Nani alimuambia Mh. Rais maneno haya?

Kiresua

JF-Expert Member
May 13, 2009
1,184
259
Ndugu zangu wana JF, ni kipindi sasa tangu Mh Rais alipotoa salamu za mwaka mpya, napenda kuchukua fursa hii kumpongeza kwa hotuba nzuri lakini iliyokuwa na mapungufu kadhaa ambayo kwa tafsiri yangu yanabeba maana kubwa sana kwa mustakbali wa nchi yetu na maendeleo yake kwa ujumla. Napenda kuzungumzia maeneo ma 4 kama ifuatavyo;-

Usalama wa Nchi

niknukuu hotuba ya Raisi "…….Kuendeleza malumbano na kuendelea kuishi kama vile kampeni za uchaguzi bado zinaendelea siyo sahihi hata kidogo.

Najua wapo baadhi ya wanasiasa na vyama vya siasa ambavyo vimepanga mikakati ya kuendeleza malumbano ya uchaguzi na kutaka Watanzania waishi kama vile nchi ipo kwenye kampeni za uchaguzi.Wamepanga wakati wote kutafuta jambo au hata kuzua jambo ili kuwachochea wananchi waichukie Serikali. Wamepanga kuchochea migomo vyuoni na maandamano ya wananchi mara kwa mara. Kwao wao huo ndiyo mkakati wa kujijenga kisiasa ili kujiandalia ushindi kwenye uchaguzi wa mwaka 2015."
"………Wao hasa wanachotaka ni ghasia kutokea na vyombo vya dola kuingilia ati waiambie jumuiya ya kimataifa jinsi Serikali yetu ilivyo katili. "
Ninani aliye muambia Mh raisi kuwa migomo inyotokea vyuoni ni uchochezi wa wanasiasa? Kushindwa kwa Serikali kipindi kirefu kushughulikia matatizo ya wanafunzi, wanafikia hatua ya kugoma wanasingizia ni wanasiasa wanachochea. Mh Raisi acha kutufanya watanzania hatuna uwezo wa kupambanua mambo. Unataka kutuambia migomo iliyowahi kutokea ilichochewa na wanasiasa? Ni juzi tu tulisikia taarifa za Serikali ikikubali malalamiko ya wanafunzi UDOM na kusema ni yamsingi, na kukubali kufidia wanafunzi wote waliopotelewa na vitu vyao kutokana na vurugu. Hivi unataka kutumbia Mpaka wanasiasa wachochee migomo ndo mtoe haki za watu?. Karibuni pia katika Chuo Kukuu cha Ardhi hali kadhalika, serikali imekubali madai yao baada ya siku nyingi za kidiplomasia kukwama.
Nashindwa kukataa wito wa Viongozi wa vyama vya upinzani kuwa panapopindishwa haki yangu niidai kwa Nguvu, na hapa Mh Raisi ulituthibithia Hivyo na kwa kuliambia Taifa hivi ….tutanya migomo na kudai haki zetu kwa nguvu
Mh Raisi nani aliyekuambia haya, na kama uliambiwa ulidanganywa, na watendaji wako wasio na uwezo wa kutenda kazi na kwa kutofuatilia kwa undani unaonekana usiye makini, na Kama ni mawazo yako basi ni unatafuta mahali pa tupia lawama kwa serikali yako na watendaji wake kushindwa kazi. Na hili halikubaliki na watanzania hata kidogo kwani Tz ya leo si ile ulikuwa unadhania.
Matumizi ya fedha
Nanukuu hotuba ya Mh Raisi
"Kwa upande wa nidhamu ya matumizi bado hatujapiga hatua ya kunifanya nipoe moyo, ingawaje kuna mafanikio yanayoendelea kupatikana. Niliwakumbusha Mawaziri kuhusu kuwepo Kamati za Matumizi ya Fedha katika kila Wizara, Idara za Serikali na Halmashauri za Wilaya na Miji ambazo niliagiza ziundwe miaka mitatu iliyopita. Niliwakumbusha kuwa, wakuu wa taasisi hizo ndio wanaoongoza Kamati hizo na hivyo wao ndiyo wanaoongoza Kamati za Wizara zao"
Nani aliyekuambia kuwa ukituambia uliwaambia watendaji wako wawe na matumizi ya nidhamu utatuaminisha kuwa unafanya kazi ya kutosha na unadhamira ya kweli kutuondoa na umaskini nchi hii?
Nani aliyekuambia kuwa ukiwaambia watanzania kwamba uliwakumbusha kuunda kamati za matumizi ya fedha tutaakuamini kuwa kuna uadilifu nadni ya serikali yako?
Kwa nini usituambie kama kamati hizo ziliundwa na tayari kazi kadha wa kadha zimekwisha kufanyika, kama hazikuundwa ni kwanini? We vipi?
Na kama hazikuundwa basi watendaji wako walikudharau (kwa maneno mengine walikupotezea!) na wewe ulikiri kuwa juzi uliwakumbusha ina maana hawakukusikia miaka m 3 iliyopita. Nani aliyekuambia tunaamini kuwa una uwezo wa kutuongoza?
Bei ya Umeme

Na hapa tena nanukuu hotuba ya Mh Raisi
"Natambua kuwepo kwa mazungumzo, katika jamii kuhusu uamuzi wa EWURA wa kukubali ombi la Shirika la Umeme (TANESCO) kuongeza bei ya umeme. Wakati mwingine mazungumzo yamekuwa na hisia kali na hata jazba kutawala. Wizara, TANESCO na EWURA wameeleza kwa ufasaha misingi iliyotumika mpaka kufikia uamuzi huo. Sina maelezo mazuri zaidi ya hayo. Ninachotaka kusema mimi ni kuwaomba Watanzania wenzangu kutokukubali suala hili la kibiashara na kiuchumi kugeuzwa kuwa la kisiasa na kutafutiwa majawabu ya kisiasa. Naomba tuamini na kukubali maelezo ya TANESCO na EWURAkwamba katika miaka minne hii gharama za uendeshaji, uzalishaji, usafirishaji na usambazaji wa umeme zimepanda kama zilivyopanda katika shughuli nyingine"

Nani aliyekuambia tutakubali tuu kirahisi hivyo? Mh Raisi, kwa kushindwa kutuambia mikakati kamambe ya kuwa na umeme wa uhakika mfano pale Stingers Gorge hata kama utakuwa ni wa miaka 7, weka plan na uwaagize wataatlmu wako kila baada ya Mize 6 waumbie umma kuwa wamefanya kitu gani ndani ya kipindi hicho katika kufikia lengo hili la muda mrefu, hii kitu ya kutuambia.. …..unatuomba tukubali bei mpya ya juu zaidi ya zamani, hatuelewe ni nani aliyekuambia haya!!

Nani aliyekuambia kuwa kama bei hazitabadilika basi inatoa uhalali wa kubadilika leo, hata kama sio sahihi, Hapa hatukubaliani nawewe!!

Tuambie kwa takwimu madeni ya TANESCO, na nini nani anayengoza kwa kudaiwa deni kubwa (kama si wizara na idara za serikali yako) na ni kwanini halipi? Kwa sababu madeni ya shirika hili ndo yanayochangia kuwafanya washindwe kutoa huduma bora kwani ni fedha ambazo hawana!!!! Tufafanulie kwa undani kama ulivyo wahi kutuainishia kuhusu Richmond LLC, ukaeleza kwa kinagaubaga mpaka tukaamini. Kwa nini kwa hili la bei unasema huna maneno mazuri zaidi ya TANESCO? Wakati wakati ule ulikuwa na maneno mazuri sana?

NANI ALIYEKUAMBIA?

Katiba
Nanukuu hotuba ya Mh Raisi
"Kwa ajili hiyo ni vyema kuwa na Katiba inayoendana na mabadiliko na matakwa na hali ya sasa. Katiba ambayo italipeleka taifa letu miaka 50 ijayo kwa salama, amani, umoja na kuwepo maendeleo makubwa zaidi…… Katoeni maoni yenu mazuri yatakayowezesha nchi yetu kuwa na Katiba itakayokidhi matakwa yetu ya sasa na ya miaka 50 ijayo"
Nani aliyekumbia tukibadilisha katiba yetu itakuwa hai baada ya miaka 50 ijao? Huu ni mtizamo hafifu sana! Unafikiri kwamba makosa tuliyofanya miaka 50 iliyopita tutayafanya tena? Thubutuu!!!
Kutokubadilisha katiba yetu kwa kipindi cha miaka 50 ndo kulifanya taifa letu luwa masikini na kutawaliwa na matabaka na ufisadi wa kutisha. Nchi kuwekwa mikononi mwa matajiri halafu hatuna hata chembe ya uhuru wa kuwafikisha kwenye vyombo vya dola washughulikiwe.
Nani aliyekuambia kizazi kijacho kitakubali kurudia makosa mababu zao waliyoyafanya! I can tell u no one!!!
Katiba tutakayo andika upya itafanyiwa marekebisho au itaandikwa upya itakapobidi sio kutuambia ni mpaka 2061 hapana, hapa unateka fikra zetu.

Nakupongeza kwa nia yako nzuri ingawa inaonekana inayumbishwa na mafisadi wa fikra. Kwa maneno haya
"Na inapohusu Katiba ya Nchi itakuwa hasara tupu. Haitakuwa endelevu na kulazimika kufanyiwa marekebisho mengi mwanzoni tu baada yakutungwa".
Nahisi kuwa una nia ya kuandika katiba mpya na sio kufanyiwa marekebishao ile ya zamani, wanataifa hili wana wasiwasi niayako kwa sentensi hii na hapa nanukuu tena…
"Jambo la nne ambalo tulilokubaliana kufanya ni kuanzisha mchakato wa kuitazama upya Katiba ya Nchi yetu kwa lengo la kuihuisha ili hatimaye tuwe na Katiba inayoendana na taifa lenye umri wa nusu karne"
Sasa Mh Raisi ni kipi na ni upi Msimamo wako (KUHUISHA au KUANDIKA KATIBA MPYA?)

Samahani kwa Post Ndefu

Nawasilisha
 
Dalili za kushindwa. Mimi naona CCM washaanza kurusha mateke ya farasi anayekufa!!!
 
Ndio nini hiyo?,

Sisi tulimwambia, kama wewe hukumwambia si kaa kimya tu!
 
Ndio nini hiyo?,

Sisi tulimwambia, kama wewe hukumwambia si kaa kimya tu!

kazi ya kengele ni kukumbusha watu muda..... lakini kengele inatabu na kazi ngumu sana ..... huwa lazima ipigwe...... unapigwa
 
kazi ya kengele ni kukumbusha watu muda..... lakini kengele inatabu na kazi ngumu sana ..... huwa lazima ipigwe...... unapigwa

Ahsante kwa sifa njema! Mungu akuzidishie.
 
kazi ya kengele ni kukumbusha watu muda..... lakini kengele inatabu na kazi ngumu sana ..... huwa lazima ipigwe...... unapigwa

kengele inapigwa pande zote sasa hii kengele inapigwa pande gani?
 
mtoto wangu anapenda sana kuangalia laptop yangu.... ninawsiwasi sana asije akaichukia jumla sababu ya avatar yako.... samahani lakini

Haaa heheh kweli? Lakini nadhani inasaidia asiichezee manake watoto nao sometimes bila mkwara unaweza kukuta kaimwagia maji..
 
mtoa mada hii na alaaniwe yeye na kizazi chake.
mh! naanza kuwa na wasiwasi na huo u-great thinker, hivi mnapoteza hata dkka moja kufukiria kabla ya kuandika comment?
jamaa amejitahidi kuleta hoja mezani alafu watu mnaonga bila kufikiria, hoja inapingwa kwa hoja sio maneno maneno tu!
 
mh! naanza kuwa na wasiwasi na huo u-great thinker, hivi mnapoteza hata dkka moja kufukiria kabla ya kuandika comment?
jamaa amejitahidi kuleta hoja mezani alafu watu mnaonga bila kufikiria, hoja inapingwa kwa hoja sio maneno maneno tu!

Si unajua tena Bruce Lee halisi alishakufa...Sasa hawa waliobaki ndo hivyo kama unavyoona.
 
Huyo ndo kikwete kama hamumjui yeye ni bingwa wa kudandanywa na wasaidizi wake afu asijue anasonga mbele tu.
 
Back
Top Bottom