Nani anastahili kukuita Mpenzi, darling, sweetheart

Kwenye jamii zetu za kibantu, NI MARUFUKU! ...binafsi sithubutu kumwita mw'mke kwa majina hayo mbele ya 'mywife' wangu, na wala yeye hathubutu kutamka hayo kwa mw'ume mwingine nikayasikia, kwani inaleta tafsiri tofauti :)

Thubuutuuu...achana na hayo maneno matamu matamu, ukitaka kupata joto la jiwe thubutu kumwambia mw'mke mwingine "sweet dreams." Yaani hiyo kasheshe yake.... Hawa maiwaifu wetu bana....
 
Mi naamini anayestahili kuitwa majina hayo kwa maana halisi ni mume wako/ mke wako. Kwa sababu maneno hayo yanaashiria zaidi upendo wa kindoa (coniugal love) kati ya mwanaume na mwanamke. Matumizi mengine ni kujaribu kupanua tu wigo wa maana ya maneno hayo. Ndo mana mtu anapoamua kuyatumia hapa lazima awe mwangalifu kwani anaweza kumkosea mtu (yule anayemwita) au anaweza kuwakwaza wasikilizaji.
 
Well...humu kwenye forum tupo tupo na tunaenda kichwa kichwa tu bila hata kujua. Watu wako anonymous na hujui nani ni nani. Mtu anaweza akaji position kama mwanamke huku ni mwanamme.

Sasa kumwita mtu darling, sweetheart ama dear bila kujua jinsia yake ni makosa. But then again, this only a forum where many social laws can and are broken on a day to day basis.

Hapo nadhani umenipa jibu AMBALO HATA MIMI nilikuwa nalo kichwani...
sijui wengine watasemaje ...
 
Maneno kama mpenzi, asali wa moyo, sweetheart ni maneno yatumiwapo mara kwa mara baina ya watu.Siyo ajabu hata kidogo kusikia marafiki wakiitana "mpenzi".... hasa marafiki wa kike ni kawaida sana.Wazazi nao huweza kuita watoto wao hasa wale wadogo kabisa "sweetie", "darling" n.k.na mara nyingi akina mama ndio hupenda sana kuwadekeza watoto wao wa umri wowote kwa neno lolote lenye kuashiria upendo.
Je kwenye mazingira yasiyo ya nyumbani, ni nani anapaswa kuita mwingine kwa majina hayo na jamii inatafsiri vipi?
Sema usikike ndugu yangu.

mimi ukiniita hivyo nitakuangalia mara 2, 2. kwa nini wanawake huitana hivyo?
 
Mara nyingi utawasikia waingilish wakimwita mtu yoyote yule hello love inategemea kama ni dukani au sehemu za kutowa huduma au hata barabarani kama kumetokea kitu cha kumjulisha mtu katika wakati ule, wezetu kwa kuwa ni lugha yao na sisi ni watu wakufuata mkondo huwa tunaweka tafsiri zetu kutokana na hisia zetu za maneno hayo.kuna wakati MTZ mmoja alikubaliana na mzungu kuwa wakutane kesho wakiwa katika hatua ya mwisho kusema bye bye MTZ akasema see you2morrow na yule mzungu akamjibu see you later MTz akamwambia mzungu hapa see you 2morrow ,yule mzungu alikuwa na maana kuwa watakutana kesho,nikutofahamu matumizi katika baadhi ya maneno ,sasa inapokuja matumizi ya hayo maneno love ,sweetheat,darling ni tafauti tunavyoyachukulia sisi tunaofuata mkondo.
 
Wos; it so much depends on your background;

Sometimes we call our parents by first names or even DOGO, it makes them laugh so much.

I call my Sisters and Mom all kind of names, Sweethert, Dear, Darling, Sister, Sweet etc and it makes sense to all of us.

I stay with my wife and because we are only two I call her all names, Sweety, baby, Mom, Ant, Mshikaji, Honey, Mywife etc. She calls me back similar names.

It is all depends with background, upbringing, and how confortable everyone is. . . .
 
Haya tupe Background yako Mkuu na hiyo upbringing tutajaza wenywe tukisha elewa Background yako,by the way huwa mnatumia lugha gani kuitana hayo majina Kiswahili au za kimakabila?
 
Haya tupe Background yako Mkuu na hiyo upbringing tutajaza wenywe tukisha elewa Background yako,by the way huwa mnatumia lugha gani kuitana hayo majina Kiswahili au za kimakabila?

Mkuu, tunatumia kiswahili. Background - strong family ties, jokes kwa sana kuanzia bibi hadi wajukuu, foreign exposure, others married in Diaspora now etc.
 
Thubuutuuu...achana na hayo maneno matamu matamu, ukitaka kupata joto la jiwe thubutu kumwambia mw'mke mwingine "sweet dreams." Yaani hiyo kasheshe yake.... Hawa maiwaifu wetu bana....

Na mpaka umwambie sweet dreams ukiwa na mywaifu wako unakuwa unatafuta nini ndugu? Na yeye akimwambia njemba njozi tamu utajisikiaje?
 
Asante Buswelu,
Kwanini wanaume hawaonyeshani kushibana au upendo wa moyoni?

Asante kwa mchango wako mzuri.
Unadhani kwanini haya maneno hayakuwepo kwenye kawaida yetu au huko vijijini? Ina maana waafrika/Watanzania hawana au hawataki kuonyesha hisia za upendo?
Kwanini sasa tunaiga utamaduni wa kigeni ilahali kila binadamu ana hulka ya kupenda na kupendwa - awe mtoto, mzazi, rafiki?

katika mila zetu haya maneno yanaonekana si ya kawaida au hayakuwa yanatumika hadharani kwa kuwa suala la mapenzi lilikuwa linatafsiriwa kama ni suala linaloendana na tendo la ndoa zaidi, hivyo likachukuliwa kuwa ni kitu cha siri mno, hata ikapelekea viungo vyake nayote yatokanayo na hilo kuwa siri, na suala la upendo wa aina yeyote likabaki kuwa ni kitu cha moyoni, ufupi hatukuwa na uasili ya kuexpress upendo tulionao kwa kutumia maneno,

lakini kutokana na mambo ya utandawazi watu tunaona na kujifunza mengi, na kuona matumizi ya maneno haya kuwa si kwa ajili ya mambo ya chumbani tu kumbe hata upendo wa kawaida kwa mtoto, rafiki au ndugu unaweza ukaulezea uakauonyesha,

sioni tatizo la kuiga utamaduni wa kigeni kama ni mzuri, binafsi naona raha nikuonyeshwa napendwa, nasikitika sijawahi kumsikia mzazi wangu akiniambia nakupenda hadi umri huu, lakini najisikia faraja, sweetheart wangu na watoto wakiniambia nakupenda, au wakiniita sweet, mpenzi, nk
 
WoS
Kuitana majina kama darling,sweetheart,mpenzi n.k. ni vionjo katika mapenzi kati ya watu. Japokuwa siyo lazima mwingine anaweza kutumia la'aziz na mengineyo.
Pia wengine kama wameoana wanaweza kuitana majina yao halisi au baba/mama naa..Inategemea na walivyozoea,wengine wanatumia wife/husband.
 
...it's 'Weird' pale mtu miaka nenda rudi alikuwa anakuita Darling, mkishaachana tu anakuita "lijanaume!" :D
 
WoS
Kuitana majina kama darling,sweetheart,mpenzi n.k. ni vionjo katika mapenzi kati ya watu. Japokuwa siyo lazima mwingine anaweza kutumia la'aziz na mengineyo.
Pia wengine kama wameoana wanaweza kuitana majina yao halisi au baba/mama naa..Inategemea na walivyozoea,wengine wanatumia wife/husband.

Asante BJ,
Je nje ya hapo mtu akikuita darling na wakati hamna uhusiano?
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom