Kwenye moja ya kipindi cha Meza ya Busara kinachorushwa na WAPO radio wiki hii nili msikia mmoja kati ya wachangiaji akisema UKAWA na CCM hakuna aliyebaki bungeni wote walitoka. Mchangiaji huyo alisema hayo akichangia kwenye mada iliyokuwa ikisema," UKAWA wametoka, Je! Nini Kifanyike?".
Mchangiaji huyo alisema CCM ndio walioanza kutoka pale walipotoka nje ya mjadala kwa mujibu wa sheria iliyowaweka pale. Alisema ukawa wao waliamua kutoka kabisa nje ya jengo la bunge. Nikiyaangalia mawazo ya huyu mtu ni wazi kuwa CCM walishatoka siku nyingi kwenye njia kuu, walichepuka kitambo tangu Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilipoanza kukusanya maoni. CCM ilikwaandaa watu na kuwaambia ni nini cha kuchangia.
Wakati wa Mabaraza ya Katiba hao CCM hawakujificha walionesha wazi kwamba wamechepuka. Kwa mantiki hiyo, UKAWA ndio walikuwa bungeni wakati CCM wamechepuka. Ukweli huu unajidhihirisha hata katika namna ya uchangiaji wa hoja. UKAWA walionesha dhahiri kwamba waliwafumbua macho na masikio wananchi waliowengi ambao hawakuwa wameisoma rasimu ya pili iliyowasilishwa. Na ni kutokana na hoja za UKAWA wananchi waliowengi wakaanza kuelewa katiba ni nini na inasema nini. Kwa kuwa CCM walikuwa wamechepuka basi hata hoja zao hazikuwa na mashiko. Na wakaamua kuzitia vibwagizo vya mipasho, matusi, kejeri na kila aina ya udhalimu walioweza kuuonesha.
Hata hivyo, kupitia radio WAPO siku hiyo watu waliochangia wengi takriban 80% waliunga mkono UKAWA kutoka nje. Wakasisitiza UKAWA wasirudi isipokuwa tu kama BMK litajadili rasimu iliyowasilishwa bungeni.