Nani aijenge na kuipigania Tanganyika kama siyo Watanganyika!?

hivi hata isue ya Baa nayo ni ya Wakristo?
Mtoa mada anaposema wakristo wanaonewa na anaposema kuna baa mbili zilichomwa anamaanisha nini?
Kuchomwa kwa baa kunahusianaje na kuonewa kwa wakristo?
 
Ni kweli kuna ubaguzi sana Zenji, mwaka 2004 nilikuwa nafanya biashara ya nafaka kupeleka Znb nilikuwa napitia Pangani naenda kuvusha nafaka kwa jahazi kutoka Mkwaja hadi Mkokotoni. Mara zote nilipofika kule masheha walinisumbua sana kwa kuwa tu ni Mbara lakini mwenyeji wangu Mzenji tuliyekuwa tunafanya biashara ya aina moja alikuwa free sana. Ubaguzi ni mkubwa sana. Huwezi kupanga chumba ukiwa Mbara hata kama umepata kibali cha Sheha
 
Kama mnahisi mnabaguliwa kwanini hamurudi nchini kwenu Tanganyika mnang'ang'ania huko nini?

what a mental slavery. Tatizo kubwa la wazanzibari ni mentality slavery iliyo vichwani mwao HM Hafif. Na si ajabu muungano ukivunjika wakaenda bahrain kumwangukia sultani mmoja aje awatawale.
 
:smash: mmmh mbona hapa bara wanapeta tu na hakuna wa kuwabagua.... hizi ni tabia za kishenzi kabisa.sasa kama we umefunga unamlazimishaje mwenzako afunge.... hivi mtu wa hivyo anafunga au anashinda njaa. kaka yangu aliishi huko miezi kama mitatu tu lakini huo upuuzi wa kubaguliwa na kuingiliwa uhuru wa kuabudu anachokitaka ulimfanya aache kazi. na kwa muda wote huo hakupata nyumba kisa tu alikua anatoka bara na si mwislam.
 
Pole sana kwa yaliyowafika. Ila tunahitaji habari za upande wa pili pia ili kujiridhisha, otherwise the information is bias. kwani inawezakana akawa ni mwanachadema tu kwa sababu zenji hawauziki basi ameanza kuwafitinisha waTZ.
Hata mimi natamani muungano ufe. thank you.
 
Jamani mimi Tanganyika ninalia na kuhuzunika kwanini watanganyika wangu hawanipendi? na wananichukia sana hawataki hata kuitwa kwa jina langu hawajitambulishi kwa jina langu hawataki hata kunisikia,nikiangalia mwenzangu kenya jinsi anavopendwa na wanawe ninaona choyo.Lakini mimi sinabahati ya kupendwa na wanangu wamejibatiza jinaq ati wanaitwa watanzania ni kwanini jamani hamnitaki mmnibadilihajina?nawalaani woote wanaonita TANZANIA
 
Hatuna uhakika sana na jina lako Tanganyika.
Historia haituambii umetoka wapi Tanganyika.
Tulikufahamu kupitia mkoloni Tanganyika.
Ila sasa tumezaliwa upya Tanganyika.
Tumepata jina zuri na tunalolifamu T'nyika.
Tanganyika hutupendi na sasa watulaani!
Kama kweli watupenda ungetuombea baraka.
Nina mengi Tanganyika, ila ngoja nikae na Tanzania.
Tujadili haya yanayotusibu kwa sasa.
 
Pole Tanganyika sie wengine ni wajukuu tumezaliwa tukakuta TANZANIA waliokufanya uwe TANZANIA walishatangulia mbele ya haki, waasisi wa Tanzania walikupenda zaidi ya sisi ndio maana wakapenda kukupa jina jipya TANZANIA, ulimwengu mzima unakujua kwa jina la TANZANIA ila nchi chake walizopata kukutawala ndio wanakumbukumbu zako kuwa babu yetu TANGANYIKA ulipata kuwepo.Mimi mzaliwa Miaka ya 1970s ukiniambia Tanganyika sipati Picha pls understand it from the bottom of my heart,

I hope unajua mapenzi ya nchi, nimezaliwa nikakuta jina Tanzania mother Tongue [Kiswahili] ikanifundisha kuimba wimbo wa Taifa wa Tanzania kwenye Primary Schools. leo hii kuniambia Tanganyika wadogo zangu wa 1980s na 1990s watakuona kama vile namna gani wewe wa wapi?Si unajua kila zama na vitabu vyake, wadogo zangu hao mimi mwenyewe wananipelekesha kwa spidi zao, Wewe ukiwapa issue ya kuwa wao mama yao ni MTANGANYIKA na hakika pata chimbika.

Jina sio tatizo kwetu sisi generation ya dotcom manake sasa hivi ulimwengu kiganjani,cha msingi maendeleo ya vijana hawa na future yao inatayarishwa vipi.

Tulifundishwa wimbo mmoja wa Patriotism tuliimba hivi "Tanzania Tanzania Nakupenda kwa Moyo wote, nchi yangu Tanzania jina lako ni tamu sana..........."

Asikwambie mtu hakuna memory nzuri kwenye maisha ya mtu kukumbuka the old school, ilikua good time ukisimama kwenye parade [most those days at Primary School, Chipukizi parade and few times at Secondary school] na kamchumba kako kauongo na kweli mnaona ufahari kweli.It was our best memory ya patriotism ya utotoni ukizingatia pia kupitia chipukizi Taifa la Tanzania liliingia vichwani mwa watanzania.

Nikiwa form one nilibahatika kusoma siasa form two civics ikaingia wadogo zangu [Ndonya] wakaingiia kwenye Civics kujua elimu ya urai.

Hivyo ukitaka TANGANYIKA waulize watu 1930-1960 waliohai lakini generation yetu sie wengine tumesoma history,na always history inakufundisha na kukuelimisha mazuri na makosa ya waliokutangulia.Zuri la Nyerere [Intellectual Man] na Karume [Brave Mana] ni kutuachia as a legacy ni Taifa la TANZANIA [No matter lilibuniwa na Mhindi wa Tanzania cha Msingi wazee wale walilikubali kutokana na mahitaji ya zama hizo kwetu ni sawa].

Dokezo langu kwa mama Tanaganyika jinsi madogo zangu generation ya DOTCOM walivyo be shown generation [Bishoo] ukitembeza kura ya maoni wachague jina lipi kati ya TANZANIA na TANGANYIKA, hakika Mama Tanganyika Itakua imekula kwake. Na TANZANIA hataibuka kidedea, manake wadogo zangu hawa ambao kwa mapenzi ya mungu mimi na wao na kaka zangu wa miaka ya late 60s ndio tunaitaji kubuild future yetu na kuanza kutayarisha vision za kwenda mbele na madogo ambao wako juu na craze na vitu kibao, kiasi kuwa madingi aka wasure[BABA] awawaelewi wamebaki kutuuliza kila siku hawa wadogo zenu vipi? Hawana kosa ndio ulimwengu wao, kutana na madogo hao ziwe [International, Medium or Kayumba [Za Kata] wote ukiwaambia waitamke hiyo Tanzania madoiodo yao si kidogo Tanziiinia [Tamka nilivyoiandika].

Wape mtihani kuwazoeza wakutamkie TANGANYIKA watakuona uko kushoto kweli yaani wakimaaanisha umepitwa na wakati nawe sio wa zama zao na hivyo unajipya wapishe. Hivyo basi Mama Tanganyika Kwa kuwa Maisha ni Mbio za Vijiti japo baadhi ya viongozi wetu awaamini hilo mpaka ukweli unapokuja kudhihili vijana [Dotcom Generation] ndio warithi wa nchi na vyote vilivyomo nao siku zikifika wawakabidhi wengine vivyo hivyo mpaka pale muumba atakaposema basi.

Tumerithi Tanzania, kwa mtu yoyote mwelewa ulithi [Treasure] uwa ni kitu muhimu cha kutunzwa hata kama hakina thamani, therefore kwangu mimi nitaendelea kukutambua kama nilivyokutambua kupitia Historia kuwa kulikua na Mama Tanganyika kwa jina lake Tanzania ilipata uhuru.

PUMZIKA KWA AMANI WE CHERISH YOU.
 
nimezungumza na waziri mmoja znz hawajui hata mswada wa katiba unasemaje. nikamuuliza kwanini anasema hawana haja nao kwani zanzibar yao wanayo. ameniumiza aliposema hakuna mapato ya znz yanayoenda bara hivyo hata hela mnazowalipa wabunge wa znz na mawaziri wao za kwetu. ndio maana wanapenda muungano waendelee kutunyonya. muungano wa unyonyaji wa nini? watanganyika tuhoji. kumbe akina rashid wanapigania maslahi wale.
 
Hawana shida yani,afu wanaleta wabunge kibao bara sijui wa kazi gani
 
mkuu niaibu wazanzibar walijadili KATIBA yao peke yao, halafu watanganyika yetu hatuna but ya litanzania tunajadili woote! NATAMANI KUJADILI KATIBA YA TANGANYIKA YANGU!
 
bado kuna wasaliti. wabara wenzetu. wanatuhujuma wabara wenzao kwa kushirikiana na mamwinyi.

mimi inaniuma sana kuona kula kitu kinaendeshwa ka rimoti kontroo ya mamwinyi wa pwani, na watanganyika wenzetu baadhi kama kina ngeleja wamesahau kuwa madini yetu kule tanganyika yanavunwa na kupelekwa ughaibunu kupitia viwanja vya ndege na bandari ya pwani. tunasahau kuwa ndugu zetu wanakula ugali wa kiporo kwa mizubho kule nhobhola, lakini mamwinyi wa pwani wanakula ubwabwa kwa nyama ya ng'ombe vinavyotoka kwenye mashamba yetu kule tanganyika.

huu ni mzaha sana kwamba ata samuweli sitta anayejisifu ni mtu makini anashindwa kwenda kuendesha mchakato wa muswada wa katiba kwao tabora, alakini anakwenda zenji kwa mamwinyi. huu ni utumwa sana wa kimwili na kiroho ambao lazima mimi 'nabii' kutoka tangayika ninapaswa kuupinga kwa nguvu zote.

watu wa bara tunajidhalilisha. tunawacha ndugu zetu vijijini wanalima mahindi na karanga na maharage yanayotumika kulisha mamwinyi wa pwani ya tanzania mpaka comorro lakini inapokuja ishu miuhimu kama katiba, watu wa bara tunatengwa bila huruma. friji za mamwinyi wa kariakoo, kisutu mpaka zenji zimejaa samaki sato na sangara, lakini watu wa mwanza wametengwa kuijadili katiba. hii ni dharau. maana yake sisi hatuna umuhimu sivyo?

wabara mlioko serekelini ya mamwinyi acheni usaliti. lazima tuungane pamoja, vinginevyo tutajikuta tunasilimishwa wote.
 
mods inabidi mtafakari kwanza kabla ya kuondoa hii post. tulipojua mwenyekiti wa chama cha mamwinyi kaja mbeya tukajua na sisi tumekumbukwa ishu ya katiba, kumbe kaja kugawa kadi kwa kitambara.

kama hii si dharau ni nini?

na watanganyika tunamshangilia badala ya kumpiga mawe!!
 
eti mtu wa bara akitaka kushiriki public hearing kituo ni dodoma; na akitaka kwenda ajigharimie kila kitu.

lakini mamwinyi wameletewa vituo vya kujadili mitaani kwao. mfano kutoka malindi, mjimkongwe, forodhabi, mlandege, darajani au mkunazini mpaka hoteli ya bwawani hauhitaji hata vespa. ila kutoka mwanza, kigoma, shinyanga, musoma, moshi, arusha, rukwa, mbozi, kuja dodoma je?

wanatuona sisi wajinga sana eti?
 
Hivi kwa nini sisi watanganyika ndio tunaogopa zaidi muungano wa Zanziba na Tanganyika kuvunjika tofuati na wa Zanzibar ambao ni kidogo?

Wengi wa Wanzibar wanataka muungano uvunjike lkn watz bara wao hawapendi kusikia kauli hiyo.

Why?
 
Mkuu siyo kwamba watanganyika tunaogopa muungano kuvunjika. Sijajua imekuwaje ukafikia kusema kuwa tunaogopa. Sikupingi ila unapaswa kutupa data zaidi ili tudrive conclusion kutoka kwenye right and true premises!
 
Ungejua watanganyika makini tunauona Muungano huu kama kiini macho, usingeandika hayo. kwa ufupi tunashangaa kuendelea kuwaona wabunge wa zanzibar (ambao uwakilishi wao unashabihiana na madiwani wa Tanganyika kwa idadi ya watu wakiendelea kuja Dodoma na malalamishi Lundo, kama mnaipenda sana zanzibar huru kwa nini msitusaidie kuzuia hao walowezi wa kizanzibari waache kuja Ddodoma?
 
Muungano huu ni kiini macho tu,kwanza katiba ya zanzibar haitambui muungani bali inatambua shirikisho.huu ni wakati muafaka wakuvunja hiki kiini macho
 
Back
Top Bottom