Elections 2010 Nani akipewa Uwaziri, Utashangaa, utasikitika au utafurahia?

yeyote aliyekuwa kwenye baraza la mawaziri lililopita akirudi ni balaaaaaaaaa........hakuna hata mmoja wao mpambanaji wa ufisadi.................inapokuja masuala ya kitaifa wote huinamisha vichwa chini wakitanguliza masilahi yake...........
 
Natamani kama baraza la mawaziri litakuwa hivi Magufuli PM. Sitta utawala bora, Ane Kilango mambo ya ndani, Mwakyembe mali asili na utalii, Ole telele ulinzi, Ole sendeka miundombinu, Mwandosya nishati na madini, Lucas Selelii Kilimo na chakula

sendeke akiwamo tutaraji mapya mengi ambayo sisi mmm hatutaki kwa makusudi kujali
 
hilo nalo kazi kwa vidole ng'ombe kwa remote ukibonyeza wanakwenda malishoni ukirudia wanakwenda kwenye maji just imagine
 
Nitashangaa JK asipomteua lowassa kuwa waziri katika serikali ya wiki ijayo.. kwa sasa lowasa ndiye mgombea mwenye usahwishi zaidi ndani ya CCM 2015. namuombea afya njema aje kupambana na DR SLAA.
 
Bula unafiki salama ya awamu ya nne ni kumrejesha edward ngoyai lowasa kitini wakamilishe zoezi la kuijenga awamu hii angalau legacy ionekane vema.
 
Mimi nitafurahi mheshimiwa Mrema akiteuliwa waziri wa mambo ya ndani. Wengine tumechoka na porojo na propaganda za majukwani ambazo hazimuongezei Mtanzanania tija hata siku moja.

Hii hapa nakubali lakini... Mrema akipewa high profile kama hiyo.. atawafunika wengine wengi.. as a matter of fact akipewa nafasi yoyote ile ya Uwaziri (which is highly unlikely) atakuwa juu sana na ata overshadow the stars of CCM. Ila Mambo ya Ndani watafurahia kurudi kwake.. kwani ni better kuliko aliyepita.. way better.
 
Ngeleja itabidi tu arudi pale madini...tangu achukue hatujasikia ufisadi kwenye wizara. Sintashangaa CCM wakimptisha kuwa mgombea wa Urais 2015
 
Prof Mark Mwandosya apewe Sayansi na Teknolojia,Magufuli PM,Ole Sendeka Miundombinu,Sita Sheria na Katiba,Membe apewe Maliasili na utalii,Jisia na watoto apewe Mma Kilango
 
Natamani kama baraza la mawaziri litakuwa hivi Magufuli PM. Sitta utawala bora, Ane Kilango mambo ya ndani, Mwakyembe mali asili na utalii, Ole telele ulinzi, Ole sendeka miundombinu, Mwandosya nishati na madini, Lucas Selelii Kilimo na chakula

James Lembeli kuwa waziri wa Mali Asili na Utalii kwakua ndio taaluma aliyoisomea alishawahi pia kufanya kazi Tanzania National Park kwa muda mrefu ataimudu hiyo sekta!:smile-big:
 
Masha akipewa uwaziri nitashangaa sana, Magufuli akiachwa uwaziri nitashangaa sana. Mwakyembe asipopewa uwaziri pia nitashangaa sana. Haya yatajumuisha kuonyesha nini vipaumbele vya serikali ya ccm
 
Ismail Aden Rage michezo
Siraju Kaboyonga(JK amteue ) kisha ampe Fedha ucumi na mipango
Tyson Kilimo
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom