Nani anasema nyumba za shirika la nyumba ni za watu wa kima cha chini?

Fani yangu ni ujenzi..najenga sana na nawajengea watu nyumba zao..
Nyumba haijengwi tu kwa mabati na matofali.. Kupandisha nyumba tu siyo kazi kubwa sana..complications zipo kwenye finishing

sasa finishing
umeambiwa tunamjengea jlo
au mfalme wa saudia arabia???????

mafundi wezi na wa gharama kama wewe siwataki
wapo mafundi wa bei poa.....

mambo ya tiles na gypsum hayo ni option

mimi nazungumzia nyumba standard ya kuishi mtu

vitu vingine wataweka wenyewe
 
Rejao
Mhm kwa kweli, na hiyo 40m yenyewe usidhani ni kiwanja kitacho toa na li garden, nop! Kwa kweli viwanja sikuhizi havishikiki

hacheni kwenda kwa madalali na kutafuta viwanja kariakoo,
hapa tunaongelea maneo ya kuishi, kama una nunua kiwanja cha kuisha TANZANIA kwa 40mil lazima uwe sharobaro
kuna maneno safi na viwanja bei nzuri,
sasa nyie muwe na njozi za kujenga nyumba sinza

Kuna nyumba mimi imekwisha ukonga kwa 30mil nyumba safi kabisa
ina vyumba 4, jiko, sebule , dinning, store and choo na bafu

naongelea nyumba ya kisasa kabisa na ni 50 kWA 30 FEET
MABATI HAYA YA KILEO
40MIL ni hela ndefu kwa ujenzi
90mil ya NHC ni wizi kama walivyozoea kuibia watanzania

matokea yake nyumba hazita uzika shirika litakwenda kwa harasa au kufa kabisa
ili shirika alita kuwa maana turnover yake itakuwa ndogo sana hakuna watanzania wa kutosha kuweza kununua nyumba ya 90mil
hata kama ni kwa mkopo wanaweza kulipa watukuu
kama wanajengea wabunge na vigogo sawa lakini kama wanajenga kwa ajili ya watanzania wajipange upya kukata cost ya ujenzi ili kujenga nyumba nafuu
 
Hivi kuna watu wao kila kitu ni kutetea tu? Kweli a normal Tanzanian anawezaje kuwa na 99m. Mbaya zaidi unatakiwa kukamilisha malipo ndani ya WIKI TATU TUU yaani kila wiki 33m we Rejeo unaakili sawasawa?
 
wewe unaonesha hujawahi kujenga kumbe..

mwenzio leo nimenunua mabati 70 na bati moja nimenunua 13,000=
piga mahesabu hapi

tofali moja sh 800 na nyumba ya vyumba vitatu wastani matofali 1500

piga mahesabu hapo...hata milioni kumi hap hatufiki...

mwenzio najenga as we speak....wait and see

Kwa hiyo ukishanunua Mabati na Matofali nyumba tayari?

Gharama zingine kama vile Tiles, Gypsum, Plaming, Umeme, Rangi, Saruji.

Na gaharama za Architecture au utajenga na mafundi wa mitaani ukuta unapimwa na kamba ya katani
 
umeona mlivyo wagonjwa?
nani kasema tiles na gypsum hapa?

umeme tanesco unalipa laki nne na sitini tu,wiring hata kama mafundi wa mitaani
wajeja wangu wakiridhika its okaay
 
Kwa hiyo ukishanunua Mabati na Matofali nyumba tayari?

Gharama zingine kama vile Tiles, Gypsum, Plaming, Umeme, Rangi, Saruji.

Na gaharama za Architecture au utajenga na mafundi wa mitaani ukuta unapimwa na kamba ya katani

walisema watajenga nyumba nafuu sasa TILES
wameweka za nini?
sakafu ya kawaida ina tatizo gani?
au na madirisha wameweka ya vioo
aisee harafu tunasema hii nchi tunakomboka tunawaza maisha ya peponi
 
hacheni kwenda kwa madalali na kutafuta viwanja kariakoo,
hapa tunaongelea maneo ya kuishi, kama una nunua kiwanja cha kuisha TANZANIA kwa 40mil lazima uwe sharobaro
kuna maneno safi na viwanja bei nzuri,
sasa nyie muwe na njozi za kujenga nyumba sinza

Kuna nyumba mimi imekwisha ukonga kwa 30mil nyumba safi kabisa
ina vyumba 4, jiko, sebule , dinning, store and choo na bafu

naongelea nyumba ya kisasa kabisa na ni 50 kWA 30 FEET
MABATI HAYA YA KILEO
40MIL ni hela ndefu kwa ujenzi
90mil ya NHC ni wizi kama walivyozoea kuibia watanzania

matokea yake nyumba hazita uzika shirika litakwenda kwa harasa au kufa kabisa
ili shirika alita kuwa maana turnover yake itakuwa ndogo sana hakuna watanzania wa kutosha kuweza kununua nyumba ya 90mil
hata kama ni kwa mkopo wanaweza kulipa watukuu
kama wanajengea wabunge na vigogo sawa lakini kama wanajenga kwa ajili ya watanzania wajipange upya kukata cost ya ujenzi ili kujenga nyumba nafuu

watanzania bana,utasema wamezaliwa marekani aisee
eti standard,na wanavaa mitumba,magari mitumba,but kujenga watakuambia eti unatumia mafundi wa mitaani
its funny...
 
NHC1.jpg

WATANZANIA watakaonunua nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa bei ya Sh milioni 25 kupitia mikopo ya benki saba zilizoingia mkataba na shirika hilo, watalazimika kulipa kati ya Sh milioni 63 na 75, kutokana na riba ya asilimia 15 na 19 itakayotozwa kwa miaka 15.

Hesabu hizo ni kwa mujibu wa Benki ya Azania, itakayotoza riba ya kuanzia asilimia 15, na KCB Bank (T) Ltd itakayotoza riba isiyopungua asilimia 19.

Benki nyingine zilizosaini makubaliano ya kutoa mikopo hiyo ya nyumba; BOA, NMB (T) Ltd, EXIM, CBA na NBC, pia zitatoza riba ya kati ya asilimia 15 na 20.

National-Housing-Corporation-NHC-300x2141.jpg

Wakizungumza kwa nyakati tofauti Dar es Salaam jana, wahusika wa mikopo ya nyumba katika benki hizo walisema Sh milioni 25 inayotangazwa na NHC ni fedha ambayo benki hizo zinapaswa kulilipa shirika hilo, kama malipo ya jumla ya nyumba moja, ambayo wateja hao wanapaswa kuyarejesha kwa benki husika pamoja na riba.

Ofisa Mikopo wa Azania, tawi la Dar es Salaam, Gulshan Saleh, aliiambia HABARILEO ofisini kwake, kuwa mteja atakayepewa na benki hiyo mkopo wa nyumba wa Sh milioni 25, kwa riba ya asilimia 15 kwa miaka 15 (miezi 180) atapaswa kurejesha Sh 349,896.78 kila mwezi, kwa kipindi hicho.

Kwa maelezo ya Saleh, kiasi hicho ni jumla ya riba ambayo ni Sh 312,500, pamoja na makato ya msingi ya Sh 37,396.78.

"Kutokana na mchanganuo huo, hadi kumalizika kwa mkopo, mteja atakuwa amelipa Sh. 2,981,420.34; Sh milioni 25 ikiwa ni marejesho yaliyolipwa na benki kwa NHC, na Sh 37,981,420.78 inayobaki kwa benki kama marejesho ya gharama za mkopo na faida," Saleh alisema.

Kwa upande wa KCB (T) Ltd, ofisa aliyezungumza kwa masharti ya kutotajwa gazetini, alisema riba yao kwa mikopo hiyo ya nyumba ni asilimia 19, ambayo hawatarajii kuipunguza kutokana na sababu mbalimbali.

Alifafanua, kuwa mteja atakayepewa mkopo wa nyumba wa Sh. milioni 25 atailipa KCB Sh 420,719.01 kwa mwezi, ambayo ni jumla ya makato ya msingi na riba.

"Kwa hesabu hizo, hadi kukamilisha mkopo wake wa miezi 180 (miaka 15) katika benki yetu, mteja atakuwa amelipa Sh. 75,729,421.8 , ambapo Sh. milioni 25 zitakuwa ni marejesho kwa fedha ambazo NHC itakuwa imelipwa kwa niaba yake, wakati Sh. 50,729,421.8 ni gharama ya mkopo na faida," alisema ofisa huyo.

Kutokana na hesabu hizo, ambazo wahusika walieleza kuwa ni za awali, mfanyakazi anayeweza kununua nyumba ya Sh milioni 25 kupitia mkopo wa benki wa muda huo mrefu ni mwenye kipato kinachoweza kuruhusu theluthi mbili ya makato kwa ajili ya mkopo huo na kubakiwa na thekuthi moja ya kuendeshea maisha.

Hiyo ni baada ya makato mengine ya lazima, kama vile NSSF, PAYE na mengineyo kama yapo.

kutoka kwa magangaone blog
 
Kwa wale wanaopenda habari kwa ufupi nyumba za kima cha chini ni ela ya madafu milioni 25. Mkopo kutoka kwa mabanki wanaweza kukulangua riba kuanzia 15 mpaka 19 ukichukua mkopo kwa banki yenye riba zaidi ndo itakuumiza zaidi. Sasa hapo kama wataka mkopo lazima uangalie banki inayotoa 15 riba kwenda chini usifaidishe fisadi.
 
Pamoja na interest kuwa juu kiasi hicho bado naamini kuna unafuu na faida kubwa kununua nyumba kwa kutumia hii mikopo ingawaje mabenki na NHC hawajaweza kuwaelewesha wateja wake;
  • Je hii nyumba ambayo mteja atainunua kwa mil 25 itakuwa na dhamani gani baada ya kumaliza mkopo i.e kama equity > interest rate basi ni uwekezaji mzuri kwenye ununuzi wa hizi nyumba
  • Fikiria kwa mtu ambaye anapanga na analipa kodi ya nyumba kati ya 300,000/= to 500,000/=...hiii kodi inamnufaisha land lord na kwa mpangaji ni pesa inayopotea, lakini kwenye mkopo wa nyumba marejesho unayofanya inakua ni pesa yako mwenyewe maana baada ya kumaliza mkopo nyumba inakuwa ni mali yako na imepanda thamani yaani kutoka 25mil na kuwa hata zaidi ya 65mil ulizorejesha.
  • Faida nyingine ya ununuzi wa nyumba kwa mkopo ni njia mbadala ya kuweka akiba ya uzeeni..Mifuko ya penseni imeshindwa kukidhi mahitaji ya wastaafu wengi na ununuzi wa nyumba kwa mkopo ni ukombozi kwani wakati wa uzeeni baada ya kumaliza mkopo unaweza kupangisha hii nyumba na kulamba kodi ya kuendesha maisha ya uzeeni vinginevyo unauza na kupata cash ya matanuzi.
 
usiwe na haraka kwani ukitaka faida nunua kwa wale walioingia kwenye mkopo na wanashindwa kuendelea
 
Shirika la UMMA kama NHC haliwezi kujenga nyumba ya bei nafuu kwa kuwa rushwa kubwa tu, wizi wa vifaa na manunuzi hewa ni sehemu ya ujenzi wa nyumba zenyewe. Ni vizuri NHC ikafikiria na njia zingine mbadala kama kuwapangisha watu huku wakizinunua taratibu nyumba hizo au kuwapa watu fedha ambao tayari watakuwa na viwanja vyenye hati.
 
He hii kazi afadhali njijengee kidogokidogo hicho kibanda changu huku kwa Mtogole kwanza naweza hata kufuga kuku na nguruwe kwenye eneo langu
 
NHC1.jpg

WATANZANIA watakaonunua nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa bei ya Sh milioni 25 kupitia mikopo ya benki saba zilizoingia mkataba na shirika hilo, watalazimika kulipa kati ya Sh milioni 63 na 75, kutokana na riba ya asilimia 15 na 19 itakayotozwa kwa miaka 15.

Hesabu hizo ni kwa mujibu wa Benki ya Azania, itakayotoza riba ya kuanzia asilimia 15, na KCB Bank (T) Ltd itakayotoza riba isiyopungua asilimia 19.

Benki nyingine zilizosaini makubaliano ya kutoa mikopo hiyo ya nyumba; BOA, NMB (T) Ltd, EXIM, CBA na NBC, pia zitatoza riba ya kati ya asilimia 15 na 20.

National-Housing-Corporation-NHC-300x2141.jpg

Wakizungumza kwa nyakati tofauti Dar es Salaam jana, wahusika wa mikopo ya nyumba katika benki hizo walisema Sh milioni 25 inayotangazwa na NHC ni fedha ambayo benki hizo zinapaswa kulilipa shirika hilo, kama malipo ya jumla ya nyumba moja, ambayo wateja hao wanapaswa kuyarejesha kwa benki husika pamoja na riba.

Ofisa Mikopo wa Azania, tawi la Dar es Salaam, Gulshan Saleh, aliiambia HABARILEO ofisini kwake, kuwa mteja atakayepewa na benki hiyo mkopo wa nyumba wa Sh milioni 25, kwa riba ya asilimia 15 kwa miaka 15 (miezi 180) atapaswa kurejesha Sh 349,896.78 kila mwezi, kwa kipindi hicho.

Kwa maelezo ya Saleh, kiasi hicho ni jumla ya riba ambayo ni Sh 312,500, pamoja na makato ya msingi ya Sh 37,396.78.

“Kutokana na mchanganuo huo, hadi kumalizika kwa mkopo, mteja atakuwa amelipa Sh. 2,981,420.34; Sh milioni 25 ikiwa ni marejesho yaliyolipwa na benki kwa NHC, na Sh 37,981,420.78 inayobaki kwa benki kama marejesho ya gharama za mkopo na faida,” Saleh alisema.

Kwa upande wa KCB (T) Ltd, ofisa aliyezungumza kwa masharti ya kutotajwa gazetini, alisema riba yao kwa mikopo hiyo ya nyumba ni asilimia 19, ambayo hawatarajii kuipunguza kutokana na sababu mbalimbali.

Alifafanua, kuwa mteja atakayepewa mkopo wa nyumba wa Sh. milioni 25 atailipa KCB Sh 420,719.01 kwa mwezi, ambayo ni jumla ya makato ya msingi na riba.

“Kwa hesabu hizo, hadi kukamilisha mkopo wake wa miezi 180 (miaka 15) katika benki yetu, mteja atakuwa amelipa Sh. 75,729,421.8 , ambapo Sh. milioni 25 zitakuwa ni marejesho kwa fedha ambazo NHC itakuwa imelipwa kwa niaba yake, wakati Sh. 50,729,421.8 ni gharama ya mkopo na faida,” alisema ofisa huyo.

Kutokana na hesabu hizo, ambazo wahusika walieleza kuwa ni za awali, mfanyakazi anayeweza kununua nyumba ya Sh milioni 25 kupitia mkopo wa benki wa muda huo mrefu ni mwenye kipato kinachoweza kuruhusu theluthi mbili ya makato kwa ajili ya mkopo huo na kubakiwa na thekuthi moja ya kuendeshea maisha.

Hiyo ni baada ya makato mengine ya lazima, kama vile NSSF, PAYE na mengineyo kama yapo.

kutoka kwa magangaone blog

ukiamua kulipa mkopo kwa miaka 7 badala ya 15, malipo kwa mwezi 464.286. Interest rate why so high compared to Europe where typical mortgage rates in range 3 to 4 %?
 
Hapo kwenye red mkuu....sababu ni stability ya pesa yetu...leo 1US$=1700TZS.... je baada ya miaka 15 itakuaje?

Nini hasa chanzo cha instability ya pesa zetu?(assuming that indeed interest rate is function exchange rate)
 
Back
Top Bottom