Nani anastahili kukuita Mpenzi, darling, sweetheart

WomanOfSubstance

JF-Expert Member
May 30, 2008
5,457
956
Maneno kama mpenzi, asali wa moyo, sweetheart ni maneno yatumiwapo mara kwa mara baina ya watu.Siyo ajabu hata kidogo kusikia marafiki wakiitana "mpenzi".... hasa marafiki wa kike ni kawaida sana.Wazazi nao huweza kuita watoto wao hasa wale wadogo kabisa "sweetie", "darling" n.k.na mara nyingi akina mama ndio hupenda sana kuwadekeza watoto wao wa umri wowote kwa neno lolote lenye kuashiria upendo.
Je kwenye mazingira yasiyo ya nyumbani, ni nani anapaswa kuita mwingine kwa majina hayo na jamii inatafsiri vipi?
Sema usikike ndugu yangu.
 
Mtu na mke wake,Mtu na mpenzi wake....,mtu na rafiki yake hii nimesikia kwa wadada wanaitana majina hayo...kuonyesha kushibana kwa urafiki....mind you wanaume hawaitaini hivyo.
Ni njia moja ya kuonyesha upendo toka moyoni...
 
Maneno haya yanatumika sana kwa sasa, mtu na mpenziwe, marafiki au ndugu wa karibu, na watoto!

nadhani inapendeza na inajenga upendo baina yenu, kwa watoto si kuwadekeza bali ni kuwaonyesha upendo na kuwapa faraja wajihisi kuwa wanapendwa, na vilevile isiwe tabu au ajabu siku atakapotokea dhalimu wa kurubuni na kumwambia hivyo!

kwa jamii yetu haswa vizazi vilivyotangulia, na huko vijijini bado haya maneno hayajazoeleka na unaweza kuonekana wa ajabu pale utakapo muita mwenzio au mtoto mpenzi maana hii itachukuliwa kwa tafsiri nyingine, nadhani yakitumika yatazoeleka na yatakuwa ni ya kawaida tu

kwa mtizamo wangu ingawa huu ni utamaduni wa kuiga si mbaya, kwa maana unatupa hisia za upendo katika nafsi zetu pindi tutamkapo na linampa faraja anayeambiwa, na linaweza kusaidia kuondoa matumizi ya majina yetu yale mabaya yanayoweza kumdhoofisha mtu nafsi na kuhisi hakuna anayemjua, mzazi anapokasirika bada ya kutumia jina kama weee jamila njoo hapa kwanini... anaweza akatumia lugha ya upole, jamila mpenzi njoo mwanangu uniambie kwanini....

WoS, Mie naona yanatumika
Kuonyesha upendo kwa yeyote ktk familia yako mume, mtoto lakini pia kwa rafiki wa jinsia moja sawa kabisa.
Ila rafiki wa jinsia nyingine mh labda huyo ndo "Man of Substance" mtarajiwa otherwise utafanya watu washtuke, au yeye mwenyewe au mwenza wake wakuwaze nini?
 
Mtu na mke wake,Mtu na mpenzi wake....,mtu na rafiki yake hii nimesikia kwa wadada wanaitana majina hayo...kuonyesha kushibana kwa urafiki....mind you wanaume hawaitaini hivyo.
Ni njia moja ya kuonyesha upendo toka moyoni...

Asante Buswelu,
Kwanini wanaume hawaonyeshani kushibana au upendo wa moyoni?

kwa jamii yetu haswa vizazi vilivyotangulia, na huko vijijini bado haya maneno hayajazoeleka na unaweza kuonekana wa ajabu pale utakapo muita mwenzio au mtoto mpenzi maana hii itachukuliwa kwa tafsiri nyingine, nadhani yakitumika yatazoeleka na yatakuwa ni ya kawaida tu

kwa mtizamo wangu ingawa huu ni utamaduni wa kuiga si mbaya, kwa maana unatupa hisia za upendo katika nafsi zetu pindi tutamkapo na linampa faraja anayeambiwa, na linaweza kusaidia kuondoa matumizi ya majina yetu yale mabaya yanayoweza kumdhoofisha mtu nafsi na kuhisi hakuna anayemjua, mzazi anapokasirika bada ya kutumia jina kama weee jamila njoo hapa kwanini... anaweza akatumia lugha ya upole, jamila mpenzi njoo mwanangu uniambie kwanini....
Asante kwa mchango wako mzuri.
Unadhani kwanini haya maneno hayakuwepo kwenye kawaida yetu au huko vijijini? Ina maana waafrika/Watanzania hawana au hawataki kuonyesha hisia za upendo?
Kwanini sasa tunaiga utamaduni wa kigeni ilahali kila binadamu ana hulka ya kupenda na kupendwa - awe mtoto, mzazi, rafiki?
 
WoS, Mie naona yanatumika
Kuonyesha upendo kwa yeyote ktk familia yako mume, mtoto lakini pia kwa rafiki wa jinsia moja sawa kabisa.
Ila rafiki wa jinsia nyingine mh labda huyo ndo "Man of Substance" mtarajiwa otherwise utafanya watu washtuke, au yeye mwenyewe au mwenza wake wakuwaze nini?

Asante mama Joe,
na je hapa JF mtu anapomuita mwingine maneno hayo ilhali hawajuani hata jinsi/jinsia ikoje hiyo?
 
Ah inabidi umuulize vizuri maana anaweza kuwa anashindwa kukutamkia (kama hauna mtu) lakini vinginevyo ukiendelea kumwita na kumwitikia hivyo siku umekaa na hubby au wakwe yatakuwa mengine - hata kama hukuwa na nia mbaya inabidi uthibitishe wee sasa taabu yanini/
 
Unamuulizaje humu jamvini maana inaweza kuanza malumbano yatakayoyumbisha kiini cha mjadala husika na kuishia kutoa burudani isiyo na tija?
 
Asante Buswelu,
Kwanini wanaume hawaonyeshani kushibana au upendo wa moyoni?

Asante kwa mchango wako mzuri.
Unadhani kwanini haya maneno hayakuwepo kwenye kawaida yetu au huko vijijini? Ina maana waafrika/Watanzania hawana au hawataki kuonyesha hisia za upendo?
Kwanini sasa tunaiga utamaduni wa kigeni ilahali kila binadamu ana hulka ya kupenda na kupendwa - awe mtoto, mzazi, rafiki?

Upendo umegawanyika katika makundi kama makuu matatu.
1. Upendo kwa Mungu( mpende MUNGU wako kwa moyo wako wote, akili yako yote na kwa nguvu zako zote).
2.Upendo kwa Wazazi.( Hapa inasisitizwa kuwapenda kwa akili na nguvu zote)
3.Upendo kwa wenzetu( Jirani, wake/waume zetu, watoto, majirani, nk) Kwenye kundi hili la tatu, ndiko maneno kama mpenzi, sweat, La azizi, mwandani, na mengine kama hayo huangukia. Lakini kwa wanaume wengi hawatumii saana haya maneno kwani inaaminika kuwa WANAUME wanapenda sana kwa kutumia akili(kichwa) wakati WANAWAKE hupenda sana kwa moyo(kifua)!
 
wanaume wengi hawatumii saana haya maneno kwani inaaminika kuwa WANAUME wanapenda sana kwa kutumia akili(kichwa) wakati WANAWAKE hupenda sana kwa moyo(kifua)!

Asante Mkuu,
Ni wanaume wa wapi ndugu yangu kwa sababu nimeshasikia wanaume ( japo siyo watanzania) wakitumia maneno hayo kwa wenzao.
Kwani tofauti ya kupenda kutumia akili na moyo iko wapi hasa ....?
 
Hata kwenye vitabu vya dini wanaume wameambiwa wawapende wake zao na waishi nao kwa akili sana. Tofauti ya kupenda kwa akili, ni kukubali kosa, kukosoa/kukosolewa, kusamehe na kusahau, ili hali kupenda kwa moyo ni kukiri kosa, kukosolewa/kukosoa, kusamehe na kutosahau. Kwa maneno mengine ni ile hali ya kusema " nitaonekanaje kama itakuwa hivi...!"
 
...Je kwenye mazingira yasiyo ya nyumbani, ni nani anapaswa kuita mwingine kwa majina hayo na jamii inatafsiri vipi?
Sema usikike ndugu yangu.

...ughaibuni kuitwa darling, love, sweetheart wala sio big deal achilia mbali kuminyiwa jicho, au kupewa busu!

Kwenye jamii zetu za kibantu, NI MARUFUKU! ...binafsi sithubutu kumwita mw'mke kwa majina hayo mbele ya 'mywife' wangu, na wala yeye hathubutu kutamka hayo kwa mw'ume mwingine nikayasikia, kwani inaleta tafsiri tofauti :)
 
hehehe mi sipendi kabisa kuitwa darling,mpenzi,sweet maana iwa naona ni wizi mtupu na si frahii kabisa na siwezi mpenzi wangu nimwite hivyo najisikia ovyo kabisa ukimwita jina lake kuna ubaya?Kama Mwanaharusi au Mwanaidi au Mwajuma hapo naona sawa.
 
Wanaonyesha sana. Mtu unapom-address mwenzako kama kichaa wangu...mwanangu...mpwa...kaka n.k....most of the time we do that affectionately.
Asante na nakubaliana nawe kuwa ni maneno ya upendo.

Lakini yana tofauti na darling, sweetie..... ni kama wanawake wanavyoitana shosti...shostito n.k. na hakuna mtu anashangaa wanapoitana hivyo na kuna wakati pia wanawake na wanaume pia wanataniana shosti japo huu ni utani wa wanawake zaidi.

Suali langu ni je, maneno yenye kuashiria upendo kwanini yanaeleta maswali pale mwanamke/mwanaume anapoyatumia kwa mtu ambaye hawana uhusiano wowote wa kimapenzi?
 
Suali langu ni je, maneno yenye kuashiria upendo kwanini yanaeleta maswali pale mwanamke/mwanaume anapoyatumia kwa mtu ambaye hawana uhusiano wowote wa kimapenzi?

Yanaleta maswali kama yepi? Unaweza kutoa mfano au mifano na muktadha (context) wa jinsi matumizi hayo yanavyoweza kuleta maswali...Thanks
 
Yanaleta maswali kama yepi? Unaweza kutoa mfano au mifano na muktadha (context) wa jinsi matumizi hayo yanavyoweza kuleta maswali...Thanks

Kwa mfano, ukikutana na office colleague njiani, kwa shauku ya kukuona akasema " Darling NN umepotea sana!" unadhani wanaosikia watapata taswira gani?
 
Kwa mfano, ukikutana na office colleague njiani, kwa shauku ya kukuona akasema " Darling NN umepotea sana!" unadhani wanaosikia watapata taswira gani?

Obviously hao innocent bystanders, kama wana common sense, watajua kuwa huyo mtu kasema hivyo kiupendo na sio upendo ule wa kimapenzi (mwanamme na mwanammke). Kwa sababu, kama huyo mtu akiwa mpenzi wangu, ni wazi siwezi kupotea kwake ki hivyo. Lazima tutakuwa na mawasiliano.

Sasa, kama ni njemba ndio inaniita darling...hakutakuwa na amani hapo. Katika lugha, kuna visheria visivyo rasmi vya matumizi ya lugha na jinsia. Wanawake kwa wanawake wanaweza kuitana hivyo. Lakini njemba kwa njemba kwa kweli haiji kabisa kuitana darling.
 
Nimeona kwenye majadiliano humu JF kuna watu wanawaita wenzao darling, sweetheart, dia ( ambayo ni dear ).... je inakuwaje?
 
Nimeona kwenye majadiliano humu JF kuna watu wanawaita wenzao darling, sweetheart, dia ( ambayo ni dear ).... je inakuwaje?

Well...humu kwenye forum tupo tupo na tunaenda kichwa kichwa tu bila hata kujua. Watu wako anonymous na hujui nani ni nani. Mtu anaweza akaji position kama mwanamke huku ni mwanamme.

Sasa kumwita mtu darling, sweetheart ama dear bila kujua jinsia yake ni makosa. But then again, this only a forum where many social laws can and are broken on a day to day basis.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom