Nani anafaa kuwa Rais kutoka vyama vya upinzani?

HAKUNA RAISI UPINZANI ZAIDI YA DEVOTA (dovutwa) FAHIM, yeye ndo ataleta siraha na viwanda vyake na kama saizi watu wamegoma ni risasi kwenda mbele! Huyu ndo raisi asiye ajaye!
 
kauli yako mzee wa mawe inaonyesha uoga fulani ndani yake... nafikiri kuna mtu alichangia hoja ya mafuta jana kwa ufasaha sana na unahofia nafasi yake uko mbeleni... watanzania tunaona kwahiyo maneno ya fitna hayawezi kutubadilisha msimamo wetu.
 
Hebu subiri kidogo kuna mtu anataka kujichomeka kwenye foleni hapa sheli, Oyaaaaaa mpushi huyo apange nyuma.
 
Endapo tunataka kufanya mabadiliko inatubidi tuwe makini tusije fanya mabadiliko ya kumuweka kiongozi atakaye kuwa kioja, hivyo inatakiwa tuwe makini kwani upande wetu wa upinzani tunaudhaifu ya wagombea wetu tuwe makini tuwachunguze, kwa makini tusije pata Rais mropokaji, mwenye maamuzi ya jazba, hana busara, hekima, mbinafsi, mdini na si mzalendo Nawaomba wanajf katika kujadili hili tusisukumwe na utashi wa udini, ukabila na ukanda
<br /> <br / jieleze vizuri hao toa majina ya wapinzani na tabia zao za ubinafs,udini, ukabila, uropokaji nk.NA WW UNAMPENDEKEZA NANI TK CHAMA CHAKO CHA MAGAMBA?
 
jieleze ufahamike , acha kubwabwaja!
we kama bado mpaka sasa hujui ukombozi uko wapi, basi
NI BORA UKAFUNGUA CHAMA CHAKO NA SISI tutaKUSUPPORT!

"BORA UWE MJINGA KWA HOJA HUKUSOMA KULIKO KUWA MJINGA KWA HOJA UMESOMA"
 
Endapo tunataka kufanya mabadiliko inatubidi tuwe makini tusije fanya mabadiliko ya kumuweka kiongozi atakaye kuwa kioja, hivyo inatakiwa tuwe makini kwani upande wetu wa upinzani tunaudhaifu ya wagombea wetu tuwe makini tuwachunguze, kwa makini tusije pata Rais mropokaji, mwenye maamuzi ya jazba, hana busara, hekima, mbinafsi, mdini na si mzalendo Nawaomba wanajf katika kujadili hili tusisukumwe na utashi wa udini, ukabila na ukanda

Mimi nashangaa sana, hili suala la ukabila, udini alivlitumia sana Kikwete kwenye kampeni zake, hii inaonyesha wazi wazi kuwa huyu jamaa ni mdini na mkabila sana, au ilikuwa defence mechanism ya kujitetea kwa Watanzania asiojua hata kuwatumikia ili wamwonee huruma?, Mwalimu katika falsafa yake alichukia sana watu wanaoeneza ukabila, udini sio tu kwa matendo hata kutamka tamka. Mimi sioni mantiki yoyote kuhusu Ukabila na Udini, make Watanzania tumekuwa tukiisshi kama kitu kimoja tangu hata kabla ya Uhuru. Ukisoma historia, Mwalimu asingepata support yoyote ya kudai uhuru kama asingepata support ya waislamu na Wakristo wote kwa ujumla. Tuachane na hizi itokadi chafu zenye lengo la kuwafanya wengine wasiweze kuwatumikia watanzania eti tu wakipewa madaraka watakuwa wakabila, wadini.......mbona hata hawa tuliowachagua sioni wanachokifanya zaidi ya kunenepesha matumbo yao na watoto wao?????? Lets wake up people, hii nchi ni ya watu wote, sio minority tu wanatakiwa kutawala, tunataka hata haya makabila makubwa tuone yakitawala Tanzania, tuachane na dhana mbovu.
 
Ni upuuzi kujadili suala la urais kwa sasa wakati kuna mambo kibao ya kitaifa yapo mbele yetu. MUDA UKIFIKA TUTAMJUA.
 
Endapo tunataka kufanya mabadiliko inatubidi tuwe makini tusije fanya mabadiliko ya kumuweka kiongozi atakaye kuwa kioja, hivyo inatakiwa tuwe makini kwani upande wetu wa upinzani tunaudhaifu ya wagombea wetu tuwe makini tuwachunguze, kwa makini tusije pata Rais mropokaji, mwenye maamuzi ya jazba, hana busara, hekima, mbinafsi, mdini na si mzalendo Nawaomba wanajf katika kujadili hili tusisukumwe na utashi wa udini, ukabila na ukanda
<br />
<br />
Inaonekana hukujiandaa kabla ya kutoa hii hoja.Upande wa upinzani kuna viongozi wengi tu wanaoweza kutawala vizuri.Kidini Tanzania iko almost 50-50. Hakuna raisi anayeweza kutawala kidini Tanzania na akafanikwa. Hizo ni porojo tu za wanasiasa. Wewe nyumbani kwako una mke una watoto wa kiume na kike.Je unaweza kutawala nyumba yako Kiume au kike ukafanikiwa? Uropokaji si tatizo kama unatatua shida za watu wako.Kuna mifano ya maraisi waliokuwa waropokaji lakini wametatua matatizo ya watu wao na wameonyesha uzalendo mkubwa. Tuna maraisi wakimya lakini legelege wametesa watu wao kwa kushindwa kuchukua maamuzi magumu.Nakushauri usome sana Historia kabla ya kuongea kitu chochote hadharani.
 
Ibrahim .H. Lipumba ndie pekee katika upinzani anaonekana anaweza kutuvusha hapa tulipo ikiwa kama tutampa urais, anafaa ana busara na hekima ni mzalendo na mchapakazi.
 
Back
Top Bottom