Nani anafaa kuchaguliwa kuwa mbunge?

Jatropha

JF-Expert Member
Apr 9, 2009
1,151
199
Ndugu wana jf naomba kuuliza swali ni yupi anafaa zaidi kuchanguliwa kuwa mbunge yule mwenye uwezo mkubwa wa kuibana serikali itimize wajibu wake kwa raia huku akiwa na uwezo mdogo sana wa kuwapigia magoti mawaziri wa serikali kuomba maendeleo kwa ajili ya jimbo la uchaguzi analotoka; au yule mwenye uwezo mdogo wa kiuibana serikali itimize wajibu wake kwa raia lakini mwenye uwezo mkubwa sana wa kuwaomba na mawaziri wa serikali na kufanikiwa kupata barabara, maji, shule, hospiatali n.k kwa ajili ya jimbo la uchaguzi analotoka?
 
Mwanye uwezo wa kuibana serikali itimize yale yote yaliyo wekwa kwa ilani zao na isiwe porojo tuu hapa.

Na tatizo lililopo ni siasa kutawala safa zote za serikali na pili serikali haitaki viongozi vihele hele kwa maana wanao ibwatukia serikali na kuikazi macho kila kukicha
 
...ni yupi anafaa zaidi kuchanguliwa kuwa mbunge yule mwenye uwezo mkubwa wa kuibana serikali itimize wajibu wake kwa raia huku akiwa na uwezo mdogo sana wa kuwapigia magoti mawaziri wa serikali kuomba maendeleo kwa ajili ya jimbo la uchaguzi analotoka; au yule mwenye uwezo mdogo wa kiuibana serikali itimize wajibu wake kwa raia lakini mwenye uwezo mkubwa sana wa kuwaomba na mawaziri wa serikali na kufanikiwa kupata barabara, maji, shule, hospiatali n.k kwa ajili ya jimbo la uchaguzi analotoka?




hao wote hawafai;

wa kwanza hatatusaidia kwa sababu wahindi watamuondoa kwa kutumia vuvuzela;


wa pili hatatusaidia kwa sababu serikali itaendelea kumpiga kiswahili kwa kigezo cha bajeti bado finyu;


atakayefaa ni yule atakayesimamishwa na chadema.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom