Nani huyu Ridhiwani Kikwete?

Ningependa kutoa ushauri kwa Pres. Jk kuwa ni bora awe anafuata mifano iliyohai mfano watoto wa JK Nyerere hawakuwa kimbelele ktk majukwaa ya siasa kwani ni hatari kwa nchi iwapo kutatokea na uhai fulani na hata watoto mkapa naye pia aliweza ku-play low juu ya watoto huo ndiyo uongozi bora mkuu wetu!
 
Kwa nini unasema Ridhwani atakuwa na wakati mgumu baada ya baba yake kumaliza kipindi chake ha URAIS mnamo 2015?

Nafikiri kwasababu aliweza kuongeza CV yake pale baba alipokuwa waziri wa mambo ya nje (kupata vi-trip vya uwakilishi) na raisi (kupata cheti cha uwakili bila kufanya mtihani halali) hivyo basi baba akiondoka madarakani kutakua hamna favor tena itamlazimu kutumia juhudi binafsi: labda Rostam au Lowassa awe rais. Ni mtizamo wangu tu huo.
 
He has a done a very early political journey !...that I agree, he is a committed ccm member ! That has no doubt.....hongera Riz1.

Whether this is true or not, I still can not figure out why is it necessary for someone to know him if your not a member of the green party?
 
Basically I feel sorry for the boy, because the same thing that he thinks will get him kwenye 'KITI CHA ENZI' is what will prohibir him from the same. Because Kikwete is going to have such a shit legacy (and unless there is somekind of religious conflict in the next 25 years).. Kikwete will f@ck up and have no legacy and as a result he will never get a chance. He's screwed before he even begins... TOO BaD.. If your father is President, make sure its GHANDI...lol not Mobutu or STALIN..

Sidhani kama anajinsi maana hamna kazi nyingine anaweza fanya zaidi ya siasa. Ikumbukwe kuwa kwenye kupata uwakili amebebwa hajafanya mitihani (hii sio tetesi nina ushahidi tosha-hii sio siri hata mstaafu Jaji Ramadhani anafahamu hilo) That being said itakua vigumu kwake ku-practice law wakati hana knowledge yakutosha. Ingekua mtu smart kidogo unaweza kumpatia crush course lakini kama akili zake ni kama za baba he has no choice zaidi ya Siasa.
 
CV yake si ndefu hivyo

Ni mtu ambaye ameishi nakuogelea ufisadi muda mrefu kuliko vijana wengi. Tabia zake zitakuwa chafu kama baba yake. Hii ndiyo CV yake kamili
 
Chief, kwanza asante sana kwa kuleta mada kuhusu Ridhiwani Jakaya Mrisho Kikwete. We're strong applause you for that. Baada ya kusema hayo, ndugu zangu wengine JF is a place of great thinkers, we drill things to the bottom.

Chief, CV ya Ridhiwani uliyotulitea hailezei chochote cha kustusha na imeacha vingi tuu ambavyo bado Watanzania wengi wana maswali navyo. Ieleweke ya kwamba Ridhiwani ni product of Nepotism and favoritism nothing less nothing more. I will defend the argument based on different reasons.

Kwanza, Kushiriki kwake kwenye mikutano hiyo mliyotaja hakumpi any qualification of be or become a potential leader. Baba yake nadhani ametembelea nchi nyingi than any president in Tanzania history, yet he is the worse president than ever in Tanzania history. Habari ya kwamba ameanza chipukizi akiwa na mwaka moja doesn't make him a leader, habari ya kwamba alikuwa sijui nini au nani Daruso doesn't make him a leader. We need substance, amefanya nini Bagamoyo?

Pili, naomba utuelezee kwa nini Ridhiwani aliajiriwa na Masha. Na jee can you separate kuajiriwa kwake na Masha na kupewa uwaziri kwa Masha na Baba yake. Vile vile kutokana na vigezo vya Masha Firm nilazima uwe na high graduate scores ili uweze kufanya internship, Jee unaweza kuprove wrong sisi tuna argue kwamba Ridhiwani hakumaliza degree na high score? Jee how can you separate Nepotism and this?

Tatu, ni uelewo wangu kwamba Ridhiwani ni Mjumbe wa UVCCM, na kuna wajumbe kadhaa (i think) ndani ya UVCCM, sasa ni kwa nini yeye anakuwa kwenye decision point zote za juu za UVCCM? Jee anatumia jina lake kuifluance maamuzi ndani ya UVCCM?

Nne, Juzi ametoa tamko kuhusu CDM and Arusha saga. Lakini hajatoa tamko kuhusu Dowans, hatajotoa tamko kuhusu IPTL, ajatoa tamko kuhusu EPA, ajatoa tamko kuhusu katiba bomu inayompa baba yake madaraka ya kugawa nafasi kwa kina Nape, ajatoa tamko kuhusu wizi wa kura. Mbona hajatoa tamko kuhusu UMASIKINI uliokithiri Tanzaina. So, is he in favor of CCM or the development of Tanzania? Tushauri kimoja tuu ambacho Ridhiwani anaona CCM are wrong on it and he stand like a men with the balls and condemn it. Tell us, is it EPA, corruption, poverty? What is it?

Tano, Jee Ridhiwani amesaidia NINI BAGAMOYO? To my understand Bagamoyo is one of the bottom of the bottom places in Tanzania. The statistics shows every worse number you can imagine concern the place, now convince me what did Ridhiwani achieved in Bagamoyo. Please don't shout kwamba aliwapa watu mitaji.


Mwisho, we need substance and not speeches. We all knows that Ridhiwani is bogus like many elites kids who were raised in the suburbs of Oysterbay. He never achieved anything based on hard working and determination. We want to hear things which have influence and effects to Tanzanian. Sio kutuambia ameshiriki mikutano, who cares.... Baba yake ametembelea nchi mia kidogo, and yet Tanzania is the poorest country on earth.
 
He never achieved anything based on hard working and determination.

Mkuu hapa ndipo busara zinapokua zinaongeza CV ya mtu......, above all sijawahi kusoma publication yeyote ile ya Riz1 anbayo angalau inaweza kutoa mwangawa maendeleo kwa wananchi ......... but he is instead proclaim his greedy ambitions...... he is nothing ... i can compare him with a "parrot"
 
Basically I feel sorry for the boy, because the same thing that he thinks will get him kwenye 'KITI CHA ENZI' is what will prohibir him from the same. Because Kikwete is going to have such a shit legacy (and unless there is somekind of religious conflict in the next 25 years).. Kikwete will f@ck up and have no legacy and as a result he will never get a chance. He's screwed before he even begins... TOO BaD.. If your father is President, make sure its GHANDI...lol not Mobutu or STALIN..

Naona Kijana anajilinganisha na John Mashaka.... Sasa huu ndio wasifu wao respectively,

Rishiwani Kikwete
LLB (UDSM),
Expirience UVCCM/Legal officer

Vs.
John Mashaka
Bsc, MBA, JD
Expirience :Investment Banker/Economist
 
Know one can write this unless he is Ridhwan Himself

Mbaya zaidi umekuwa kama wasifu wa marehemu!! unajichulia dogo,

Tunachojua ni kuwa ulikua na nafasi nzuri ya kuonyesha uko tofauti na baba yako, Okonkwo alifanya hivyo!! umeonyesha wewe na baba yako akili moja, kumbuka baba yako anamaliza urais 2015 tu, baada ya hapo, pray that opposition wont win! wakishinda dogo una wakatii mgumu sana.

usije sema sikukueleza

pal... maneno mazito sana haya
 
Mkuu hapa ndipo busara zinapokua zinaongeza CV ya mtu......, above all sijawahi kusoma publication yeyote ile ya Riz1 anbayo angalau inaweza kutoa mwangawa maendeleo kwa wananchi ......... but he is instead proclaim his greedy ambitions...... he is nothing ... i can compare him with a "parrot"
tangu nizaliwe sijawahi kuona cv inaandikwa hivi...

lazima mimi mshamba
 
habari za leo wajukuu zangu?

ni kwa kipindi kirefu kweli nimeshuhudia huu mjadala juu ya huyu kijana mwenzenu! kama ilivyo ada yangu, leo nimeamua nijitokeze tena; pamoja na mambo mengine mengi ambayo yametokea hapa karibuni na mwaka huu mpya leo nataka nieleze kwa ufupi juu ya huyu kijana na jinsi ninavyo mjua mimi.........

RIDHIWANI KIKWETE,kama wengin wanavyomjua alizaliwa katika hospital ya wilaya ya bagamoyo tarehe 16 mwezi wa NNE mwaka 1979. kijana huyu alizaliwa toka kwa mama AZIZA bint SABURI na baba JAKAYA MRISHO KIKWETE.

RIDHIWANI ni kijana wa kwanza kwa wazazi hawa na alifuatiwa na mdogo wake anayejulikana kwa jina la SALAMA ambaye kwa sasa ni daktari na mwalimu pale MUHIMBILI chuoni.

kijana huyu alianza shule ya msingi mwaka 1987 pale shule ya msingi MATANGINI,nachingwea mkoa wa LINDI.sababu kubwa za yeye kuanza shule huko ni kazi aliyokuwa akifanya baba yake kipindi hicho. ikumbukwe kuwa bwana Kikwete alikuwa katibu wa CCM ,wilayani hapo. mwaka mmoja baadae, bwana ridhiwani na baba yake waliamia MASASI,mkoa wa MTWARA.akiwa huko alijiunga na shule ya MKOMAINDO kwa masomo yake ya darasa la pili kabla hawajarudi DAR ES SAALAAM, mwaka1989 ambapo alijiunga na shule ya FORODHANI iliyopo maeneo ya posta ya zamani hadi alipomaliza darasa la saba.

masomo ya sekondari aliyapata katika shule ya SHAABAN ROBERT na baadae MKWAWA mkoani IRINGA kabla ya kurudi DAR ES SALAAAM kwa ajili ya elimu ya juu katika CHUO KIKUUU CHA DAR ES SALAAM, sehemu ya mlimani na baadae ENGLAND,kwa masomo ya cheti cha elimu ya juu.

KISIASA
kisiasa kijana huyu alianza akiwa mdogo sana.historia inaanza akiwa nyumbani kwao na babu yake pale bagamoyo, ambapo alishiriki katika shughuli za kucheza gwaride kama chipukizi wa chama na hata alipokwenda huko NCHINGWEA NA MASASI aliendelea na shughuli za kucheza gwaride la chipukizi wa chama cha mapinduzi.

mwaka 1992, alikuwa ni mmoja kati ya vijana walioshiriki kama wajumbe kwenye mkutano mkuu wa chipukizi wa ccm taifa uliofanyika mbeya ambao ulimchagua bwana RAYMOND MANGWALE kuwa mwenyekiti wa jumuiya hiyo taifa. ( ikumbukwe bwana RAYMOND ni katibu wa UV-CCM, mkoa wa DODOMA ,kwa sasa). hata hivyo pia, wakati wa enzi hizo za masomo ya shule ya msingi, ridhiwani atakumbukwa kama kijana aliyechangia hela nyingi kwenye mradi wa mabasi ya UV-CCM na hata kupeWa nishani na RAISI mstaafu wa AWAMU YA PILI, ALHAJI ALLY HASSAN MWINYI katika viwanja vya KARIMJEE sherehe ambazo zilihudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo mabalozi wa nchi mbalimbali na viopngozi wa serikali.

wakati yupo sekondari aliendelea kuwa mwana harakati wa kawaida pale shuleni DAR ES SALAAM na hata baadae IRINGA.Waliosoma naye iringa wanakumbuka pilika zake na wenzake katika siasa za wanafunzi ,na michezoni.alikuwa mcheza mpira mzur sana enzi hizo.sijui siku hizi kama anacheza au bado.kumbukumbu zinaonyesha ushiriki wake katika kampeni za kufanikisha wenzake kupata nafasi za uongozi.

wakati akiwa chuoni, alikuwa mstari wa mbele katika siasa za DARUSO. RIDHIWANI amewahi kuwa katibu wa serikali ya wanafunzi, WIZARA YA MAMBO YA NJE NA WANAFUNZI WANAOTOKA NCHI ZA NJE, na baadae alikuwa MBUNGE MWAKILISHI TOKA KITIVO CHA WANAFUNZI WA SHERIA, kabla hajawa MWENYEKITI WA DARUSO-KITIVO CHA SHERIA.

katika kipindi hiki tumeona alivyokuwa akishiriki katia siasa za wanafunzi na hata kushirikiana na wenzake kuhakikisha kuwa yale mambo wanayoyataka katika mazingira ya chuoni hapo yanakuwa vizuri.

Wakati yupo chuoni, akiwa mwaka wa tatu, 2002 aliteuliwa kuwa MUHAMASISHAJI WA UVCCM-wilaya ya BAGAMOYO.ikumbukwe kipindi hiki ni kipindi bwana SAIDI MTANDA ambaye kwa sasa ni MBUNGE WA JIMBO LA MCHINGA,LINDI alikuwa ndiyo MWENYEKITI WA UVCCM wilaya ya bagamoyo.ufanisi wa bwana RIDHIWANI katika mambo ya shughuli za vijana ikiwemo kushirikiana na wenzake kufanya makambi ya kuwaandaa vijana kwa shughuli za jumuiya na mchango wake ulimpelekea kuchaguliwa 2004 kuwa MJUMBE WA BARAZA LA UVCCM-PWANI.ikumbukwe kuwa kipindi hiki mwenyekiti wa vijana mki=oa wa pwani alikuwa BW.KULWA SAID.

katika uchaguzi wa ndani wa CCM , mwaka 2007 bwana RIDHIWANI lichaguliwa kwa kura nyingi , tena kwa kuongoza kwa wingi wa kura kuwa MJUMBE WA MKUTANO MKUU WA CCM TAIFA (nafasi abayo anayo hadi sasa).Pamoja na hillo pia RIDHIWANI katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2008 lichaguliwa na vijana wenzake wa wilaya ya BAGAMOYO kuwa MJUMBE WA MKUTANO MKUU WA UVCCM-TAIFA na pia MJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA CCM YA WILAYA -BAGAMOYO.

nafasi ya ujumbe wa halmashauri ya ccm ya wilaya , inampa nafasi ya kuwawakilisha vijana wenzake ndani ya vijao vya chama ngaz ya wilaya. mwaka 2008 alichaguliwa kuwa MJUMBE WA BARAZA KUU LA VIJANA TAIFA kuwakilisha UVCCM-PWANI na kabla kikao cha baraza kuu akijamchagua yeye kuwa MJUMBE WA KAMATI YA UTEKELEZAJI YA UVCCM-TAIFA.

RIDHIWANI amekuwa akishiriki katika shughuli za vijana kila siku. kama walivyovijana wengine amekuwa mstari wa mbele kukitetea chama chake cha CCM na pia sera zake. ameshiriki katika mambo yanayohusu vijana wenzake katika makundi mbalimbali hasa yale ya wanafunzi,wanamuziki,wanamitindo,walemavu na mengoineyo mengi.

Kichama ameshiriki kwenye mambo mengi hasa ili la kampeni za chama safari hii. yeye na wenzake akiwemo MAKAMU MWENYEKITI, KATIBU MKUU,NAIBU KATIBU MKUU na wengineo ambao waligawanyika katika makundi mbalimbali wakikinadi chama chao.kubwa zaidi ni jinsi walivyojipanga vijana hasa kukisaidia chama chao kirudi lakini Ukiacha yote ni jinsi kijana alivyokuwa mstari wa mbele kuhahakikisha mambo yanakuwa mazuri.

RIDHIWANI amewahi wakilisha nchi yetu katika mikutano mbalimbali toka akiwa mtoto. mtakumbuka mkutano wa watoto ,ROME 1992, YES-SUMMIT MEXICO 2001,PANEL ON ENVIRONMENTAL SINGAPORE 2005,COMMONWEALTH YOUTH ORGANISATION MALTA 2007- YES-AFRICAN CAUCAS LESOTHO 2006, DEVELOPMENT AND CHALLENGE FACING RULLING PARTIES-SOUTH AFRICA 2008 na mengineyo mengi

RIDHIWANI ameoa na mungu amemjalia mtoto mmoja wa kike anaitwa AZIZA.

ni imani wajukuu zangu sasa mnamuelewa kidogo RIDHIWANI.tunapojadili ndani ya kitivo hiki cha waelewa nafikiri ni vyema tukaanzia hapa.kwamba ridhiwani tunayemjua anafanana hivi. na ni imani yangu kuwa kidogo kama sio kwa msaada swali '' HUYU RIDHIWANI NI NANI, ANAZUNGUMZA KAMA NANI NA ANAFANYA HIVI KAMA NANI LINAWEZA KUWA LIMEPATIWA JIBU''

MNYONGE MNYONGENI, LAKINI HAKI YAKE..................................

babu unazeeka vibaya.

so unataka nini baada ya kuandika izi crap?
 
Wewe MTAWALA mbona unamkosea heshima huyo R na hao wenzake uliowataja? Mke wake amekukosea nini hata ukamtusi hivyo?

Ungehoji hayo maandishi yake tu lakini hayo matusi mengine hayana manufaa kwetu sisi.
 
Back
Top Bottom