Nani anasema nyumba za shirika la nyumba ni za watu wa kima cha chini?

kama unaweza kununua kiwanja chako,USINUNUE nyumba za NHC.
watanzani tumeshazoea kuhamia nyumba semi finished,unamalizia nyumba ukiwa unaishi humo humo after 5 years nyumba imeshakamilika ,kuna bustani na vikuku.nchi za ulaya e.g UK hawaruhusu mtu kujijengea nyumba na kuna sheria nyingi za kukuzuia.lakini kwa bongo 80% ya Ardhi haijawa surveyed so ni uwezo wako tu kujenga then unaanza kufanya survey na taratibu za kuhalalisha umiliki.
nyumba za NHC zenye thamani ni zile za mjini TU,upanga, na city centers mikoani,unachukua halafu unatafuta mpangaji atakayelipa pesa ya kutosha mkopo na visent vya kubakia kwa ajili ya ada za watoto etc.
ukichukua nyumba ya mkopo alafu ukaishi humo humo inakula kwako.

You were travelling in my mind brother. a good use of critical analyisis
 
NHC1.jpg



WATANZANIA watakaonunua nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa bei ya Sh milioni 25 kupitia mikopo ya benki saba zilizoingia mkataba na shirika hilo, watalazimika kulipa kati ya Sh milioni 63 na 75, kutokana na riba ya asilimia 15 na 19 itakayotozwa kwa miaka 15.


Huu ni wizi wa mchana kweupe. Sasa hivi nchi nyingi za magharibi kama unachukua variable mortgage rates (5 Years) utapata chini ya 3% na kama unachukua fixed mortgage rates (5 Years) ziko chini ya 4%.
 
Mkuu that is how it works, ukilipa taslim hakuna hiyo riba. Ukilipa say in 2 years unaweza kukuta unalipa say 30mln. All in all kwa mikopo ya nyumba ilitakiwa iwe in a tune of less than 10%, sasa sema hiyo hela yetu nayo haiko stable kabisa. Lakini pia kama alivyosema mchangiaji mmoja hapo juu it's far much better kuliko kulipa the same amount au 70% ya kulipa pango. Lakini pia ni opportunity kwani unaanza kuitumia nyumba hiyo immediately tofauti na nyumba nyingi unakuta mtu anaijenga taratibu for more than 20 years, umaliziaji baada ya mafao ya kustaafu.

Kuna Basic mortgage calculator hapa (Bonyeza Hapa) ingiza hizo figures mkopo, interest na muda wa malipo utapata picha pana ukizibadilisha badiliisha say miaka au interest rate.

Ni balaa, nimeizungusha kwa miaka 15, 15% mkopo wa $100,000 mtu anatakiwa alipe $322 kwa wiki, kwa mwezi $ 1400. Malaika wa bwana awe nanyi......... Amen
 
Ni balaa, nimeizungusha kwa miaka 15, 15% mkopo wa $100,000 mtu anatakiwa alipe $322 kwa wiki, kwa mwezi $ 1400. Malaika wa bwana awe nanyi......... Amen

Ndiyo hivyo mkuu, mambo mazuri yana gharama! hahaha ahahahahah!
 
Hi Ndo dawa ya Madalali wa nyumba kule sinza,
Kibanda kibovu unapangishwa sh 350,000,kudadeki ! Sasa wapangaji wote wa sinza tunaenda kwenye hii option .Kwa hii option pango la nyumba halipandi kwa miaka yote ntakayoamua kulipa deni ,kama ni 15yrs basi ni sh 350,000 kwa mwezi kwa hiyo miaka yoye hakuna those letters ukirudi toka offisini unakutana nayo Landlord akikuambia kutokana na kupanda kwa vifaa vya ujenzi anaongeza kodi kidogo(sometimes up to 50%).mbali ya hizo faida baada ya 15yrs namiliki nyumba pale ubungo buleeeee hahahaha it is too good to be true . Tibaijuka hoyeeeeee
 
Mazee, kama kuna mtu mwene data za UHAKIKA kuhusu hii kitu atumwagie, Kama vipi Uzi ufungwe, maana guessworks zinapoteza wakati.
 
Nyumba zipo au hazipo, Kama zipo zipo maeneo gani? Na wapi kwa kuzifuatilia? Usiniambie nikagoogle.
 
Nini hasa chanzo cha instability ya pesa zetu?(assuming that indeed interest rate is function exchange rate)

Demand vs supply ya dollar.....tunatakiwa kama nchi ku export zaidi...maana yake tuzalishe biidha zenye ushindani za kuuza ndani na nje kwa wingi badala ya kuenda kununua huko uchina...maana yake serikali kuweka mazingira mazuri kuanzisha viwanda hasa vidogo vidogo vyenye ufanisi vya uzalishaji humu humu nchini...kuwekeza kwenye elimu kwa wataalamu wa daraja la kati kama vile VETA....kuwekeza kwa vitendo kwenye kilimo!
 
mimi naomba tuu hizi nyumba zikikamilika ziwe na maji ya uhakika labda lile bomba linaloenda ikulu, labda kiyoyozi cha kwenda na wakati, waweke eneo la maana lakupaki magari. Wengine mnaweza mkaweka wish list zenu…..
 
mimi naomba tuu hizi nyumba zikikamilika ziwe na maji ya uhakika labda lile bomba linaloenda ikulu, labda kiyoyozi cha kwenda na wakati, waweke eneo la maana lakupaki magari. Wengine mnaweza mkaweka wish list zenu…..
 
Mimi napenda utendaji kazi wa CEO mpya wa NHC. Sijui lakini wenzake wako pamoja. Kwa sasa sijajua nini hasa ni madhumuni wa sera ya sasa ya NHC. Zamani kwa uelewa wangu ilikuwa NHC wajenge nyumba na zuzipangisha kwa watu.

Kwa sasa inaelekea kuwa mkakati wake ni kujenga na kuuza nyumba kwa Watanzania. Sasa napata wasiwasi kuwa nyumba hizo za kuuza zinalenga watu wenye kipato gani.

Kati nyumba 15,000 zinzotegemewa kujengwa , two thirds (10,000 units) zimelenga watu wenye kipato cha juu na kati.(nadhani kwa NHC, hawa ndiyo majority ya Watanzania). Ujenzi huu pia umelenga zaidi kwenye kuvunja nyumba za zamani na kujenga high rise buildings. Kwa kuwa nia ni kuuza , je NHC itabidi kuachia title deeds za hizi viwanja.

Kwa nini sera isiwe kupanua na kujenga makazi mapya na halafu baadaye warudi kuvunja zile za zamani na kuzijenga kwa mipangilio mizuri. Kitachotokea ni kuleta misangamano ya majumba na ukosefu wa parking za magari na matokeo yake ni kuharibu mandhari ya mji.

Sijui kama existing infrastructure ina weza kucope na existing expansion ya matumizi ya majengo haya mapya (siyo za NHC tu, pamoja nareal estate developers wengine). Tutegemee smog karibuni, water supply system kufaill , electricity supply na sewer system kufail.

Sijajua success ya mauzo ya projects zao mpya. (Dodoma na Arusha). Ngapi zimeuzwa na ngapi wamepangisha na ngapi bado. Wasiwasi wangu mwingine ni kutokea kwa watu wachache wenye uwezo wa kununua nyumba zaidi ya moja na wao kuwa mini NHC.

Hawa ndiyo watakuwa malandords.
 
Asante sana, It is a healthy thinking BUT If ONLY you have 25m CASH at hand. Mkopo is the best way to invest and run business

25m=kiwanja cha heka 1 chalinze +kibanda cha vyumba viwili na sebule + eneo kubwa na hewa tosha + eneo la mbele kujenga fremu za maduka + uwani kufuga kuku na mbuzi.....TO HELLLLL NA NYUMBA ZA 100SQUARE METER KATIKATI YA MJI WAKATI MIE MKULIMA.
 
Watanzania wenye uhakika wa kulipa deni basi sioni cha kuhofia hapo ni kuchangamkia fursa tena kwa pupa kwa sababu zifuatazo:

1.kwa wale wote wanaoishi nyumba au vyumba vya kupanga na wanataratibu za kulipa kwa mwaka ambayo ni majumrisho ya kodi ya kila mwezi tuchukue mfano Tshs.200,000/= unampa mwenye nyumba na unaweza kupanga kwa takribani miaka 10 na bado nyumba sio yako ni mali ya aliekupangisha.Sasa huoni NHC wanakuwezesha kumiliki nyumba kwa kuwalipa kiasi cha Tshs.200,000 kwa mwezi na baada ya miaka 15 mpaka 20 utamiliki hiyo nyumba?? Huu ni mchanganuo wa kawaida na ni wanyumba yenye thamani ya Tshs mil 25.

2.kwa kununua nyumba za NHC itakuwezesha kuchukulia mikopo benki nikimaanisha mara tu utakapo maliza deni hilo utapewa hati ya nyumba na itakuwezesha kukopea mkopo benki kwa ajiri ya biashara na shughuri zako zingine.NADHANI WENGI TUNAJUA UMUHIMU NA FAIDA ZA MIKOPO KAMA UTAUTUMIA KULINGANA NA MIPANGO.

3.Inakuwezesha kumiliki nyumba kwa uharaka zaidi kuliko ule utaratibu wa kujenga kwa kudunduliza,Hii ningependa watanzania waingalie kwa umakini maana wengi wanaojenga wanakua wamepanga kwenye nyumba au chumba sasa katika harakati za ujenzi anapokuwa amekwama mahali basi anasimamisha ujenzi ila anaendelea kulipia kodi kama kawaida kwenye hiyo nyumba aliyopanga na pesa inaweza ikawa na matumizi mengine yasiyo ya lazima ambayo ni hasara kwa mpangaji instead angeitumia hiyo ela kumalizia ujenzi wake.NHC imeyaona hayo yote na imetupa fursa watanzania kwenye swala la MAKAZI.

NHC imekuja na utaratibu mpya uliozoeleka kwenye nchi zilizoendelea sasa watanzania tuupokee na naamini utabadilisha makazi yetu.Kingine utakuza pato la raia watakao miliki hizo nyumba pia na pato la taifa kwa ujumla kwa kujenga nyumba zingine kwa faida itakayo patikana baada ya kuuza na kupangisha nyumba hizo.NHC IS OUR ONLY HELP IN REAL ESTATE DEVELOPMENT.
 
Shirika la UMMA kama NHC haliwezi kujenga nyumba ya bei nafuu kwa kuwa rushwa kubwa tu, wizi wa vifaa na manunuzi hewa ni sehemu ya ujenzi wa nyumba zenyewe. Ni vizuri NHC ikafikiria na njia zingine mbadala kama kuwapangisha watu huku wakizinunua taratibu nyumba hizo au kuwapa watu fedha ambao tayari watakuwa na viwanja vyenye hati.

Hapana wanaweza kwani jukumu la kujenga sio lao wao wanatangaza tenda labda nyumba ya 20 Mill kampuni inayoweza ije, mkandarasi akishajenga na NHC akiridhika ndio unalipwa chako na NHC anauza/kukopesha.
 
kama unaweza kununua kiwanja chako,USINUNUE nyumba za NHC.
watanzani tumeshazoea kuhamia nyumba semi finished,unamalizia nyumba ukiwa unaishi humo humo after 5 years nyumba imeshakamilika ,kuna bustani na vikuku.nchi za ulaya e.g UK hawaruhusu mtu kujijengea nyumba na kuna sheria nyingi za kukuzuia.lakini kwa bongo 80% ya Ardhi haijawa surveyed so ni uwezo wako tu kujenga then unaanza kufanya survey na taratibu za kuhalalisha umiliki.
nyumba za NHC zenye thamani ni zile za mjini TU,upanga, na city centers mikoani,unachukua halafu unatafuta mpangaji atakayelipa pesa ya kutosha mkopo na visent vya kubakia kwa ajili ya ada za watoto etc.
ukichukua nyumba ya mkopo alafu ukaishi humo humo inakula kwako.

Mkuu, kula 5 kwanza,

Halafu pia kula tano ingine pale unaposema ukiishi humo humo unakuwa unakula kwako -yaani unakuwa huja"invest" kwenye hio nyumba.

Upo sawa sawa na mawazo yangu, hakuna tatizo kabisa unanunua hiyo nyuma na unaipangisha (buy to lent).

Ukinunua nyumab kama hiyo unaifanyia "reasonable furnishing" kwenye maeneo yote ni lazima itapata wapangaji.
 
Pamoja na interest kuwa juu kiasi hicho bado naamini kuna unafuu na faida kubwa kununua nyumba kwa kutumia hii mikopo ingawaje mabenki na NHC hawajaweza kuwaelewesha wateja wake;
  • Je hii nyumba ambayo mteja atainunua kwa mil 25 itakuwa na dhamani gani baada ya kumaliza mkopo i.e kama equity > interest rate basi ni uwekezaji mzuri kwenye ununuzi wa hizi nyumba
  • Fikiria kwa mtu ambaye anapanga na analipa kodi ya nyumba kati ya 300,000/= to 500,000/=...hiii kodi inamnufaisha land lord na kwa mpangaji ni pesa inayopotea, lakini kwenye mkopo wa nyumba marejesho unayofanya inakua ni pesa yako mwenyewe maana baada ya kumaliza mkopo nyumba inakuwa ni mali yako na imepanda thamani yaani kutoka 25mil na kuwa hata zaidi ya 65mil ulizorejesha.
  • Faida nyingine ya ununuzi wa nyumba kwa mkopo ni njia mbadala ya kuweka akiba ya uzeeni..Mifuko ya penseni imeshindwa kukidhi mahitaji ya wastaafu wengi na ununuzi wa nyumba kwa mkopo ni ukombozi kwani wakati wa uzeeni baada ya kumaliza mkopo unaweza kupangisha hii nyumba na kulamba kodi ya kuendesha maisha ya uzeeni vinginevyo unauza na kupata cash ya matanuzi.

Mkuu unaona mbali.

Ila pia watu wa NHC ni wajanja kwani wanajenga tena estates nyingi ambazo ukipiga hesabu ya haraka haraka utaona ikiwa wanafanikiwa kuuza nyumba hizo ambazo ni kwa mtanzania wa kawaida, wanakuwa wanapata faida kubwa ukilinganisha na kama wangejenga nyumba hizo kila moja kwenye kiwanja chake.

Ila bado mtanzania mwenye wa maisha ya kawaida ambae amezoea kuishi pale tandika mabatini au pale kwa mtogole bado hio itakuwa ni ndoto ya kuishi kwenye nyumba hizo.
 
Mkuu unaona mbali.

Ila pia watu wa NHC ni wajanja kwani wanajenga tena estates nyingi ambazo ukipiga hesabu ya haraka haraka utaona ikiwa wanafanikiwa kuuza nyumba hizo ambazo ni kwa mtanzania wa kawaida, wanakuwa wanapata faida kubwa ukilinganisha na kama wangejenga nyumba hizo kila moja kwenye kiwanja chake.

Ila bado mtanzania mwenye wa maisha ya kawaida ambae amezoea kuishi pale tandika mabatini au pale kwa mtogole bado hio itakuwa ni ndoto ya kuishi kwenye nyumba hizo.

Mkuu NHC wako kibiashara 100% na wanakumua at the maximum..kwamba ni shirika la umma ndio litawasaidia wananchi wa kawaida ni siasa tu na kwa mtanzania wa kawaida na hata wa kati kuweza kununua nyumba hizi bado itakuani ndoto! Mahitaji ya nyumba kwa Tanzania ni makubwa sana na upatikanaji wake ni wa taabu kweli kweli, si ajabu hata hizo nyumba ambazo NHC wanazotangaza kuuza ukakuta zote zimeshanunuliwa.....Serikali lazima iweke mazingira mazuri (mfano kurahisisha upatikanaji wa viwanja vilivyopimwa na mitaji) kwa private developer kuweza kuingia uwanjani na kujenga nyumba za low cost ili kuleta ushindani!
 
nakumbuka system hii hii ya nhc ndo ilipelekea kutokea kwa financial crisis in US
 
Apartments za Ubungo nimeona kwene magazeti ya leo wanaziuza ila cha ajabu hawasemi ni kwa sh.ngapi.
 
What if ninayo cash ya 25mil na sitaki kupitia mambo ya benki????
 
Back
Top Bottom