Nani anafaa kuwa waziri mkuu baada ya Pinda?

TUNTEMEKE

JF-Expert Member
Jun 15, 2009
4,587
579
Habari zilizopo ni kwamba jk yupo kwenye wakati mgumu sana akifikiria ni nani hashwa anaweza kuwa mbadala wa Pinda.Maoni na mawazo yetu ni muhimu.
 
Habari zilizopo ni kwamba jk yupo kwenye wakati mgumu sana akifikiria ni nani hashwa anaweza kuwa mbadala wa Pinda.Maoni na mawazo yetu ni muhimu.
Mkuu JK mlikutana wapi akakuambia kwamba yuko kwenye wakati mgumu na kisha kukuomba msaada??
 
Habari zilizopo ni kwamba jk yupo kwenye wakati mgumu sana akifikiria ni nani hashwa anaweza kuwa mbadala wa Pinda.Maoni na mawazo yetu ni muhimu.

Magufuli akamatishwe ishu hiyo..au la bora kumrudisha EL
 
Edward N. Lowasa (Laigwenan). Heshima ya CCM itarudi upya na kwa kasi kubwa.
 
Mkuu JK mlikutana wapi akakuambia kwamba yuko kwenye wakati mgumu na kisha kukuomba msaada??

habari toka vyanzo nyeti vilivyo karibu na Ikulu.Toa mapendekezo yako uenda yakafanyiwa kazi na sio baada ya jk kuteua ndio uanze kulalamika.,nafas ni yako
 
Hakuna anayefaa... Labda amwombe Mama Maria Nyerere tu ndiye ninayemwona anafaa CCM.. lasivyo wampe Slaa atengeneze njia nzuri zaidi...
 
habari toka vyanzo nyeti vilivyo karibu na Ikulu.Toa mapendekezo yako uenda yakafanyiwa kazi na sio baada ya jk kuteua ndio uanze kulalamika.,nafas ni yako
Mkuu, mimi pendekezo langu ni wewe.
 
Edward N. Lowasa (Laigwenan). Heshima ya CCM itarudi upya na kwa kasi kubwa.

miongoni mwa mambo aliyokataa kabisa ni kumrudisha Lowasa pia inasemekana hata Lowasa mwenyewe hayuko tayari kukirudia kiti hicho akikwepa kuonekana yeye ndiye anayesababisha serikali kuyumba ili apate tena uPM.
 
Kwa case ya CCM hakuna hata mmoja maana wote wameasi na kugeukia mbali na uso wa MUNGU wakiidharau sauti ya watu wa MUNGU ambao kwao hulia usiku na mchana wakimlilia MUNGU wao juu ya uovu na uonevu unaofanywa na tawala zilizoko madarakini dhidi ya utu, mali na heshima zao. Hata washindwe kumwabudu na kumtumikia MUNGU wao katika ROHO na kweli
 
Nani amekundanganya kuwa Pinda sio waziri Mkuu Hadi 2015.

Tatizo Watanzania hawanjui kabisa Rais wao lakini Rais wao anawajua na kwaelewa Watanzania kuwa hawana Janja yeyote! Hawamuwezi ... na upepo utapita tu... !!
 
Apewe mzee wa kiraracha kwani naona afya yake babu wa loliondo kairudisha. Nasikia hatumii tena rv.
 
Kwa maslahi ya CCM napendekeza Magufuli. Kwa maslahi ya nchi napendekeza, Dr Slaa anaweza sana hii kazi. Ikishindikana kumweka dr basi Zitto anaiweza hii kazi. Hata hivyo Zitto hana uzoefu wa kutosha kwa ofisi kama hii, ila kwa uwezo wa Mungu anaweza kama akimtegemea.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom