Nani afumbue fumbo hili?

Shukuru

JF-Expert Member
Sep 3, 2007
748
15
Mtu mmoja alikuwa ndani ya nyumba yake. Ghafla wakaja wageni kadhaa. Katika wageni hao kulikuwa na wababa wawili, watoto wawili, babu mmoja na mjukuu mmoja. Ikiwa jamaa (mwenyeji) anataka kukaa nje na wageni wake wote, Je atatoka na viti vingapi?

Welcome guys!!!
 
Vitano mkuu :D

Tuanzie hapa mkuu
mjukuu wa huyu babu, baba ni mtoto wa huyu babu.
Hivyo baba hapa ni wawili, upo?
Mtoto wa huyu babu ana mtoto ambaye ni mjukuu wa huyu babu.
Babu(baba), baba (mtoto wa babu) na mtoto (mjukuu)
Hapo imekaaje? viti vitatu ama?
 
:D baba wawili ni baba wa mapacha wawili; babu na mjukuu. si ni watano hao?:D
 
Mtu mmoja alikuwa ndani ya nyumba yake. Ghafla wakaja wageni kadhaa. Katika wageni hao kulikuwa na wababa wawili, watoto wawili, babu mmoja na mjukuu mmoja. Ikiwa jamaa (mwenyeji) anataka kukaa nje na wageni wake wote, Je atatoka na viti vingapi?

Welcome guys!!!

VITATU!!

BABA WAWILI-Babu na Baba ake mtoto.

WATOTO WAWILI-Mtoto na Baba ake (mtoto wa Babu)

MJUKUU-Mtoto mmoja(mjukuu kwa Babu).

Apo Vipi Shukuru?
 
wote mmekosea teh teh teh ila kosa lenyewe ni dogo sana..... yaaani kiduchu.

si unajua mambo ya kwenda na moja kichwani? ndio yanayotumika hapa....

one more post.. tunatoa jibu
 
Mtu mmoja alikuwa ndani ya nyumba yake. Ghafla wakaja wageni kadhaa. Katika wageni hao kulikuwa na wababa wawili, watoto wawili, babu mmoja na mjukuu mmoja. Ikiwa jamaa (mwenyeji) anataka kukaa nje na wageni wake wote, Je atatoka na viti vingapi?

Welcome guys!!!

Labda swali halijakamilika, hivyo jibu laweza kuwa namba kati ya 3 na 6!
Kama hawa ni watu wa jamaa moja (kwa maana ya babu, baba na mjukuu) basi 3 ni jibu sahihi...lakini yawezekana ni wa ambao hawana uhusiano wa aina yoyote, basi 6 ni jibu sahihi.
 
Mimi nakurupuka na kusema viti saba.
Wababa wawili =viti viwili
Babu mmoja = Kiti kimoja
Watoto wawili = Viti viwili
Mjukuu mmoja= Kiti kimoja
Mwenyeji wao = Kiti kimoja
Jumla viti= SABA
 
Mtu mmoja alikuwa ndani ya nyumba yake. Ghafla wakaja wageni kadhaa. Katika wageni hao kulikuwa na wababa wawili, watoto wawili, babu mmoja na mjukuu mmoja. Ikiwa jamaa (mwenyeji) anataka kukaa nje na wageni wake wote, Je atatoka na viti vingapi?

Welcome guys!!!

Kwani lazima atoke na viti? Si achukue jamvi au mkeka wakae wote?
 
Mimi nakurupuka na kusema viti saba.
Wababa wawili =viti viwili
Babu mmoja = Kiti kimoja
Watoto wawili = Viti viwili
Mjukuu mmoja= Kiti kimoja
Mwenyeji wao = Kiti kimoja
Jumla viti= SABA

Sasa bubu huko ulikofika siko... yaani viti sita kawaka we unasema saba? au ndio mahesabu ya mlinganyo? ila nimeona kosa ambalo wenzako hawakuligundua.. naimani jibu litapatikana muda si mrefu..
 
Kwani lazima atoke na viti? Si achukue jamvi au mkeka wakae wote?

Kashija hapo umenimaliza!
Si lazima wakae kwenye viti hata jamvini panatosha.Au kama hawana maongezi marefu basi wasikae kabisa!
 
Swali lina majibu kadhaa, ili swali kuwa na jibu moja inabidi swali lieleze kama linataka namba ndogo kabisa ya viti inayowezekana au namba kubwa kabisa ya viti inayowezekana.

wababa wawili, watoto wawili, babu mmoja na mjukuu mmoja

Namba ndogo kabisa ya viti ni 4, babu, baba, mtoto wa nasaba moja na mwenyeji.

Namba kubwa kabisa ni 7, baba wawili tofauti, watoto wawili tofauti, babu mmoja tofauti, mjukuu mmoja tofauti na mwenyeji.
 
Back
Top Bottom