MwanajamiiOne
Platinum Member
- Jul 24, 2008
- 10,470
- 6,562
wakuu nina tatizo nimekaa nalo muda mrefu sana moyoni mwangu'
tumezaliwa wanne kwenye familia yetu' sisi ni wachaga na tumekulia na kulelewa na kusoma uchagani'
lakini kwa kadri tulivyokuwa tunaendelea na maisha niligundua mama yangu mzazi anamthamini mtoto mwenye mali peke yake'
baada ya kugundua hilo niliamua kunyamaza kimya japo nilikuwa na uchungu moyoni'
lakini hicho kitendo kilijidhiirisha hata kwa watu wanaotufahamu kijijini kwetu na ilileta matatizo makubwa'
kwa kweli kutoka moyoni mwangu nimejikuta simpendi kabisa mama yangu lakini bado namweshimu kama mzazi wangu'
nikienda nyumbani mara moja kwa mwaka sijisikii kabisa hata kukaa naye hata kwa dakika 10 inakuwa ngumu sana,
niliumia sana kwa kuwa mimi ndiye maskini kabisa na ndiye ambaye sipewi heshima kabisa
naombeni kujua kama kuna mtu mwenye matatizo kama haya na naombeni kujua kama kunaweza kutokea matatizo yoyote katika maisha yangu kwa hilo
nawakilisha.
episodes pole sana kwa kweli ni maisha magumu haya ila mshukuru MUNGU kwa yote. ... chukulia ni kitu cha kawaida .(Si nasikia wachaga wanahusudu sana wenye pesa hadi wanawaamkia..shikamoo mwanangu!!- kama ni kweli ). Hii post yako imenigusa sana but amini unapoweka 'grudges' juu ya mama yako Moyoni mwako ndivyo unavyozizuia baraka za Mwenyezi Mungu katika maisha yako. Tumeambiwa tuwaheshimu wazazi wetu ili siku zetu zipate kuwa nyingi humu duniani lakini pia ziwe za mafanikio. Huwezisema unamheshimu wakati unamchukia!! hebu kaa na utafakari hiyo heshima yako ikoje----- heshima ni zaidi ya shikamoo mama; aksante mama e.t.c. Heshima ni ule m-package mzima wa shukrani, thamani na appreciation- Sasa kama unasema unamheshimu lakini humpendi- kutokumpenda kunawezakukuzuia kumthamini na hata kuappreciate anayokufanyia au malezi alokupa.
Funguka..........kama unaweza jenga ukaribu naye kisha mweleze..Mama najua sina uwezo kiasi cha kukuriddhisha, but mama jinsi unavyotutreat mimi na mdpgp wangu nakwazika..............mweleze unavyojisikia pengine ye anafikiri hujagundua au hujui. Mweleze kuwa unajua, wamama tuna huruma na huumia sana pale tunapowakosea wenetu (hatunaga ile pride ya mimi ni mzazi wako -so sistahili kukuomba msamaha) unawezashangaa akawa karibu nawe zaidi.
Funguka moyo ili upate kuachia baraka za MUNGU zimiminike kwenye maisha yako na kuyafungua madirisha ya baraka na mafanikio nyumbani kwako. Kila la khheri