Nani aliyepanga haya mauaji ya hawa Marais Abraham Lincoln na John Kennedy?

Mwanamke aliyetabiri kifo cha kennedy sio ndio yule Babushka lady anayetafutwa na alikuwapo wakati kenedy anauawa google babushka lady au cheki youtube


kwa msaada zaidi

The Babushka Lady is a nickname for an unknown woman present during the 1963 assassination of President John F. Kennedy who might have photographed the events that occurred in Dallas' Dealey Plaza at the time President John F. Kennedy was shot. Her nickname arose from the headscarf she wore similar to scarves worn by elderly Russianwomen (бабушка ? babushka ? literally means "grandmother" or "old woman" in Russian). The Babushka Lady was seen to be holding a camera by eyewitnesses and was also seen in film accounts of the assassination.[SUP][1][/SUP][SUP][2][/SUP] She was observed standing on the grass between Elm and Main streets and can be seen in the Zapruder film as well as in the films of Orville Nix,[SUP][3][/SUP] Marie Muchmore, and Mark Bell[SUP][4][/SUP] (44 seconds and 49 seconds into the Bell film: even though the shooting had already taken place and most of her surrounding witnesses took cover, she can be seen still standing with the camera at her face). After the shooting, she crossed Elm Street and joined the crowd that went up thegrassy knoll in search of a gunman. She is last seen in photographs walking east on Elm Street. Neither she, nor the film she may have taken, has yet been positively identified; no known photograph with her in frame captured her face, because in all cases she was facing away from the camera or (in the case of the Zapruder film) had her face obscured by her own camera.


Babushka-Lady.png






babushka-lady.jpg






babushka-lady1.jpg







 
C.T.U ....

Huyo "Mwanamke" hawajampata hadi leo??
 
Last edited by a moderator:
Mauaji yote hayo ni ya kupangwa,tena kwa ustadi wa hali ya juu.Hiyo ni mipango ya ILLUMINATI;genge la hatari linaloabudu shetani.Wanajiita 'The Elites One.'
 
Mauaji yote hayo ni ya kupangwa,tena kwa ustadi wa hali ya juu.Hiyo ni mipango ya ILLUMINATI;genge la hatari linaloabudu shetani.Wanajiita 'The Elites One.'
Illuminati ni watu gani mkuu?
 
Imetulia ni story nzuri pamoja na kwamba ni ndefu haichoshi kusoma nimeifowadi kwenye group langu
 
Ule msemo wa kuwa duniani ni wawili wawili una
ukweli ndani yake.Fuatilia maisha ya hawa marais
wa marekan JF KENNEDY na ABRAHAM LINCOLIN
utathibitisha ukweli.wengine husema ni mtu mmoja
aliyekufa na baada ya miaka mia akafufuka na kuwa
rais tena.
=======================================
Tukubaliane kwamba maswali ni mengi sana kuliko
majibu katika mambo haya. Kwa watakaofuatilia
kwa karibu zaidi mambo yanayotendeka
watagundua kuwa ukweli wa mambo ni tofauti
sana na jinsi tunavyoambiwa na kutakiwa tuamini.
Duniani kuna mambo yanayotokea kwa bahati
mbaya, lakini mengi tunayodhani ni ya bahati
mbayaau ni kujirudia kwa historiani mambo
yaliyopangwa kutukia. Na mengine yanaruhusiwa
yatokee, kama ilivyo kwa tukio la Septemba 11,
2001, au matukio mengine mengi ya Septemba
ambayo orodha yake haiwezi kutosha katika mada
moja ya hapa
Kuna mengi sana ambayo yanatokea na yalitokea
Marekani na dunia kwa ujumla ambayo hayana
majibu hadi leo,wengine wanadai huu ni upotoshaji
au ni uzishi tu
Ukigeukia Marekani si tu shamba la habari kwa
waandishi, bali pia ni bahari ya habari. Kama
nitakavyosema yanatia mashaka, tazama na haya
mengine, kisha uamue mwenyewe kama ni bahati
mbaya, au ni kujirudia kwa historia, au vinginevyo.
Mambo mengi (si yote) yanayotendeka Marekani
yamepangwa na, huenda, yamepangwa karne
kadhaa zilizopita na yanaendeshwa na watu
maalum. Hawa watu maalum ni pamoja na wale
walioanzisha mabenki na mashirika makubwa ya
dunia.
Mashirika yao yana alama zao wanazozijua wao
kwa wao, na dunia inaambiwa kuwa mashirika
hayo ni kwa ajili ya mustakabali mwema wa dunia.
Watu hawa, kwa nyakati tofauti, walitofautiana na
Marais wawili wa Marekani, John Kennedy na
Abraham Lincoln, na baada ya kutofautiana huko,
mwisho wa maisha ya Marais hao ulikuja haraka
kuliko ulimwengu ulivyotarajia.
Huenda wasomaji wasikubaliane na hilo wakidai
kuwa utafiti umepotoka, au umetegemea vyanzo
visivyojitosheleza. Lakini tutazame lile tunaloweza
kukubaliana, ambalo tunaweza kudai kuwa ni ama
sadfa, bahati mbaya au kujirudia kwa historia juu
ya Abraham Lincoln na John Kennedy.
Abraham Lincoln alichaguliwa kuingia katika Bunge
la Marekani mwaka 1846. John F. Kennedy naye
alichaguliwa kuingia katika Bunge hilo mwaka
1946. Hiyo ni tofauti ya miaka 100, au tuseme
karne moja tangu kutokea kwa tukio moja hadi
lingine. Pengine ni historia ilijirudia. Lakini kuna
mengi zaidi ya hilo.
Mwaka 1856 Lincoln hakupata kura za kumtosha
kupendekezwa kuwa mgombea Urais. Mwaka
1956 Kennedy naye alishindwa kuteuliwa
kugombea umakamu wa Rais 1956. Hiyo ni miaka
100 barabara.
Abraham Lincoln alichaguliwa kuwa Rais wa
Marekani mwaka 1860. John Kennedy
akachaguliwa kuwa Rais 1960. Katika mbio za
uchaguzi, Lincoln alimshinda Stephen Douglas
aliyezaliwa mwaka 1813. Kennedy naye alimshinda
Richard Nixon aliyezaliwa 1913.
Wote wawiliLincoln na Kennedywalijishughulisha
na haki za kiraia, na wote walisomea sheria. Wake
zaoMary Todd Lincoln na Jacqueline Bouvier
Kennedywalifiwa na watoto wakati waume zao
wakiwa Ikulu. Mtoto wa Lincoln aliitwa Edward
Baker Lincoln aliyefariki mwaka 1846 akiwa na
umri wa miaka minme.
Mtoto wa Kennedy, Patrick Bouvier Kennedy,
alifariki dunia mwaka 1963 katika muda wa saa 48
tangu alipozaliwa. Watoto wote hao walikuwa
wakitumia majina ya koo za mama zaoBouvier
(Kennedy) na Baker (Lincoln).
Wote wawili, Abraham Lincoln na John Kennedy,
waliuawa kwa kupigwa risasi siku ya Ijumaa na
walipigwa risasi kichwani. Tofauti ni idadi tu ya
risasi zilizopigwa.
Katibu wa Abraham Lincoln aliitwa Kennedy, na
katibu wa John Kennedy aliitwa Lincoln. Marais
wote wawili waliuawa na watu waliotoka kusini
mwa nchi hiyo, na wote, baada ya kuuawa,
walirithiwa na watu waliotoka kusini mwa
Marekani.
Marais wote wawili, Kennedy na Lincoln, walikuwa
na Makamu wa Rais waliokuwa na majina
ya Johnson. Makamu wa Rais wa Lincoln aliitwa
Andrew Johnson ambaye alikuwa mjumbe wa
Baraza la Wawakilishi mwaka 1847. Makamu wa
Rais wa Kennedy aliitwa Lyndon Johnson ambaye
alikuwa mjumbe wa Baraza la Wawakilishi mwaka
1947.
Warithi wao wote (Makamu wao wa Rais) waliitwa
Johnson. Andrew Johnson, ambaye alimrithi
Lincoln, alizaliwa mwaka 1808. Lyndon Johnson,
aliyemrithi Kennedy, alizaliwa mwaka 1908.
John Wilkes Booth, ambaye ndiye muuaji wa
Lincoln, alizaliwa mwaka 1838. (si mwaka 1839
kama ilivyodaiwa na masimulizi fulani ya historia).
Lee Harvey Oswald, ambaye alimuua Kennedy,
alizaliwa mwaka 1939. Ni tofauti tu ya mwaka
mmoja.
Wauaji wote wawili walijulikana kwa majina yao
yote matatu, na majina yao kila mmoja yana herufi
15.
Lincoln alipigwa risasi akiwa katika ukumbi
ulioitwa Ford kwa heshima ya aliyekuwa
mtengenezaji maarufu wa magari duniani aliyeitwa
Henry Ford. John Kennedy alipigwa risasi akiwa
katika gari lililoitwa "Lincoln" lililotengenezwa na
kampuni ya Ford Motor Company iliyomilikiwa na
Henry Ford.
Muuaji Booth, baada ya kumuua Lincoln, alikimbia
kutoka ukumbini alimofanya mauaji na
akakamatiwa katika bohari. Tofauti kidogo na
huyo, muuaji Oswald alikimbia kutoka katika
bohari na kukamatiwa ukumbini. Wauaji wote
wawili, Booth na Oswald, waliuawa kabla kesi dhidi
yao hazijaanza.
Rais Lincoln alizaliwa Februari 12, 1809 na kufariki
Aprili 15, 1865 akiwa na umri wa miaka 56. Rais
Kennedy alizaliwa Mei 29, 1917 na kufariki dunia
Novemba 22, 1963 akiwa na umri wa miaka 46.
Mwezi mmoja kabla Lincoln hajauawa alikuwa
katika eneo linalojulikana kama Monroe lililoko
Maryland, Marekani. Kwa upande mwingine, mwezi
mmoja kabla John Kennedy hajauawa alionekana
akiwa na mchezaji sinema maarufu aliyeitwa
Marilyn Monroe, ambaye waandishi wengine
wanadai kuwa alikuwa hawara yake.
Sinema peke yake iliyokamilika ambayo
inaonyesha mauaji ya John Kennedy ilitengenezwa
na mtu aliyeitwa Abraham Zapruder, na maelezo
yaliyokamilika yanayoelezea mauaji ya Abraham
Lincoln yaliandikwa na mtu aliyeitwa John
Zelfindorfer.
Mtoto wa Lincoln aliyeitwa Tad alizikwa Julai 16,
1871. Baadaye maiti ya mtoto huyo ilichimbuliwa
kutoka katika kaburi alimozikwa na kupelekwa
kuzikwa katika eneo lingine la makaburi.
Mtoto wa John Kennedy, JFK Jr., akirusha angani
ndege yake, alitoweka bila kujulikana alikokuwa na
hatimaye kukutwa amekufa pamoja na abiria wake
wawili waliokuwa katika ndege hiyo. Mmoja wao
alikuwa mchumba wake. JFK Jr., alifariki Julai 16,
1999 (tazama hizo tarehe). Baada ya kupatikana
maiti yake ilichukuliwa na kuzikwa upya.
John Kennedy na Abraham Lincoln, wote, kwa
nyakati tofauti, walisoma sheria na wote waliwahi
kufanya kazi jeshini.
Kennedy alichaguliwa kuwa Rais Novemba 8.
Lincoln alichaguliwa kuwa Rais Novemba 8.
Kennedy alikuwa mtoto wa pili katika familia yake.
Lincoln naye alikuwa mtoto wa pili katika familia
yake.
Wote wawili walitumia majina ya babu zao.
Kennedy alikuwa na watoto walioitwa Robert na
Edward, kadhalika Lincoln alikuwa na watoto
walioitwa Robert na Edward. Kennedy alizaa
watoto wanne, na Lincoln alizaa watoto wanne.
Lincoln alikuwa na daktari wake aliyeitwa Charles
Taft. Kennedy naye alikuwa na daktari wake
aliyeitwa Charles Taft. Lincoln alikuwa na rafiki na
mshauri aliyeitwa William Graham. John Kennedy
alikuwa na rafiki na mshauri aliyeitwa Billy Graham.
Inasemekana kuwa Billy na William ni majina
mawili yanayotofautiana katika kuandikwa lakini si
katika maana.
Chanzo kimoja cha habari kinasema kuwa mwaka
mmoja kabla Lincoln hajauawa alipokea barua 80
zilizotishia maisha yake. Kadhalika, chanzo hicho
hicho kinasema, mwaka mmoja kabla ya kuuawa
Kennedy alipokea barua 800 za kutishia uhai wake.
Barua za kennedy ni mara kumi ya zile za Lincoln,
lakini namba yake ni nane.
Lincoln aliuawa mbele ya mkewe na Kennedy
aliuawa mbele ya mkewe. Wake zao
hawakudhurika wakati wa mauaji ya waume zao.
Orodha hiyo inaweza kuendelea hadi tukajaza
kurasa nyingi za gazeti hili.
Kwa kutazama hilo, tunaweza kusema kuwa hiyo
ni ama sadfa, bahati au kujirudia kwa historia. Ni
rahisi kuamua haraka kiasi hicho. Haijulikani kama
ni historia ilijirudia ama vinginevyo, lakini angalau
tunaweza kukubaliana kuwa hiyo ndiyo hali halisi
na ya wazi.
Kwa kuitazama vyema historia ya Marekani,
utagundua kuwa Marais wote wa nchi hiyo
waliochaguliwa katika miaka inayoishia na 0,
ukiondoa mwaka 1840, ama waliuawa au walikufa
wakiwa madarakani kutokana na kile
kilichoonekana kuwa ni kifo cha kawaida.
Mwaka 1840 Marekani ilikuwa na Rais wa nane,
Martin Van Buren, aliyetawala kuanzia 1837-1841.
Kinachotia shauku zaidi ni kwamba matukio hayo
hutokea, au tuseme yalikuwa yakitukia, kila baada
ya miaka 20 kwa miongo mingi iliyopita.
Robert Ripley aliyekuwa mchoraji maarufu wa
katuni na mtunzi wa kitabu cha vichekesho chenye
jina Ripley's Believe It or Not katika jalada lake,
aliwahi kutaja mtindo wa kila miaka 20 ya vifo vya
Marais wa Marekani kati ya mwaka 1840 na 1920
kisha, katika sentensi moja iliyo chini ya katuni
moja, akaandika 1940!?
Aliweka alama ya ulizo kwa kuwa hakujua kile
ambacho kingetokea mwaka 1940 kwa sababu
kilichapishwa mwaka 1935, miaka mitano kabla ya
mwaka aliouwekea alama ya ulizo (?).
Ripley alikuwa akifikisha ujumbe kamili kwa
wasomaji wake, lakini kwa kuwa wengi
walimchukulia kama mchekeshaji tu, walipuuza,
lakini alijua yaliyokuwa yakitendeka. Alikuwa
akipitisha ujumbe wake kwa njia ya vichekesho, na
watu hawakuupokea.
1940!? ilidokeza kwamba Rais wa Marekani
aliyechaguliwa mwaka huo angekufa angali akiwa
Rais wa nchi. Je, Ripley alikuwa akichekesha tu?
Lilikuwa jambo la bahati mbaya au kujirudia kwa
historia hata Ripley akajua kwa hakika kile
ambacho kingetukia? Rais huyo hakufa akiwa
madarakani? Haya ni maswali ya kitoto?
Tangu alipokuja duniani Jumatatu ya Januari 30,
1882, kupitia kwa baba na mama yake, James
Roosevelt na Sara Delano Roosevelt, Franklin
Delano Roosevelt hakujua kuwa Jumanne ya Aprili
4, 1933 ndipo angekuwa Rais wa 32 wa Marekani.
Na hata baada ya kujua hivyo, hakujua kuwa kuna
mengine ambayo hakuyajua.
Wamarekani walimchagua tena mwaka 1936 dhidi
ya mpinzani wake, Alfred M. Landon. Tofauti na
marais wengi wa nchi hiyo, Roosevelt alitumikia
zaidi ya vipindi vitatu. Lakini hilo si muhimu kwa
maana ya Robert Ripley.
Alipochaguliwa kwa kipindi cha tatu mwaka 1940
dhidi ya Wendell Willkie, akatimiza kile
kilichotazamiwa. Ikajulikana kwa watu wachache
sana wa ulimwengu huu waliojua siri kuwa
angekufa akiwa madarakani.
Hata hivyo alisonga mbele. Ukaja uchaguzi
mwingine mwaka 1944, Roosevelt akamshinda
Thomas E. Dewey. Lakini hilo halikuondoa ukweli
kuwa alichaguliwa mwaka 1940. Alhamisi ya Aprili
12, 1945, Roosevelt, akiwa katika kipindi cha nne
cha kutawala kwake, akafa angali akiwa Rais.
Hiyo ni bahati mbaya? Au ni kujirudia kwa historia?
Kama twafikiri hivyo, tuwe makini zaidi. Mwanzoni
mwa karne ya 20 mwanamke mmoja wa Australia
aliyeitwa Foster Turner, akiwasiliana kwa njia
ya upepo na mtu aliyeitwa Arthur Conan Doyle,
walitabiri kuzuka kwa Vita Kuu I na matokeo yake.
Vyote alivyotabiri vikatokea. Je, alitabiri au alijua
mipango iliyokuwapo? (Soma kitabu cha Max
Freedom Long kiitwacho The Secret Science
Behind Miracles ).
Kitabu kiitwacho How to Succeed cha Brian Adams
© 2004 (uk. 5) kinasema hivi katika aya ya
pili: Mauaji ya John F. Kennedy yalitabiriwa na
mbashiri anayejulikana zaidi Marekani (mwanamke
ambaye hakutajwa jina). Alitaja kwa usahihi kabisa
wakati, mahali na tarehe ambayo mauaji hayo
yangefanyika. Kwa bahati mbaya, onyo lake
halikusikilizwa.
Huo tutauita utabiri? Huyu ni Rais aliyechaguliwa
mwaka 1960, mwaka unaoishia na 0, na huyo
aliyetabiri ni Mmarekani. Tunajuaje kama huyo
ambaye mwandishi Brian Adams anamwita
mbashiri alijua mipango ya kuwaua watu hawa
hata akajua wakati, tarehe na mahali ambapo
mauaji ya Kennedy yangefanyika?
Mwanamke huyo mbashiri ambaye kitabu hicho
hakikumtaja jina, siye peke yake aliyetabiri
kuuawa kwa Kennedy. Mbona Robert Ripley
mwaka 1935 alitabiri kifo cha Roosevelt miaka
kumi baadaye ambaye pia alifariki akiwa
madarakani? Je, hakuuawa? Au tuseme hakuuawa
kwa njia ile ile aliyouawa John Kennedy au
Abraham Lincoln?
Kwa kutazama vile vipindi vya kila miaka 20,
wanajimu wengi, au wale waliojiita wanajimu,
walibashiri kifo cha Rais John Kennedy mara
alipochaguliwa kuwa Rais mwaka 1960. kikatokea
hatimaye.
Kwa njia hiyo hiyo ilitazamiwa pia kwamba hata
Rais Ronald Wilson Reagan angeuawa au kufa kifo
cha kawaida angali Rais, jambo ambalo lilikaribia
kabisa kutimia.
Jumatatu ya Machi 30, 1981, akiwa na umri wa
miaka 70 na baada ya kukaa ofisini kwa siku 69 tu
tangu aapishwe, Rais Reagan alijeruhiwa kwa
risasi tano au sita zilizofyatuliwa na John Hinckley
(25) na kukimbizwa katika Hospitali ya Chuo Kikuu
ya George Washington kufanyiwa upasuaji.
Kilichostua ni rais wa Marekani George W Bush
ambae hakuuwawa hadi anatoka madarakani
Inasemekana kuwa sababu yeye na familia yote ya
Bush tangu vizazi vingi vilivyopita wanajua na
kushiriki mambo mengi huko Marekani. Hata
George (Baba) Bush alijua, na pengine (aliandika
mwandishi mmoja) alikuwa na mkono katika tukio
la Reagan wakati yeye akiwa Makamu wake wa
Rais.
Kwa kushangaza, marais waliochaguliwa katika
miaka iliyoishia na 0 wote walifariki wangali
madarakani na walikufa katika miaka inayoishia
na 1, 3 na 5. Kwa hiyo, mwaka 2005 ulikuwa
ndio wa George W. Bush. Lakini huo umepita.
Katika hili kuna mambo ya kutazama pia. Rais wa
12 wa Marekani, Zachary Taylor (1849-1850),
alifariki dunia akiwa madarakani. Lakini
hakuchaguliwa mwaka unaoishia 0. Alichaguliwa
mwaka 1848 na akafariki dunia mwaka 1850
kutokana na maumivu ya tumbo.
Ilisemwa kuwa ni kifo cha kawaida, lakini
uchunguzi unaodokezwa na vielelezo vingi vya
kihistoria ni kwamba bila kutambua Rais huyo
alilishwa sumu iliyochanganywa na kemikali nyingi.
Haikuwa lazima Taylor achaguliwe mwaka ule
wa 0. Mwaka 1991, ikiwa ni miaka 141 tangu kifo
chake, mwili wake ulifukuliwa kwa ajili ya
kufanyiwa uchunguzi upya kuthibitisha madai hayo.
Lakini, baada ya uchunguzi, serikali ya Marekani
ilisema madai hayo ni ya uongo. Hakuna
aliyetazamia serikali ingesema madai hayo ni ya
kweli, kwani kwa kufanya hivyo ingekuwa serikali
ndiyo iliyomuua Rais wao na hivyo kuharibu rekodi
ya Marekani.
Tazama orodha ya marais hao ilivyo (miaka ya
kuchaguliwa kwao ikiwa katika mabano). Thomas
Jefferson (1800), alinusurika jaribio la mauaji dhidi
yake, hatimaye alifariki dunia Julai 4, 1826. James
Monroe (1820) naye alinusurika. Alifariki Julai 4,
1831.
William Henry Harrison (1840), alifariki akiwa Rais
Aprili 4, 1841 kutokana na kichomi(?). Abraham
Lincoln (1860), kama ilivyotajwa mara nyingi katika
makala hii, aliuawa Ijumaa ya Aprili 15, 1865.
Wengine ni James A. Garfield (1880) aliuawa Julai
2, 1881. William McKinley (1900), aliuawa
Septemba 19, 1901. Warren G. Harding (1920),
aliuawa Agosti 2, 1923 kwa kulishwa sumu
iliyowekwa katika chakula. Franklin D. Roosevelt
(1940), alifariki Aprili 12, 1945 kutokana na kile
kilichoitwa kiharusi, lakini kumbukumbu nyingi za
matibabu yake hazijawahi kupatikana. John F.
Kennedy (1960) aliuawa kwa risasi Novemba 22,
1963 na Ronald Reagan alikoswa koswa Machi 30,
1981, hata hivyo hatimaye akafariki dunia Juni 5,
2004.
Kuna marais wengine wa Marekani ambao
waliwahi kunusurika. Lakini hii inaonekana kuwa
ajali zaidi kuliko makusudi kama inavyoonekana
kwa wengine waliotajwa hapo juu.
Sasa ndugu zangu hii ni bahati mbaya au ni
kupangwa kwa haya matukio?
Kama yalipangwa ni nani aliyeyapanga?
 
Back
Top Bottom