Nani amewaloga wabunge wa CCM?

Alfu Lela Ulela

JF-Expert Member
Oct 29, 2010
1,255
77
Nilisikitishwa sana kuona unafiki uliovuka mipaka wa wabunge wa chama cha mapinduzi hususani kwenye uchaguzi wa Spika jana.

Kila mtu anafahamu mchezo uliochezwa na mafisadi kumwingiza Chenge dakika za majeruhi ili kuvuruga. na kweli akafanikiwa kuvuruga. matumaini ya watanzania kumwona tena yule mtetezi wa wanyonge aliyerejesha hadhi ya bunge mhe.Samuel Sitta ikadidimizwa na kile kilichoitwa usawa wa kijinsia.

Eti kamati kuu ya ccm ikaacha kuangalia uwezo wa mTu na vitu muhimu kama taaluma, wakaangalia kigezo kimoja tu kiitwacho ujinsia.

huu ni UBAGUZI. Kumchagua mtu kwa ajili tu ya ujinsia wake ni unyanyasaji wa kijinsia kwa yule aliyeachwa kwa ajili tu ya jinsia yake.

lakini nikategemea wabunge wachache wa ccm tuliowaamini kama Dr.Mwakyembe, na hata Sitta mwnyewe wangeleta mageuzi ya demokrasia nchini kwa kupinga udhalimu wa kamati kuu ya ccm kwa kutompa kura huyo aliyedhulumu haki ya wengine.

Lakini cha ajabu wakampa kura karibu wote ikimaanisha kuwa hata wale tulioowaaamini. hata Sitta? hata Mwakyembe nae?? kumbe ccm hakuna kundi la wapambanaji wala mafisadi. kuna kundi moja maarufu liitwalo wasanii. wanaotumia uwezo wao kucheza na akili za watanzania.

ama kweli ng"ombe mwenye michango huzaa ndama mwenye michango. Wabunge "wapambanaji wa ccm" kura zenu ziko wapi?? ni nani aliyewaloga??
 
Hizi mada za spika zinaumiza kichwa! Tusbiri bunge lianze tuone itakuwaje.
 
Ama kweli huu ni mwaka wa shetani, kila kitu ni maumivu ya kichwa--uraisi umechakachuliwa, hatujakaa sawa uspika nao umekuwa tena kitendawili!
 
kama ulikuwa hujui hivyo ndivyo ilivyo kama unakumbuka DR.Slaa alisha sema hakuna mpambanaji wa kweli ndani ya ccm ila wapo tu wanaowahadaa wapiga kura wao.!!!!!!!!
 
Kweli wamelogwa siku nyingi zilizopita hivi ni kwa nini Mgombea yoyote achaguliwe na watu wasiozidi 20 (CC) halafu anapelekwa kwenye Halmashauri nayo haibishi, ndio maana Zenj wakishoana kipindi cha Rais mpya wanabeza ngoja Dodoma wawachagulieni leo mpaka kwa Spika mambo ya NYERERE mpaka atoke Butiama
Inaelekea pabaya ipo siku VIJISENT au E.L atapitishwa na CC kugombea Urais wabunge na wajumbe wa Mkuano Mkuu watapitisha jina kwa NDIYOOO
Leo Spika kapitishwa kwa kura nyingi hata 6 na mkewe wakati wanajua wamepachikiwa m2 aliyelipiwa deni 1bn na mafisadi ili warudi madarakani (msininukuu ameshakanusha)
Hebu wabunge m-badilike muwe na kura za No kwa mambo mnayoyaona
 
Kama kuna siku nimewahi kukerwa na ccm basi leo ilikuwa too much.

Huwezi elewa kama lilikuwa ni bunge au kijiwe cha wavuta bangi. Kwanza mama Anna Makinda hana sifa ya kuendelea kuwa spika maana ameonesha upendeleo wa waziwazi kwa chama jinamizi cha ccm.

Mgombea kiti cha unaibu spika wa chadema ameulizwa swali na Stella Manyanya ambalo kikanuni lilikuwa nje ya utaratibu.

Tundu Lissu kama mwanasheria mbobevu akatoa ufafanuzi makini kuwa Manyanya aulize swali kuhusu hoja iliyopo mezani maana suala la CHADEMA kutomtambua rais si hoja iliyokuwa inajadiliwa. Hivyo Manyanya ajadili hoja na si kujadili uhusiano binafsi wa mtoa hoja na chama chake.

Kwa maana hiyo manyanya kikanuni amevuruga utaratibu.

Lakini ktk hali ya kushangaza kabisa ni Spika kusema eti Lissu ndiye aliyekiuka kanuni, eti ndiye aliyevuruga utaratibu kwa kumsaidia mgombea kujibu.

Nimesikitika sana,

nimetamani Sitta angekuwepo labda angekuwa msaada maana yeye ana uelewa kidogo wa mambo ya sheria.

Ni aibu mama Makinda (mtu asiye na uelewa wowote wa sheria) kupinga hoja iliyotolewa na NGULI WA SHERIA aliyefanya kazi mahakama kuu ya Tanzania kwa miaka mingi.

Lakini cha kushangaza zaidi ni kuona jinsi wabunge wa CCM walivyokuwa wanapayuka kishabiki.

Wakaweka mambo waliyotumwa na wananchi kando, wakaanza kushabikia itikadi za chama chao.

Hapo ndipo nilipoamini kuwa wabunge wa CCM hata wakipewa Mwanasesere wakadhibitishiwa kuwa ndiye aliyepitishwa na halmashauri ya chama chao, watampigia kura kwa ushabiki mkubwa hata kama upinzani wamesimamisha Profesa.

Maana ktk CCM itikadi kwanza uwezo baadae.

Nimepata hasira mno kuona namna CCM wanavyotumia vibaya madaraka waliyopewa na wananchi.

Nikasema laiti wananchi wangekuwa wanawasikiliza wasingekubali kuwachagua tena 2015.

Lakini nikagundua kuwa CCM mtaji wake ni wajinga, na wananchi wa majimbo mengi yaliyo chini ya CCM wako duni kielimu.

Kwa hiyo CCM wana uhakika kuwa hata wakicheza KIDUKU bungeni wananchi wao hawana upeo wa kuona, kwa hiyo watawachagua tu.

Hivi CCM ni CHAMA AU ZAHMA? Tafakari!!
 
Watanzania wanasubiri kwa hamu 2015 ili wakamilishe kazi waliyoanza mwaka huu 2005. Vyama vinavyoishi kwa propaganda, visubiri kuelekea jalalani.
 
Back
Top Bottom