Namwachia nyumba mama mkwe

Kwa haraka na kutumia maelezo yako..huyu mama ana mapepo yanamsumbua... na kijana wake amekosa sifa za kuitwa Baba wa nyumba..hivyo usimtegemee kama ataweza kutatua hizo issues...

Kikubwa ujue wewe ndiye mwenye mji..inabidi umuheshimu mama lakini siyo kwa nidhamu ya woga..Kupeana ukweli, kwa lugha ya heshima ni njia sahihi..

Lakini kabla ya yote lazima umwonyeshe mama kuwa hata wewe unao wazazi..kama wazazi wako wako hai waite waje (kwa gharama yeyote) na itakuwa vizuri ukaongea yote "black and white" mbele ya wazazi wako na huyo mama..bila kuogopa what is next... Najua wazazi wako hawatavumilia lugha mbaya kama huyo mama ataanza..na hivyo itakusidia wewe kukaa kimya na remote control kikao..

All in all, lazima ufanye kitu ASAP... binafsi sikushauri kukimbia nyumba kwa sababu ya mtu mmoja mwenye mapepo yanayomsumbua..Wewe hapo ni kwako na mama ni mgeni..Apewe heshima zake lakini sio kwa woga.. kama vidonge apewe..anywe, apone mapepo!
Ni shauri zuri Mkuu. Kwa mama mkwe namna hii dawa si kuondoka, kwani mke akiondoka atakuwa amemrahisishia kazi ya kutimiza malengo yake. Hata mumewe akirudi, mama mkwe atabakia hapo na mume hana kauli kwa mama yake. La kufanya hapo ni kumfanyia maisha ayaone magumu, awe yeye wa kuondoka. Wala si kwa njia ya kumtukana bali kusimama naye kimo kimoja, akimwaga mboga anamwaga ugali.
 
Ndugu yangu mwambie huyo mama straight wala usimshirikishe mumeo, mwambie mama naomba urudi kwako, kukaa kwako hapa kunanikosesha amani, je unahitaji msaada gani, kama wa pesa uwe unampatia kila mwezi. yanini kuumia wakati uko kwenye nyumba yako, mwambie straight nataka niishi na familia yangu tu. full stop akichukia na kuondoka ndio vizuri zaidi atakoma kuja kuja kwako, akikataa mwambie nakuachia nyumba kaa uishi na mwanao, bila kuwa kauzu atakusumbua sana, I have been there.
 
FL1...uko sahihi kabisa hii pia inaweza kuwa njia sahihi, nyie wawili tu, sababu kama kukiwa na mtu wa tatu, kwa aiubu ataleta ubishi na hatakubali kukusikiliza. Mtafutie siku , wawili tu. Unaweza kumfuata chumbani ukafunga mlango na kumwambia akueleze tatizo ni nini, Openly mwambie umechoka na mambo yake, anakukera, na kuwa hapo ni kwako hautaondoka. Jamaa mekuzimia na yeye hana jinsi ya kuibadilisha hiyo.....in short mpe Mkwara wa nguvu lakini uliojaa facts tupu!

Hapa ni kudanganyana tu. Wewe unataka kumharibia zaidi badala ya kutibu na sidhani kama FL alimaanisha hiki unachokisema wewe. Unapokaa kujadili suala tete kama hili hutakiwi kwenda na "the so called" MKWARA WA NGUVU kwani haujui yeye atakuja na MKWARA wa aina gani. Busara na kiasi lazima vitawale mazungumzo ya aina hii ili muweze ama kufikia muafaka au kukubali kutofautiana bila kugombana.
 
dunia hii c ya kumwogopa mtu ye aliolewaga ndo akamzaa mumeo sasa muulize ye wakwe zake walimsumbua hawa ndo jamii ya wakwe ambao wanafkuzwagwa na watoto wao. Mwambie mumeo akuitie mamake umpe fakt tupu halaf uwe tayari kwa lolote au mpe makavu laiv ye c mwanamke kama ww bana'
 
Mimi ni mwanafunzi so siijui ndoa sasa ushauri wangu usijaribu kukimbia nyumba yako hata siku 1, piga mkwara mzito, then mtupie vilago vyake nje heri lawama kuliko fedhea.

ucjaribu hilo kabisa......uiache nyumba kisa mama mkwe? masihara hayo.....labda uniambie na mume umemchoka pia, lakini mama yake tu ndo akufanye uiache nyumba?
 
Pole sana Esperance; kwa kweli hata mimi sikushauri uiache nyumba yako kisa mama mkwe! Kwa jinsi ambavyo inavyosimulia vituko vyake, basi naona kwa kweli huyo mama ana pepo, sio kawaida! Kwa hapo kwa kweli, unahitaji maombi, ili Mungu aingilie kati; either abadilike au aondoke! Hakuna lisilowezekana kwa Mungu; yote yawezekana kwake aaminiye. POLE na Mungu akusaidie.
 
Pole sana ndoa ni ya mke na mume tuu na si wazazi.wao wananafasi yao kama wazazi,washauri na si kuingilia lolote unless imeonekana kuna tatizo kubwa kati yenu.mimi nimeoa na yote tunayoyafanya tulishakubaliana na mke wangu kabla hatujaoana.mf hakuna ndugu yeyote anayeweza kuja kukaa kwetu bila sababu,kama ni kazi atasaidiwa kama tunaouwezo wa kumsaidia hivyo ni kwa specific time.kama ni kusomesha si lazima ukae na ndugu ndio umsomeshe unaweza kumsaidia hukohuko aliko shule zipo popote kama ni lazima aje kwangu basi atakaa bording,mie sitaki migogoro na yeyote.kama ni wazazi wana kwao,so kwangu ni kuja kusalimia tu na wanarudi kwao kama wanaumwa wanaweza kutibiwa kwa muda maalum na kuondoka,misada mingine itatumwa hukohuko.huo ndio msimamo wetu na wote tumeafiki na maisha ni mazuri ya upendo,kama kuna ndugu yeyote anakuja tunashirikishana kabla na tunajipanga how to handle the ishu.maisha ni mipango na si kuishi kwa kubahatisha.nampenda sana sana mama yangu lakini kamwe yeye si mke wangu hivyo hana mamlaka yeyote juu ya ndoa yangu isipokuwa ushauri wake wa hekima.kwa ufupi mama mkwe hana kosa ila tatizo ni la huyo mumeo bado hajakomaa na hajui nini maana ya kuoa hana msimamo haiwezekani akamruhusu mama yake aishi hapo bila sababu,kama ameng'ang'ania kukaa hapo si mhame mkapange kwingine mumwachie nyumba.tumieni hekima hatawashinda.hata wewe kama unakipato kidogo tafuta nyumba chukua watoto wako mkaishi.....suala la kurudi kwa wazazi ni mambo ya kizamani na pia inategemea mazingira je kama wapo bukoba na wewe unakaa dsm na unakazi yako au shughuli yeyote ya kibiashara itakuwaje? Pia mazingira ya nyumbani yanaruhusu wewe kuishi hapo tena na familia?kama ulishaoondoka nyumbani kwenu maana yake we ni mtu mzima unayeweza kuishi maisha yako pia,take your own action kama unakipato maana mumeo hawezi kuwa na jipya la kukushauri maadam tatizo linaelweka no body can blame you.
 
Pole sana!wamama kama hawa ni hatar sana wamejaa fikra za kimagamba.Never loose hope fight for your marriage,utashinda!
 
Pole sana dia ila kwa maelezo yako naona kama pia huyo mama mkweo anakufanyia makusudi akijua hakuna wa kumfanya chochote maana ukoo wote ameucontrol. Kutokana na hali yako haina haja ya malumbano wala ugomvi, jifikirie kwanza wewe mwenyewe kwa sasa na mtoto wako aliyetumboni. Jitambue tu kuwa uko kwenye uwanja wa mapambano.......one mistake.......double goals. Nakuombea Mungu akusaidie kuwa na maamuzi sahihi yatakayoleta a permanent soln.

Kila heri.
 
Kwenu? No Sikushauri uende kwenu, Hapo ndiyo kwako, Mama mkwe yupo hapo kwa muda tu, Tatizo ninaliona hapo ni kwamba Familia Hiyo siyo Stable, kama kuna Baba Mkwe, Kaka na wote hao hawawezi kumshauri huyo mama kuondoka hilo ni Tatizo, Komaa hapo hapo tu, Kama mama mkwe amekimbia nyumba yake na kuenda kujificha kwa watoto ni yeye, Wee komaa tu, Ila Ongea naye umwambie ukweli kuwa wewe ni mwanamke kama yeye na mume anaye kama wewe ulivyoolewa na na mwanaye anayokufanyia kama akifanyiwa yeye atafurahi? Umwambie kuwa wewe umzuii kukaa kwa mwanae, lakini ajue kuwa wewe ndiye mkewe, Na hilo hawezi kulibadili.
 
umechelewa sana kumwambia ukweli wake umefuga kidonda karb kinakua donda ndugu vunja ukimya mwambie aende zake nymbani kwake ala!
 
Mi naona kama uhamie kule kwa baba mkwe au vipi, ongea na mumeo uende kule limama likija huko ndio mnakaa kikao sasa cha ukweli na uwazi bila woga
 
Kwanza kabisa wazazi wako huwa wanalipokeaje hili tatizo lako unapowapelekea naomba utufahamishe hilo kwanza jibu la hapo pia nalo ni la muhimu.Pia wote mlochangia msiwe mahakimu wa kutoa hukumu kwa kusikiliza utetezi wa upande mmoja
 
Back
Top Bottom