Namuunga mkono Anna Kilango Malechela kwa nguvu zote

Kweli mkuu kwa Sophia na Kilango tungepata/tutapata burudani ya kutosha kwa sababub kila mmoja ana dark side zake na wote hawaogopi kuumbuana; itakuwa ni sinema tosha acha tukae mkao wa kula!!

Mkuu Kunta Kinte hilo ni bonge la movie.
 
Last edited by a moderator:
nawshauri UWT wawapige chini hawa wote wawili hawafai mtazidi kukiua chama chenu
 
Mkuu Molemo kumbe huwa unakuwa hata upande huu wa pili ma una watu unaowaunga mkono huku? Safi sana.

Yaa ni kweli mkuu Kimbunga.Nilipendezwa na sera ya Sofia Simba ya wanawake wa ccm kuwanyima unyumba waume zao wanaoshabikia CDM.
 
Last edited by a moderator:
Hii theme ni kiboko.
Ubaya ni kwamba kuna wale munaokitakia mema hicho kitu CCM. Uzuri kwetu ni kuona kikiweka pua chini. kwani jumuiya hii ina maana tena? NI kikundi cha taarabu ya kanga moja! Kanga tepwe tepwe, ndembwe ndembwe!

Mipasho, ufuska, na yote. Kwani CCM wanawatumiaje hao wana UWT?
 
kwani hakuna mtu mwingine anaweza kugombea zaidi ya Anna na simba?....manaake tangu nakua namckia sophia
 
Mama Simba ni light weight ambaye uwezo wake wa kujenga hoja na kuongoza vinafanana. Vyote ni vya kiwango cha chini na unajiuliza kama kweli alikuwa ni mhitimu wa kweli wa shahada ya sheria ambayo hufundisha watu kujenga hoja.

Hata wale waliomuunga mkono kushinda kiti hiki wameshakiri kwamba huyu mama si mtu wa tija katika mapambano ya uongozi na kujenge makakati madhubuti wakati wa ushindani.

Anachojua yeye ni kushangilia na kusuta watu katika vikao vya ndani lakini katika uongozi wake hakuna wakati aliotoka nje na kuongoza mapambano ya hoja dhidi ya mahasimu wa kundi lake au wa chama chake. Na mfano hai ni leo ambapo ameshindwa kupambana na wimbi la Chadema na hata kauli yake haijawahi kusikika.

Wanawake huu ndiyo wakati wenu wa kuendesha balanced score card na kupima utendaji wa mama huyu.
 
Mama Sophia Simba ni mtu Makini na ndiyo maana JK amempa Uwaziri akamtosa Anne Kilango Malecela. Mkuu Mbopo M4C ni kama Mvua ikiamua inanyesha na huwezi izuia
 
Last edited by a moderator:
Kufuatia Mh. Sophia Simba kukalia hicho kiti awamu iliyopita na kuamua kutetea kiti chake awamu hii huku wakichuana vikali na Mh. Anna Kilango Malechela mimi msimamo wangu ni kumuunga mkono Mh Anna kwa hali na mali kwasababu zifuatazo:-

1.UNDUGU NA KUJUANA KUMEZIDI

Jumuiya hii imekuwa ikipoteza mantiki kabisa na kuwa jumuiya ya wake na watoto wa vigogo na mijimama ya mjini yenye majina makubwa ilhali uwezo wa mtu kuongoza na kukiletea chama maendeleo hauangaliwi kabisa wala kuzingatiwa. Kama huna jina mujini na pesa haiongei fungua njia kitoto chaanza tambaa. Na hili limedhihirika sana kipindi hiki kinachoisha cha Mh. Simba, ni dhahiri tukiendela kumkabidhi usukani kitakuwa chama cha watu fulani flani na mijimama ya mjini. Bora tubadili upepo tumuweke huyo mpare tuone hali itakuwaje ila hali ya Mh. Simba haifai!....

Wewe ni mpiga kura? au unataka kuleta mambo ya Simba na Yanga hapa.
 
Kilango asubiri uchunguzi dhid yake juu ya kuomba rushwa kwa katibu mkuu nishati na madini,
maza fisadi sana huyo!
 
Nyie ndiyo wakwanza kumwaga pumba kuhusu JF lakini inapofika mnataka kugombe sehemu ya kupima upepo ni JF. Mshindwe na Mlegee kamwambie JF haijawai kubadilika.:nerd:
 
Waache hawa GOLD diggers wachafuane na in the process wakichafue chama cha magamba; kwani katika ugonvi huu lazima mahasimu wanaume wataingia na hapo sinema itakuwa burudani ya kutosha!!
 
Kilango asubiri uchunguzi dhid yake juu ya kuomba rushwa kwa katibu mkuu nishati na madini,
maza fisadi sana huyo!

Huyu ni fisadi babu kubwa kwani amechukua rushwa hata kwa ile kampuni ya kichina iliyokuwa inawania tenda ya kujenga magati bandarini!! Hana msimamao kwani siku hizi ameanza kujipendekeza kwa EL kama mwenzie Beatrice Shellukindo!!
 
mtoa mada hujui hata unachoongea sijui tayari bia ilikua kichwani. umesema humuungi mkono simba kwa sababu hiyo jumuiya imejaa wake na watoto wa vigogo ndio maana unamuunga mkono kilango..je nikuulize kilango yeye sio mke wa kigogo? wote ni wake za vigogo na hii kitu ya kuridhishana au kiongozi mwanamke lazima awe mke au alishatembea na kigogo flani tumeshaichoka. Tumuunge mkono mwanamama ambae hana connection na kigogo yoyote serikalini au kwenye chama then hapo tutapata mtu ambaye atakua katikati anasikiliza kila mtu
 
...

Jumuiya hii imekuwa ikipoteza mantiki kabisa na kuwa jumuiya ya wake na watoto wa vigogo na mijimama ya mjini yenye majina makubwa ilhali uwezo wa mtu kuongoza na kukiletea chama maendeleo hauangaliwi kabisa wala kuzingatiwa. Kama huna jina mujini na pesa haiongei fungua njia kitoto chaanza tambaa. Na hili limedhihirika sana kipindi hiki kinachoisha cha Mh. Simba, ni dhahiri tukiendela kumkabidhi usukani kitakuwa chama cha watu fulani flani na mijimama ya mjini. Bora tubadili upepo tumuweke huyo mpare tuone hali itakuwaje ila hali ya Mh. Simba haifaiiiiiiiiiiiiiiiiii!

Ebo, yaani unadhani hali hiyo inasababishwa na Mh. Simba? Watafute kwanza wenye kauli ya mwisho kuhusu vigezo vya kumpa mtu nafasi ya uongozi ndani ya UWT ndio uelewe undani wa jumuia yenyewe. Au muulize madame Rita Mlaki mpasho aliopewa alipojaribu "kujipendekeza". Jumuia imepoteza mwelekeo? Unachokiona kama kupoteza mwelekeo ndio mwelekeo wenyewe. Wakuu wa chama hawataki UWT "serious" hata siku moja. Wanataka watu wa kucheka nao ndani ya jumuia. Bila shaka hata huyo "mpare" naye ana gia yake ya kuchekeshwa. Usiumie kichwa ndugu yangu, kwa kifupi ni kuwa UWT itakuwa imara pale CCM itakapoacha maskhara, si vinginevyo.
 
nyie ndiyo wakwanza kumwaga pumba kuhusu jf lakini inapofika mnataka kugombe sehemu ya kupima upepo ni jf. Mshindwe na mlegee kamwambie jf haijawai kubadilika.:nerd:

umenisikia nikimwaga pumba au unapenda kuropokaaaaaaaaaaaa bila ushahidi!
 
Back
Top Bottom