Nani anatudharau sana waafrica kati ya hawa 3?

mshikachuma

JF-Expert Member
Dec 2, 2010
2,853
626
Tuache unafiki na ubishi wa kujifurahisha nafsi wa funika kombe mwanaharamu
apite. Ukweli ni kwamba bara la Africa limevamiwa na wageni wengi kutoka nje.
wengi wa wageni hao ni Wazungu,wahindi na waarabu. Kwa hapa Tanzania ime
fikia wengine kupata uraia bubu ilimradi mambo yao yaende,na wengine wamepata
uraia kwa kuzaliwa hapahapa. Lakini kiukweli ukiwachunguza kwa makini hawa watu
utagundua kuwa wengi wao kama si wote wanawazarau watanzania usipime!
Yaani kwao mtu mweusi (mwafrica) si chochote si lolote.
Ndiyo maana nauliza kati ya Mzungu,muhindi,na mwarabu ni nani anazarau sana
waafrica? - Nakaribisha mgongano wa kimawazo na kimtazamo. Ahsanteni.
 
Mimi naishi hapa Marekani na nitakwambia hii inatokana na mtu. Kitu kimoja cha muhimu ni kwamba unatakiwa utharau watu wanaokubagua kwasababu si tatizo lako bali ni lao na ukianza kifiria nani ananibagua zaidi ndiyo mwanzo wa wewe pia kuwa na matatizo. Wewe kama kuna mtu anakutharau fanya kazi yako au biashara yako vizuri na baadaye atagundua kuwa yeye ndiye mwenye matatizo ya kuelewa binadamu na si wewe. Dawa ya ubaguzi ni kuitharau na si kuipa topics kama hizi, na usilaumu hawa watu kwasababu vyombo vingi vya habari hasa huko kwao vinatuongea Waafrica vibaya sana na wanakuwa watuwazima na ile picha kichwani hivyo ni tatizo lao si lako!
 
Tunadharaulina, dharau ipo sio kwa wageni tu bali hata sisi kwa sisi, yaani mbongo na mbongo.

Sasa hivi tanzania kuna social classes kama ulikuwa hujui ndugu yangu,

Kati ya tajiri na fukara hapa kuna dharau ya hali ya juu though wote tu watanzania.Bado hujaja kwenye ukabila na udini.

Sorry mie niko neutral kwenye mada yako nikimaanisha kuwa dharau iko kote kote bila kuangalia race, religion au social class.
 
Mkuu nimekusoma vizuri sana! Lakini tuache zarau za wabongo kwa wabongo kwani zinakuwa kwa mda tu'tena penye mgongano
wa kimaslahi au bifu fulani la kiaina. na akitokea mtu au watu kupatanisha basi bifu na zarau zinaisha na heshima,urafiki urejea tena.
Lakini kwa hao watu niliyowataja hawana hivyo vitu,bali kwenye akili zao wamejaa zarau na husuda kwa waafrica kila siku
 
Mimi naishi hapa Marekani na nitakwambia hii inatokana na mtu. Kitu kimoja cha muhimu ni kwamba unatakiwa utharau watu wanaokubagua kwasababu si tatizo lako bali ni lao na ukianza kifiria nani ananibagua zaidi ndiyo mwanzo wa wewe pia kuwa na matatizo. Wewe kama kuna mtu anakutharau fanya kazi yako au biashara yako vizuri na baadaye atagundua kuwa yeye ndiye mwenye matatizo ya kuelewa binadamu na si wewe. Dawa ya ubaguzi ni kuitharau na si kuipa topics kama hizi, na usilaumu hawa watu kwasababu vyombo vingi vya habari hasa huko kwao vinatuongea Waafrica vibaya sana na wanakuwa watuwazima na ile picha kichwani hivyo ni tatizo lao si lako!
Na akitokea umependana na binti wa kihindi au kiarabu na kufikia mnataka kufunga ndoa, kisha wazazi wa huyo binti wanapiga pin kwa kukataa kukupa
mtoto wao na huku mnapendana! je utafanya nini?
 
Mimi naishi hapa Marekani na nitakwambia hii inatokana na mtu. Kitu kimoja cha muhimu ni kwamba unatakiwa utharau watu wanaokubagua kwasababu si tatizo lako bali ni lao na ukianza kifiria nani ananibagua zaidi ndiyo mwanzo wa wewe pia kuwa na matatizo. Wewe kama kuna mtu anakutharau fanya kazi yako au biashara yako vizuri na baadaye atagundua kuwa yeye ndiye mwenye matatizo ya kuelewa binadamu na si wewe. Dawa ya ubaguzi ni kuitharau na si kuipa topics kama hizi, na usilaumu hawa watu kwasababu vyombo vingi vya habari hasa huko kwao vinatuongea Waafrica vibaya sana na wanakuwa watuwazima na ile picha kichwani hivyo ni tatizo lao si lako!

Beautiful....!

Very well said indeed.
 
Pia nashukuru kwa kukubari kuwa hizo zarau wanazo. So jaribu kujibu topic yangu - kati ya hao 3 nani anazarau sana mwafrica?
 
Hakuna mwenye nafuu kati ya hao watatu kwani ubaguzi ni ubaguzi tu; dharau ni dharau tu bila kujali nani kaonesha. Hakuna cha nafuu!
 
Beautiful....!

Very well said indeed.
Mkuu huyo unaemsifia Beautiful very well said indeed amekubari kuwa zarau za ki
ubaguzi zipo ila ajajibu swali langu la kati ya hao 3 ni nani anazarau sana waafrica?
Nitashukuru iwapo na wewe utajibu ni nani kati ya hao 3
 
Pia nashukuru kwa kukubari kuwa hizo zarau wanazo. So jaribu kujibu topic yangu - kati ya hao 3 nani anazarau sana mwafrica?

Fikisha fikra kwa upana, "dharau" una nia tulitumie au unaangalia linapotumika sisi waafrika tunaathika vipi na utekelezwaji wa dharau, sisi waafrika tunajidharau, tunajidharaulisha, ndiyo maana tunadharauliwa, ukijua kuwadharau wasiofanana nawe, utawapelekea somo kujifunza kukuheshimu, pia zingatia aliyosema aliyejitambulisha kuishi marekani.
 
nakubaliana nawe kwa upande mmoja ila Mshikachuma kwa upande mwingine kuna waafrika ambao wanadharau waafrika wenzao kuliko hata unavyofikiria ndugu yangu. nalo hilo tusemeje?
 
Kwahii topic yangu nimefikisha fikra ki upana, ndiyomaana hata wewe na uyo aishie marekani mkaisoma na mkaamua kucoment.
Hata kama waafrica tunadharauliana lakini si kihivyo mkuu! hawa jamaa wamezidi!. Je ulipata kusoma au kusikia kisa cha Adelina
kuvuliwa chupi na mzungu kule mgodini Geita? Na je unawajuwa wahindi na waarabu wanavyotunyanyasa kiaina ndani ya nchi yetu?
 
nakubaliana nawe kwa upande mmoja ila Mshikachuma kwa upande mwingine kuna waafrika ambao wanadharau waafrika wenzao kuliko hata unavyofikiria ndugu yangu. nalo hilo tusemeje?
Mkuu kwanza hongera kwa kujiunga na JF leo na karibu sana jamvini!. Ni hivi nakubariana ni kweli kuna waafrica wanawadharau
waafrica wenzao kinamna fulani. Lakini amini penye waafrica 10 utakuta ni mwafrica 1 au 2 ndiye mwenyedharau hizo tena anafanya
hivyo kwa kujiangalia kuwa yeye anakipato fulani au anacheo fulani kweye jamii. Au niseme waafrica hasa watanzania hawana dharau
ila wanaulimbukeni tu. Lakini kwa hao niliyokutajia ukikuta wapo kundi la watu 10 basi ujue 9 wote wanatudharau na kutubagua kiaina flani
 
kimsingi mimi nimeishi na makundi yote matatu uliyoyataja na pia kundi la nne unaloliona la wadharauriwa (waafrika) dharau ya ubaguzi ni dharau iwe kubwa au ndogo yote ni dharau na inaumiza, cha msingi kuto kuangalia nani anakudharau/kubagua kuliko nani maana utajijengea hasira na kuanza kumbagua pia.

Nikijibu HOJA yako wote hao watatu ni wabaguzi lakini WAHINDI ni babu kubwa(kumbuka kuna wahindi waislam,singasinga, wakristo na wahindu) Wahindi wa dini ya hindu ni noma tena wengi wao watokao ktk jimbo la GUJARAT HAO NI SOO na hiyo inatokana na DINI yao ya HINDUISM ambayo inabainisha kuwa duniani binadamu tupo katika matabaka na kunatabaka la untouchable ktk tabaka hilo waafrika tumo kama ilivyo kwa jamii ya wahindi wenzao, wahindi weusi (GOA)

Hila kumbuka viongozi wetu wa Tanzania na Afrika ni watu wa kujipendekeza na kuthamini wenye nacho tabia hiyo imepelekea kujipendekeza kwa jamii ya WAHINDI ambao wanawatumia viongozi wetu kama condom siku wakipoteza madaraka wanawabagua kama waafrika wengine, tabia ya viongozi wetu ndio imeongeza hali ya waafrika weusi kubaguliwa hata katika nchi zetu wenyewe na viongozi wetu wakishiriki kufanikisha hali hiyo.

Cha msingi ukichukia kubaguliwa kwa rangi au ufukara wako nawe usibague wengine au wanaokubagua maana kama nawe unabagua hautokuwa na tofauti na hao wabaguzi wenzako
 
Mimi ni Mtanzania naishi china kwasasa, wachina nao niwabaguzi wa rangi sana hasa ukiwa mweusi alafu unatokea africa ndio kabisa, tena ukiwa mweusi saaana sana kama wenzetu wasudan unaweza ukaingia sehemu wachina wakakimbia wote au kama ni watoto wakaanza kulia kama kwamba wamevamiwa na mtu anaye tisha.Hii ni kwasababu ya picha mbaya ambayo wanayo kuhusu mwafrica au mtu mweusi kutokana na mambo ya utumwa,pia wafundishwa mashuleni mambo mabya sana kuhusu africa kwamba kumejaa magonjwa ,umaskini n.k.Yani wanavyo mconsider mtu mweusi alivyo kwa kweli wana pitiliza.

Kwahiyo mimi navyo ona mtu mweusi kokote pale anapokwenda anabaguliwa sana,kutokana na stereotype ambazo watu wanazo kuhusu mtu mweusi.

Wazungu hasa wanao tokea america ( USA na Canada) wanadharau sana, tena wengine uku china wana dundwa maana wanajiona yani kama wenyewe pekeyao ndio wako juu ya dunia wengine tuko chini.Waarabu sio kwa sana jamani....mizingu ndio imezidi yani.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom