Nani alimpa u-'SIR' George Kahama?, Tanzania wenye cheo hiki wapo wangapi?

.
.
.
ndege ikaruka mara ya kwanza --- george akaguna...
ndege ikaruka mara ya pili -- george akaguna tena kwa sauti --mmmmnh (ule mguno wa kihaya)
iliporuka mara ya tatu -- nikamsikia george akipiga kelele -- maweeeee!!!!!

(RIP nyerere)

Acha kudanganya watu, hiyo speech JK. Nyerere alikuwa anamtania George Kahama (mtani wake kwa maana Nyerere ni wa Mara na Kahama ni wa Kagera), alikuwa anazungumzia ukabira bado upo nchini, watu wasijidanganye wakasema ukabila umekwisha Tanzania, alisema kukiwa na shida ya kweli kweli watu wanarudi mkwenye ukabila wao! Akamtania George kwa kusema aliwatuma kwenda Zaire (kwa sasa DRC):-
...ndege ikaruka mara ya kwanza, George Kahama akasema 'My God!' (yaani anajifanya ameendelea anajuwa kiingereza tu!)
...ndege ikaruka juu zaidi akasema 'Mungu wangu!'(woga umemuingia akarudi kwenye uswahili!)
...ndege ilipo ruka juuu zaidi akasema 'Maweeeeeh!' (woga umemshika zaidi akarudi kwenye ukabila!)

Nyerere alikuwa ni Mwalimu mzalendo wa kweli achana na hawa wanaowaza kila siku kudandia Fast Jet!
 
Sio kweli, hana wake wawili. Ana mke mmoja na hawala/malaya mmoja. Wakatoliki sheria ya Mungu na ya nchi inasema mke mmoja na mume mmoja. Rekebisha maandishi yako.

Usibishe mkuu.....ni kweli ana wake wawili tena wa tumbo moja......Janet ndiye mdogo....tuwape pole kwa kufiwa na mtoto wao!

images
 
laun hebu tujadili MAMBO ya maendeleo sio WATU! Huku ni kupoteza muda ambao ukienda HAURUDI!
 
Last edited by a moderator:
Wapi alipo huyu mzee ? Aliwahi kuwa waziri awamu ya kwanza na ya 3 . Na hiyo heshima ya kuwa sir aliipata kwa kufanya nini?
hiyo tiltle ilitokana na utani alikuwa akiitwa hivyo na rafike yake Mwl. Julius Kambarage Nyerere. Si Andy Chande ndiye pekee aliyepewa hiyo title na malkia
 
Usibishe mkuu.....ni kweli ana wake wawili tena wa tumbo moja......Janet ndiye mdogo....tuwape pole kwa kufiwa na mtoto wao!

images
safari, katisha sheria za kikatoliki, na sheria ya ndoa ya mwaka 1971, mkristo anakuwa na mke mmoja. Hivyo hichi kingine sio mke, ni malaya /hawala wake. SIO KWA DEFINITION YA MKE KWA MUJIBU WA CHRISTIAN FAITH/SHERIA YA NDOA YA MWAKA 1971 UNLESS HE PROFESSES PAGANISM/CUSTOMARY MARRIAGE!
 
kama kuna mtu atabisha na ana uhusiano nae akamuulize,wakati yupo CDA aliwahi kusafirisha vitu vyote vya ujenz kuanzia cement hadi madirisha usiku kwa gari na dereva ya CDA,kupeleka shinyanga,alimtesa sana yule dereva! ufisadi wa miaka hiyo!
 
alipata Sir kama jina la matani kutoka kwa Mwl nyerere kwani wakati Nyerere yuko Ulaya Bwana Kahama alikuwa anasomeshwa ulaya na chama cha kahawa kutoka Kagera na alikuwa na uwezo wa kumsaidia Nyerere hela za matamizi. hii wengi wetu tunaijua hata vyuonni kuna watoto wenye uwezo wa fedha kuliko wengin`!
 
Mkuu elmagnifico, ahsante kwa post yako, angalau imekata shauku yangu ya kutaka kufahamu huyu mzee angalau kwa uchache tu.
 
Last edited by a moderator:
Wadau hebu tukumbushane ni kitu garni alifanya George kahama mpaka malkia wa uingereza akamtunuku u sir
 
Nyerere baada ya kurudi toka China, alianza kuvaa ki-Mao. Wanasiasa wote wakamwiga (na waka acha baada ya Mwinyi kushika madaraka) isipokua Kahama ambaye aliendelea kuvaa suti. Kwa utani, akiwa amevalia suti, Mwalimu almwita Sir George. Tangu siku hiyo akawa anaitwa hivyo, and he didn't mind. Huyo u Sir hakutumukiwa na Elizabeth II, ALIBANDIKWA na Nyerere


Mkuu Archbishop Macinkus
Hili neno ni Kimau Lilianza kutumika tangu Enzi za askari wa Kijerumani kumaanisha gwanda lisilo na ukosi na si Ki-Mao.
 
Hivi huyu mzee Sir George bado yupo hai kweli maana last time nilipomuona alikuwa mdhaifu kiaina. hawa ndo wazee walioifaidi Nchi hii kwa muda mrefu.
 
Huyu mzee namuheshimu lakini wazee kama hawa wanaposhindwa kuwa active now kuisema na kuwasemea watanzania wanyonge sasa wakati tunawahitaji kuliko wakati wowote mpaka tunaomba Nyerere afufuke wao wapo wapo tu kazi kusifia serikali iliyopo madarakani.wasimame sasa tuzisikie sauti zao! Haina maana watu wazito ktk historia ya nchi kama yeye hata vijana hawamfahamu na yupo hai akiwa na akili timamu kabisa! Legacy haina mwisho na hatutaki kukumbuka historia yake tu bali hata sasa akiwa hai anatoa mchango gani? Mandela ametetea wanyonge mpaka kumsemea mbovu Bush hadi uzee ulipomzidi!! Hawa wanaokula pension tu alafu wanaisema serikali kiuoga hawatendei haki legacy wanayopewa na watanzania!!

Bora hata Mama Maria Nyerere angalau anajitahidi kuwaita waandishi na kuhusia mawili Matatu ...na Wastaafu wengine Kama Warioba ,na Cleopa
Mzee Kahama Kama waziri wa pekee wa Serikali ya kwanza aliyebakia anatakiwa kuongea mengi Zaidi ...Huo ni UJUMBE wetu kwake .
 
nadhani alikuwa KNIGHTED na Queen of England; hiko sio cheo by the way, you get that by doing 'significant' work to help people or if you make a 'notable' impact to the course of humanity; and OF COURSE If YOU are a citizenship of the Commonwealth Country;
 
Napenda kujua mtu mpaka anaitwa SIR awe na vigezo gan?. Halaf mbona sijawah sikia mwanamke akiitwa SIR!??. Karibun tujadili.
 
Back
Top Bottom