Elections 2015 Nani hatari zaidi kati ya malaika aliyegeuka shetani, Au shetani aliyegeuka malaika?!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,442
113,451
Wanabodi,

Leo tena naendelea na zile makala zangu za malaika na shetani.

Kwa wasomaji wapya katika kukumbushana tuu, hapo hapo mwanzo, shetani alikuwa malaika kabla hajawa shetani, tena ndio alikuwa malaika Mkuu! .

Kwenye himaya ya mashetani shetani hayuko peke yake, yuko na wale malaika wengine waliojiunga nae ambao sasa wote ni mashetani wengine walioamua kujiunga nae!.

Katika la jeshi la malaika wa mbinguni from time to kuna baadhi ya malaika huwa wana defect na kumfuata shetani na hivyo hugeuka mashetani.

Vivyo hivyo kwenye jeshi la shetani kuna mashetani huwa wanatubu na kumrudia Mungu hivyo hurejea na kuwa malaika. Hawa sasa ni harmless kwa sababu ushetani wao wote wanakuwa wameuacha kule ushetanini!.

Lakini inapotokea malaika akaamua kufanya kazi ya shetani huku amepose kama malaika!, huyu ni hatari kuliko hata shetani mwenyewe!, maana you can't tell!. Watu wa Mungu watamsikiliza wakidhani ni malaika kumbe nje na ngozi tuu ndio ya malaika lakini ndani ni ibilisi mwovu shetani wahedi! .

Swali ni jee?, nani ni hatari zaidi kati ya shetani aliyetubu na kugeuka malaika au malaika aliyegeuka shetani kwa kufanya kazi ya shetani huku akiendelea kupose as malaika?!.

Tafakari na chukua hatua.

Nawatakia Jumatano njema.

Pascal

 
Mkuu Pasco tumeshakusoma. Hii inaweza kuswamwa sambamba na andiko linalokataza kuwa vuguvugu. Ya kwamba wana adhabu kali sana vuguvugu!! Kwangu miminaona shitwani aliye tubu anaweza kuwa muungwana kuliko shetani anayepoz kama malaika.

Uzuri mimi si mmoja wa undecided voters! Nimewkisha fanya maamuzi, na aenende kwa amani.

Mkuu najua umeshanielewa...
 
Last edited by a moderator:
Mkuu hii mada yako inachanganya. Malaika kugeuka Shetani ni hatari kwani hakuna asiyejua habari za Shetani na mambo yake. Tatizo ni hilo la pili la Shetani kugeuka Malaika; hili ni gumu kulijadili kwa sababu hatuna japo mfano mmoja. Malaika alishawahi kugeuka Shetani ndio maana leo tunazungumzia habari za Lusifa na mashetani wenzake.

Kwa upande mwingine, haijawahi kusikika au kuandikwa popote Shetani kugeuka Malaika - haipo. Hivyo, sina budi kusema kwamba mfono wako ni irrelevant na Shetani ataendelea kubaki Shetani milele yote.
 
Mtatupa tupa sana miguu na kubana, lakini mwishowe DAWA ITAINGIA TU

Ni bora mtulie ili sindano isikatikie ndani mambo yakawa magumu zaidi
 
Hii hadithi tu....Shetani na Malaika zake walishahukumiwa na hawana nafasi tena ya kutubu.....tafuta mfano unaokwenda na ukweli ....

ya mungu yahache uyawezi kwani mungu si ni mwingi wa rehema kwani mungu akiamua kumsamehe shetani si anaweza mbona uwa wanawasiliana na kujivunia watu wao wanaomwabudu, mbona alimbadilisha poul na kumtumia kwa viwango vya juu hivyo ata akihamua kumsamehe shetani imawezekana maana kwa mungu akuna kisicho wezekana,
mkuu shetani aliyetubu ni bora kuliko malaika aliyegeuka shetani
nimekupata mno
 
Pasco,hata Mtakatifu Paulo alikuwa muuaji wa wakristu akiitwa SAULI,hivyo vyote vya wezekana kwa Mungu.Ila badala ya hii ya Shetani na Malaika.bora ungeiweka hii ya SAULI kuwa PAULI.

Pole Mungu ndiye ahukumuye kwa HAKI.

Kwa sasa nikipiga akili MASWALI ni mengi kuliko majibu.
 
Wanabodi,
leo tena naendelea na zile nakaa zang za malaika na shetani.

Kwa wasomaji wapya katika kukumbushaba tuu, hapo hapo mwanzo, shetani alikuwa malaika kabla hajawa shetani, tena ndio alijua malaika Mkuu! .

Kwenye himaya ya mashetani shetani hayuko peke yake, yuko na wale malaika wengine waliojiunga nae ambao sasa wote ni mashetani wengine walioamua kujiunga nae.

Katika la jeshi la malaika wa mbinguni from time to kuna baadhi ya malaika huwa wana defect na kumfuata shetani na huo hugeuka mashetani.

Vivyo hivyo kwenye jeshi la shetani kuna mashetani huwa wanatubu na kumrudia Mungu hivyo hurejea na kuwa malaika. Hawa sasa ni harmless kwa sababu ushetani wao wote wana kuwa wameuacha kyle ushetanini!.

Lakini inapotokea malaika akaamua kufanya kazi ya shetani huku amepose kama malaika!, huyu ni Hatari kuliko hata shetani mwenyewe maana you can't tell!. Watu wa Mungu watamsikiliza wakidhani ni malaika kumbe nje na ngozi tuu ndio ya malaika lakini ndani ni ibilisi mwovu shetani waged! .

Swali ni je ni nani ni Hatari zaidi Kati ya shetani aliyetubu na kugeuka malaika na malaika Aliyegeuka shetani kwa kufanya kazi ya shetani huku akiendelea kupose as malaika?!.

Tafakari na chukua hatua.

Nawatakia Jumatano njema.

Pasco[/shetanilTatizo mashetani yenu hayajitambulishi kama mashetani mengine ni maaskofu, mapadre, masheikh. Sasa kutubu hakuko hivi yakubali kwanza yenyewe ni mashetani. Gwajima ni malaika au shetani? Sumaye ni malaika au shetani.
 
Umewahi kusikia wapi hiyo? Shetani kutubu? Shetani ni Shetani milele yote wala msamaha kwake haupo. Mfano uliotolewa ni wa kijinga na irrelevant.

Mkuu
Hivi Shetani na Mungu huwaga wanapiga Story ki rafiki kabisa ?
Kwenye habari ya Ayubu tunaona Mungu na Shetani ni kama walikuwa wana bet vile..?!?!?!
 
Mkuu
Hivi Shetani na Mungu huwaga wanapiga Story ki rafiki kabisa ?
Kwenye habari ya Ayubu tunaona Mungu na Shetani ni kama walikuwa wana bet vile..?!?!?!

Mkuu hoja hapa ni Shetani kutubu, kugeuka kuwa Malaika. Kwenye habari ya Ayubu hata kama Shetani ali-bet na Mungu lakini mwisho wa siku aliendelea kuwa Shetani; hakusamehewa. Sijui kama nimeeleweka.
 
Pasco,hata Mtakatifu Paulo alikuwa muuaji wa wakristu akiitwa SAULI,hivyo vyote vya wezekana kwa Mungu.Ila badala ya hii ya Shetani na Malaika.bora ungeiweka hii ya SAULI kuwa PAULI.

Pole Mungu ndiye ahukumuye kwa HAKI.

Kwa sasa nikipiga akili MASWALI ni mengi kuliko majibu.

Absolutely! This is relevant example. Binadamu hutubu na kugeuka sio Shetani. By the way, sijui kwa mfano wa Pasco Shetani ni nani na Malaika ni nani? Binadamu ni binadamu sio Shetani wala Malaika. Upotoshaji wowote ni lazima ukemewe kwa nguvu zote na kwa wakati.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu hoja hapa ni Shetani kutubu, kugeuka kuwa Malaika. Kwenye habari ya Ayubu hata kama Shetani ali-bet na Mungu lakini mwisho wa siku aliendelea kuwa Shetani; hakusamehewa. Sijui kama nimeeleweka.

Nimekusoma Mkuu vyema kabisa.
Hoja yangu ilikuwa ni different topic kabisa.
 
Absolutely! This is relevant example. Binadamu hutubu na kugeuka sio Shetani. By the way, sijui kwa mfano wa Pasco Shetani ni nani na Malaika ni nani? Binadamu ni binadamu sio Shetani wala Malaika. Upotoshaji wowote ni lazima ukemewe kwa nguvu zote na kwa wakati.

Naona akirudi atajirekebisha.
 
Back
Top Bottom