Nani anatakiwa abadilike mimi au mke wangu?

Aaa wapi, unatuchezea akili weye. Hiyo si ndio post ya kwanza ya IP? Hahahaha1 Timekustukia.
Sasa Mkuu chrispin umemstukia nani huyo IP au nani? Si umeona hapo post yake ndo ya kwanza baada ya kuambiwa na mumewe asome maoni ya wadau ndo akamua kujiunga atoe na yeye upande wa shilingi? au hujamuelewa?
 
Hapo wa kubadilika ni mama. Lazima aende na wakati bana. Kama hawezi swahiba tafuta anayeendana na hali halisi ujivinjari naye. Asikuletee za kuleta.
Binamu kwa shortcuts sikuwezi!

Kabla ya kumshauri mleta hoja pls hebu niambie ilikuwaje miaka yote wakati mnakatiza makontinents na kupanda ngazi moja hadi nyingine..ina maana mlikuwa hampo wote hadi ukamwacha kiasi hicho? Ninasema hivi kutokana na uzoefu katika mambo haya.Watu wengi huanza from humble begginings wakiebadilika kuanzia umri hadi status... na katika mchakato huo wa mabadiliko wote wawili mnapitia transformation - kuanzia kujifunza lugha mpya, kujifunza ettiquete na ustaarabu wa sehemu mbalimbali, kuanzia uvaaji, makulaji, mikao, mapose n.k. Ina maana wewe ulibadilika ghafla bin vuuu yeye akiwa wapi mpaka sasa unashtuka kuwa anahitaji kubadilika?
 
Mhh Nyamayao! Hapa umeniangusha, nini hujaelewa. Mimi nakukubali sana kwenye hizi mada. Mkuu hapa yuko wazi kabisa kwamba Mamsapu wake hataki mambo ya kisasa yaani mabadiliko. Na yeye yuko kwenye next level. So anachouliza ni kwamba yeye abadilike aendane na Mamsapu au ni Mamsapu abadilike awe wa kisasa. Nadhani hiyo ndo dhana kuu.

icon10.gif
icon10.gif
icon10.gif
icon10.gif
 
Sasa Mkuu chrispin umemstukia nani huyo IP au nani? Si umeona hapo post yake ndo ya kwanza baada ya kuambiwa na mumewe asome maoni ya wadau ndo akamua kujiunga atoe na yeye upande wa shilingi? au hujamuelewa?

Ukweli ni kwamba, hamna cha mke aliyeandika hapa. Aliyeandika hii ni huyohuyo aliyeandika ile, anataka kutupima akili zetu. Stuka kimey.
 
Wadau,
Hili ni tatizo lililopo kweli lakini si kama tunapigana. Nimeona nimwambie mke wangu aweze kusoma maoni ya wengine pia. hata registration hakuwa anaweza nimemsaidia. Bado naomba ushauri maana tunaongelea hali halisi na wala hakuna chochote cha kutunga wala mchezo. Hakuna sababu ya mchezo maana hakuna faida kwa hilo. Zaidi ingetupotezea wakati sisi kwa kuandika mambo yote haya.
Ukweli kwa kujibu hoja ya MAMSAP naomba arejee ukweli kwamba ni siku 4 kwa sababu leo ni JUMATANO na tuliongea JUMAPILI , therefore we have J2, J3, J4, na J5 .
Hoja ya kuwa pamoja ni kweli wakati nasoma M Sc. yeye alikuwa TZ. Na baada ya hapo tumekuwa wote tu na nimejaribu kuelimisha mengi ambayo alishindwa nilitupilia mbali.
1) Kuhusu kutembea: kuna ubaya gani kusema mwanamke fulani anatembea kwa kujiamini? hili wajamani kwa mamsap ni kosa la jinai. haya niliacha.
2) TV show, ukweli sijasema mtu apende show fulani. lakini, nilikuwa nina watch shows ninazopenda na kuzitetea jinsi zinavyo pendeza hilo kosa! Ikabidi niwe na TV bed room. Wakati nataka ku_watch Trumph the celebrity, yeye angalie anachopenda. Nilikubali.
3) Kunenepa: unene una madhara yake wengi wanajua. Sasa kosa langu ni nini?
Tukumbuke kuwa elimu ya ndoa haifundishwi shule wala kusoma si lazima kuwa na elimu ya uhusiano wa ndoa.
Mwisho naomba kwa vile amesema yake na mimi nimesema, tuwaachie wadau wachangie ili haki itendeke.
 
Kuna ukweli katika hilo dada!!

Wangu alikosa kitchen party,na tuko miaka mitatu ya ndoa,naona kuna mambo hataki kubadilika na namuacha nyuma kidogo....

Mfano...tunachangia harusi,tunapewa kadi,siku ya kwenda anatia mgomo....inabidi niende mwenyewe....hapo???

Na vya kwenda kupata ka-tusker pale grocery ya karibu hiyo company ndo hawezi kunipa kabisa....

Swala la mawazi,nalo nina shaka,maana kuna mavazi ya kisasa namnunulia tena kwa bei ghali,lakini anayatosa kiaina

Bado naendelea kumbadilisha laikini.....nahisi tunakoelekea sio kuzuri sana..

Natamani apate kitchen party hata za watu wengine tuu..


eeeeh pole sana ndugu yangu mie nashindwa kuelewa kwa nini akina mama tunakuwa hivi jamani ...? nashindwa nitoe ushauri gani hapa
 
Mbona katika thread sijaona jamaa akisema mke wake anajihusisha na magroup ya umbea? au hizi pre judgement zako unaziweka vp? Mbona nyie mnao jiita classic ndo mnaongea sana umbea huko kwenye masalooni yenu ya classic? au umbea wenu tofauti?
hahhahahahhahahaaaaaa tena hujawahi ona , labda tofauti yao ni kwamba wambea wa classic saloon wanapiga umbea wa 'Bossip' but celebrities wa kibongo, miss nani kafanya nini, marketing manager wa kampuni flani anatoka na demu flani, beyonce inasemekana anamcheat 'camel' na jamaa gani.
lakini all in all wote wambea.
ila la muhimu ni kwamba huyo kaka hajasema kama mkewe ana magroup ya umbeya .
 
Kwani umeshindwa hata kutafuta spare tyre mkuu mbona shazi sana.
 
Hahahaha Tukuyu nilisha chapa mwendo mbona muda naonja radha tofauti tofauti nitakuja na majumuisho mkuu then nahamia kanda ya ziwa nako.

Lol! Mkuu utapata ladha za pande zote. Ulinibania, hukunipa contacts za looser flani.
 
Mbadilishe kimya kimya, mara leo umemnunulia kimini,kesho kitop, keshokutwa suruali mara kikaptula huku ile mikanga unaificha au siyo mukubwa......
 
Nimepitia maisha ya aina mbalimbali nchi mbalimbali magharibi na mashariki. Mwisho nimefika mahali ambapo ninaheshimika. Nimejaribu pia mke wangu abadili mtazamo wake kwa maisha ya leo. Bahati mbaya hataki kubadili mtazamo wako.

Hapo kwenye nchi mbali mbali ulikuwa naye huko???

Jibu:
tatizo, alipoondoka kwenda US alikaa huko miaka 3 aliporudi ndo akaanza 1) mimi mnene nipungue 2) Nitembee kama so and so. 3) Nipende show fulani fulani TV, zote


Leo ninapenda mke wangu awe classic kama akina Michelle. Natamani awe na confidence katika kila anachokifanya. Akitembea asijihisi na kutembea kama mama wa kijijini! Akiongea asiwe anajishuku shuku. Akiwa na rafiki zetu asiwe na mkao wa mwambao! mnanielewa.

Na hapo juu man mmh kweli JF kiboko. Yaani wewe kwenda US kimasomo unarudi after 3yrs unaanza kumkandia mamsapu eti abadilike kwa kuwa umekuja na u know u knows zako. Afadhali huyu IP amejitokeza kwani wewe huku-display all material facts kama hii kuwa ulikuwa US for 3 yrs na ukawa umemwacha huku and then unakuja simply wewe umeona akina XXL, XL etc huko US nawe unataka wife achange.

Mimi ndimi mke anayelalamikiwa,
Nimelazimika kutoa maoni yangu kwa PI, baada ya kuniambia kusoma comments za watu kuhusu maisha yetu.
Kwanza kuna mengi ambayo hakusema hapa lakini ametoa kipande tu cha maongezi ya juzi siku mbili na si tano kama anavyosema.
........ Kama swala ni la elimu. Alinioa nikiwa na elimu ya kidato cha sita kipindi kile tena PCB! Yeye alikuwa na degree moja. tatizo, alipoondoka kwenda US alikaa huko miaka 3 aliporudi ndo akaanza 1) mimi mnene nipungue 2) Nitembee kama so and so. 3) Nipende show fulani fulani TV, zote nimejaribu kwa kuendana na anayotaka lakini hayo hasemi. Tatizo ni hili la kubadili mwendo, nasema hapo no way.
Elimu nimejiendeleza nina diploma nzuri tu na kazi ninayo ya kuweza kubadili mwelekeo wowote. Lugha ipo kisawasawa anachotaka aseme ni mabadiliko gani siyo kula pweza hapa.

Yeye sasa ni mtu mzima asitake namimi niwe na PhD ndo aone nimebadilika. Yeye ni mhadhiri na PhD ni lazima kwake mie kazi yangu haiitaji PhD. Mabadiliko hayo yana malengo mengine na siyo kama anavyo sema. Yeye analazimika kuandaa publications ili kazi isimame anataka na mie niandike papers! NO WAY.

Another point ambayo namkubali huyu mamsapu.

Mume wangu nakupenda tu hivyo ulivyo. Nitakusaidia ubadilike.
Note: I was not an idler that's why I am not a begger!
IP

Very Big point though!


Kweli JF kiboko inaweza imarisha NDOA za watu!!
 
eeeeh pole sana ndugu yangu mie nashindwa kuelewa kwa nini akina mama tunakuwa hivi jamani ...? nashindwa nitoe ushauri gani hapa

asante dada...
natamani na mimi nimweke hapaJF apate shule kidogo...
na nitafanya hivyo...
Thanks
 
Wote mnatakiwa kubadilika, wewe kama mwanaume unatakiwa kumpeleka mkeo akafanye shopping, mchukue mwende wote na umuonyeshe mavazi gani wewe unapendelea yeye avae. Umweleweshe kwa upendo kwamba mke wangu napenda uvae hivi uwende na wakati, kama mwanamke anayetaka ndoa yake idumu atabadilika tu.

Vile vile kwa upande wa mwanamke anaweza kabisa kubadilika, hata kama ana miaka 50, mie nimeona wamama wana miaka zaidi ya 50 na wanachange kabisa, wanaenda kutokana na wakati ili kulinda ndoa zao. Wapo wanawake wanafanya hadi style za kisasa kwa wanaume zao ili kulinda ndoa zao. Wewe mama IP kuwa makini na mumeo, ukifanya mchezo mumeo atachukuliwa na wadada wanaoenda na wakati.
Tena shukuru mumeo anakwambia mapungufu yako, wapi ubadilike. kuna baadhi ya wanaume hata hawasemi kwamba ubadilike, hao wanatoka kimya kimya tu nje.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom