Nani amfanyie JK semina elekezi kuhusu "value for money."

Byendangwero

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
871
56
Kwa maoni yangu, kama kuna eneo rais ameonyesha mapungufu makubwa, ni katika kulinganisha gharama iliyotumiwa na faida iliyopatikana (value for money). Kwa mfano, hivi majuzi wakati akifungua semina elekezi kwa viongozi waandamizi serikalini pamoja na mambo mengine rais alisikika akiwahimiza viongozi hao kutotumia mda wao mwingi maofisini, bali wafanya ziara huko vijijini ili kuyajua matatizo ya wananchi. Kuna watu wengi hapa nchini na mimi nikiwemo, tunao ziona hizi ziara za viongozi huko mikoani kuwa ni mzigo mkubwa kwa uchumi wetu. Kwa hesabu za haraka haraka, inasemekana msafara wa viongozi wa juu serikalini ughalimu kati ya shs, 300-500 milioni kila siku. Kiasi hicho cha fedha kinatosha kujenga zahanati angalau mbili. Hii ina maana kiongozi huyo akifanya ziara ya siku 10 mikoani anakwamisha ujenzi wa zahanati siyo chini ya 20. Na faida inayotokana na ziara hizo ni kama hakuna, kwa sababu huko mikoani serikali ipo, na kama isingelikuwa inatimiza wajibu wake angalau baada ya ziara kama hizo tungelisikia wakuu hao wanachukuliwa hatua, jambo ambalo ni nadra kulisikia. Sasa ikiwa kila kiongozi na watendaji waandamizi serikalini wote watafanya ziara vijijini hiyio gharama ambayo hakuna uwezekano wa kuzaa matunda yeyote nani aikabili!
 
Kuna mada inayoendelea kujadiliwa humu ndani iliyotokana na uandishi wa ndugu A. Nguruno, Kama JK au wasaidizi wake wakiamua kuisoma na kuielewa, nadhani itakuwa semina tosha!
 
Juzi juzi alipita Mkuu mmoja kwenye ofisi ninakofanyia kibarua, akalazimisha apewe vocha za Voda za 50,000 na gari zake 2 zijazwe full tank!
Pia ameagiza kuwa watoto wake wanaosoma maeneo ya huku wafuatwe shuleni shule zikifunga, wakatiwe tikezi za ndege kurudi Dar!..yote hayo hayamo kwenye bajeti ya Ofisi, hivyo inabidi yafanywe kiujanja ujanja...my hairs!

Akamwambia mwandamizi wangu bila woga kuwa atajua mwenyewe jinsi ya kuzilipa na kuweka sawa mahesabu.

Ziara nyingi za hawa watu ni mizigo sana kwa wenyeji wao, na huwa wakiondoka tu, amani inaanza kurejea kwa kuchungulia!
Shida ni kwamba wanapiga mahesabu ya kunufaika zaidi na hizo ziara kuliko kazi waliyojia!
 
Katibu mkuu mstaafu Lut. Yusufu Makamba anaweza kutoa Semina sababu amekuwa kwenye uongozi wa juu zaidi ya miaka 30, pia nam-nominati asaidiane na kijana machachari, kijana wa Magamba a.k.a mwasisi wa CCJ, wasaidiane kazi hii.
 
Kama huyo afsa wa juu anadai apewe hizo favour kwa wanawe na hesabu irekebishwe, kauli kama hii inafanywa mara ngapi na mahesabu mangapi yamerekebishwa? JK unahitaji semina elekezi sana value ipi unaitaka hali hata mkurugenzi wa TBC alihudhuria semina yako? Are we serious? au mie nachanganya kuwa mkurugenzi wa TBC naye ni kiongozi wa wananchi kwa maana ya waziri? Kama sivyo nakubaliana na wenzagu kuwa matumboni ndo yanawapeleka vijijini na si huduma kwa wananchi.

Madiwani na wenyeviti wa halmashauri wafanye kipi?
 
Mh.alimaliza semina kwa kuwataka wanasemina waanze kuandaa uchaguzi wa 2015,na waanze kumuandaa atakayepokea kijiti. Haraka haraka apa naona ilikuwa officeparty ya wana wa ccm,kwa iyo igp,mkuu wa vikosi vya jeshi,makatibu,mawaziri,na wote waliohudhuria walipewa jukumu ilo. Alaf utaambiwa igp hana chama,upumbafu!
 
Juzi juzi alipita Mkuu mmoja kwenye ofisi ninakofanyia kibarua, akalazimisha apewe vocha za Voda za 50,000 na gari zake 2 zijazwe full tank!
Pia ameagiza kuwa watoto wake wanaosoma maeneo ya huku wafuatwe shuleni shule zikifunga, wakatiwe tikezi za ndege kurudi Dar!..yote hayo hayamo kwenye bajeti ya Ofisi, hivyo inabidi yafanywe kiujanja ujanja...my hairs!

Akamwambia mwandamizi wangu bila woga kuwa atajua mwenyewe jinsi ya kuzilipa na kuweka sawa mahesabu.

Ziara nyingi za hawa watu ni mizigo sana kwa wenyeji wao, na huwa wakiondoka tu, amani inaanza kurejea kwa kuchungulia!
Shida ni kwamba wanapiga mahesabu ya kunufaika zaidi na hizo ziara kuliko kazi waliyojia!

PJ Yaani hapo huyo boss anelekeza wizi, na mtu akishajua kurekebisha mahesabu ya boss wake na yeye ataanza kurekebisha mahesabu ya kwake kama alivyomfanyia boss, hawa wakuu hawana adabu kabisa na dhambi kwa Mungu, wanapewa kila kitu bado wanataka hata visivyo halali, taifa hili linahitaji kikombe kwa kweli
 
Value 4 Money tunaiweza sana sie wahasibu,kama mkulu akitutaka muelekeze,mara zote tunausike kufanya VMA,valuE 4Money audit. Hata Time Value for Money. Kazi ya kihasibu iyo!
 
Back
Top Bottom