Tukipata namna nzuri ya kuhifadhi, kulinda na kutumia vizuri mali ya UMMA hatuhitaji UBEPARI wala UJAMAA. Wachina, WaVietnam na hata WaCuba ni wakali mno kwa wabadhirifu wa mali za UMMA. Wanazo sheria na maadili makali na wanayasimamia kwa nguvu zote bila kujali dunia nyingine ya wanaojiita wanaharakati wa haki za binadamu watasema nini.
Nchi za Scandinavia nazo wanasimamia sana maadili na uwazi katika kazi zao. Wana viwango vidogo mno vya rushwa au haipo kabisa. Kwao kama ilivyo Japan UONGOZI ni dhamana tu. Ukishindwa unaondoka haraka tena kwa heshima zote. Japan kwa miaka hii mitano wana Mawaziri Wakuu wastaafu zaidi ya wanne. Walichokifanya Japan ni kujenga taasisi zenye nguvu.
Zisizo na uhusiano wa mojakwamoja na vyeo na nafasi za kisiasa. Hapa kwetu ni mpaka pale Waziri Mkuu anapolalamika kuwa polisi wanasindikiza sukari kwenda Kenya ndipo hatua za muda tu zinachukuliwa. OCD, RPC, DCI na IGP wanaendelea na vyeo na nyadhifa zao kama kawaida!
Nchi kufanikiwa kuendelea na kuwaendeleza watu wake ni zaidi ya mifumo hii ya UJAMAA na UBEPARI.