wakikipa kitu airtime lazima kitapendwa namiss sana Ambilikile Mswapile
 
Back
Top Bottom