Namuheshimu mama yangu lakini simpendi

wakuu nina tatizo nimekaa nalo muda mrefu sana moyoni mwangu'
tumezaliwa wanne kwenye familia yetu'
sisi ni wachaga na tumekulia na kulelewa na kusoma uchagani'
lakini kwa kadri tulivyokuwa tunaendelea na maisha niligundua mama yangu mzazi anamthamini mtoto mwenye mali peke yake'
baada ya kugundua hilo niliamua kunyamaza kimya japo nilikuwa na uchungu moyoni'
lakini hicho kitendo kilijidhiirisha hata kwa watu wanaotufahamu kijijini kwetu na ilileta matatizo makubwa'
kwa kweli kutoka moyoni mwangu nimejikuta simpendi kabisa mama yangu lakini bado namweshimu kama mzazi wangu'
nikienda nyumbani mara moja kwa mwaka sijisikii kabisa hata kukaa naye hata kwa dakika 10 inakuwa ngumu sana,
niliumia sana kwa kuwa mimi ndiye maskini kabisa na ndiye ambaye sipewi heshima kabisa
naombeni kujua kama kuna mtu mwenye matatizo kama haya na naombeni kujua kama kunaweza kutokea matatizo yoyote katika maisha yangu kwa hilo

nawakilisha.

Hakuna unachoweza kufanya zaidi ya kuapa kuwa wewe hutawafanyia hivyo wanao. Msamehe mama yako...

Huyo mama ni wa hajabu. SIsi mama yetu anampendelea zaidi asiye na uwezo na sisi hatusikii vibaya kwani tunaona ni huruma ya mama kwa mtoto. Yani tulikuwa na kaka yetu mama alikuwa anampendelea sana kwa kuwa alikuwa hana mbele wala nyuma; aliamua kwenda shule kwa sasa ana kazi yake na yuko mbali; ila those days alipokuwa arosto ndio alikuwa kipenzi na ukimsema vibaya kwa mama tegemea kununiwa.

Hiyo sio point nzuri unapoanza kumshauri mtu (usimfanye aone anavo hisi yeye ni sahihi),...
Back to the point,...

Mkuu,pole sana kwanza kwa yaliyo kukuta,..
Lakini mara nyingi ili hata Mungu akubariki inabidi ujifunze kuchukua "msalaba" wa mwenzio!
Hata kama unahisi una mchukia mama yako kwa sababu uliyo eleza,jaribu kujifanya mjinga kidogo,...

Assume kwamba wewe ndio tatizo la yeye kua hivo,yawezekana sababu ulizotoa kwamba
anapenda "wenye mali" ni mtazamo wako tu na sio kweli kwamba anapenda wenye mali,..

kwa mfano,mdogo wangu alikua hapendi sana kusoma,mimi nilikua napenda kusoma sana
na mara nyingi nilifanya vizuri,mdogo wangu alinionea wivu maana siku zote "nilikua mfano kwake kila
mama anapo ongea nae",....

Kwa mfano ungesikia "mbona kaka yako **** anafanya hivi na anafaulu,me sitaki watu wasio jituma
na wazembe kama wewe",......kama huyu dogo asingejituma na kuanza kuniiga katika kusoma,..
na kama "asingeongea na mama kwamba hapendi kila anapo ongea nae anitolee mimi mfano"
basi leo hii huyu dogo angekua ana lalamika kwamba mama hampendi.

Point yangu ni kwamba,kaa chini,hata kama hujisikii kuongea nae jitahidi tu,....ongea na mama yako
kuhusu unavo jisikia juu yake,kua muwazi kabisa na utaondoa hasira zote ulizo nazo juu yake
(kwa kuongea nae tu kwanza),...then sikia atasemaje!

mwambie ukweli,mama nakupenda sana lakini mara nyingi sijisikii kuongea na wewe maana naona
kama hunipendi na unapenda watoto wako wenye mali tu

believe me,ni maneno magumu sana kuyatamka,lakini impact yake ni kubwa sana katika kujenga mahusiano
mapya na ya kudumu na mzazi wako,...

nakumbuka niliwahi kuongea kitu na mama kilicho kua kina nitatiza (kama mdogo wangu alivo ona napendelewa
nami kuna vitu niliona anapendelewa),niliongea nae kwa hasira kweli kiasi kwamba nikawa nalia wakati naongea,...
nilivomaliza nilienda kulala,mama alikaa kimya na kila nilipo msalimia alikaa kimya,.....
baadaye nilikuja kumuomba msamaha kwamba nimekosa kwa kuongea nawe kwa hasira,...this time ilikua
zamu yake kulia na kuniomba msamaha pia,....since then,life has never been the same!!!!!!

Kama ni ngumu sana kuongea na mama yako,basi kaa chini na ndugu yako mmoja unae mwamini,
mwambie kwa uwazi kabisa duku duku lako,then yeye ataongea na mama yako na mtajua chanzo cha tatizo ni nini,

yawezekana kabisa wewe ndio tatizo,ila hutajua kama wewe ni tatizo hadi muongee kwa
kina kujua chanzo cha yote hayo

Option za kuwa muwazi na kuongea ni ngumu sana nakuhakikishia,lakini option
nyingine ya kukaa kimya ni ngumu zaidi maana "una mpa shetani nafasi ya kukudanganya kuhusu nini ufanye
juu ya hali iliyopo
",.....trust me,shetani hata kushawishi kufanya mazuri,....

Matokeo yake ndo tutasikia oooh,kamuua ndugu yake,mdogo wake,mama yake (God forbid in Jesus name)!!!!

Njia pekee ni kuomba,then kaongee nao!
Yawezekana na wao (ndugu zako) na mama yako wana duku duku nyingi sana
kuhusu wewe lakini wanaona kuna namna flani ya ukuta kati yenu,....UVUNJE UKUTA HUO SASA!

All the best

mkuu baba yangu hakuwa tajiri,tuliishi maisha ya kawaida kabisa,lakini waliweza kutulea

kwa kweli jambo la kusema tulazimishe kupata mali mimi nipo kinyume kabisa

naishi maisha ya kawaida nina nyumba,kazi na kausafiri,na nina watoto wangu wazuri sana

jamani nifanye nini mimi ili niheshimike?

What more do you want? Una:
1. Mke
2. Watoto
3. Nyumba
4. Gari
5. Kazi

Mbona una basic necessities in life? Menigine ya upendo na amani ktk familia yako sivihesabu.

Wewe ni kaka mkubwa, claim your right and be who you are. Mafanikio ya wadogo zako yasikutishe. Kuwa dynamic kaka!

Usipoangalia utaidumbukiza familia yako kwenye matatizo kwa mambo madogo eti kisa unahisi mama yako hakuheshimu.

Kaka, respect is earned. Kuwa mtulivu, utakuwa mtu wa ajabu sana ukianza kufikiri humpendi mama yako. Mawazo mabaya sana hao.

mkuu mama yangu anatoka machame

sipendi niongee sana hilo lakini kwa ujumla maisha ya baba na mama yalikuwa ni matatizo makubwa
Episodes, maisha ya ndoa ya baba yako na mama yako hayakuhusu. They solved their problems their way.inawezekana ulikuwa upande wa baba yako kipindi chote hiki na ndio maana unamwona mama yako hafai.

Kuwa makini sana, mama ni mama.

Hiyo sio point nzuri unapoanza kumshauri mtu (usimfanye aone anavo hisi yeye ni sahihi),...

Back to the point,...

Mkuu,pole sana kwanza kwa yaliyo kukuta,..

Lakini mara nyingi ili hata Mungu akubariki inabidi ujifunze kuchukua "msalaba" wa mwenzio!

Hata kama unahisi una mchukia mama yako kwa sababu uliyo eleza,jaribu kujifanya mjinga kidogo,...

Assume kwamba wewe ndio tatizo la yeye kua hivo,yawezekana sababu ulizotoa kwamba

anapenda "wenye mali" ni mtazamo wako tu na sio kweli kwamba anapenda wenye mali,..

kwa mfano,mdogo wangu alikua hapendi sana kusoma,mimi nilikua napenda kusoma sana

na mara nyingi nilifanya vizuri,mdogo wangu alinionea wivu maana siku zote "nilikua mfano kwake kila

mama anapo ongea nae",....

Kwa mfano ungesikia "mbona kaka yako **** anafanya hivi na anafaulu,me sitaki watu wasio jituma

na wazembe kama wewe",......kama huyu dogo asingejituma na kuanza kuniiga katika kusoma,..

na kama "asingeongea na mama kwamba hapendi kila anapo ongea nae anitolee mimi mfano"

basi leo hii huyu dogo angekua ana lalamika kwamba mama hampendi.

Point yangu ni kwamba,kaa chini,hata kama hujisikii kuongea nae jitahidi tu,....ongea na mama yako

kuhusu unavo jisikia juu yake,kua muwazi kabisa na utaondoa hasira zote ulizo nazo juu yake

(kwa kuongea nae tu kwanza),...then sikia atasemaje!

mwambie ukweli,mama nakupenda sana lakini mara nyingi sijisikii kuongea na wewe maana naona

kama hunipendi na unapenda watoto wako wenye mali tu

believe me,ni maneno magumu sana kuyatamka,lakini impact yake ni kubwa sana katika kujenga mahusiano

mapya na ya kudumu na mzazi wako,...

nakumbuka niliwahi kuongea kitu na mama kilicho kua kina nitatiza (kama mdogo wangu alivo ona napendelewa

nami kuna vitu niliona anapendelewa),niliongea nae kwa hasira kweli kiasi kwamba nikawa nalia wakati naongea,...

nilivomaliza nilienda kulala,mama alikaa kimya na kila nilipo msalimia alikaa kimya,.....

baadaye nilikuja kumuomba msamaha kwamba nimekosa kwa kuongea nawe kwa hasira,...this time ilikua

zamu yake kulia na kuniomba msamaha pia,....since then,life has never been the same!!!!!!

Kama ni ngumu sana kuongea na mama yako,basi kaa chini na ndugu yako mmoja unae mwamini,

mwambie kwa uwazi kabisa duku duku lako,then yeye ataongea na mama yako na mtajua chanzo cha tatizo ni nini,

yawezekana kabisa wewe ndio tatizo,ila hutajua kama wewe ni tatizo hadi muongee kwa

kina kujua chanzo cha yote hayo

Option za kuwa muwazi na kuongea ni ngumu sana nakuhakikishia,lakini option

nyingine ya kukaa kimya ni ngumu zaidi maana "una mpa shetani nafasi ya kukudanganya kuhusu nini ufanye

juu ya hali iliyopo",.....trust me,shetani hata kushawishi kufanya mazuri,....

Matokeo yake ndo tutasikia oooh,kamuua ndugu yake,mdogo wake,mama yake (God forbid in Jesus name)!!!!

Njia pekee ni kuomba,then kaongee nao!

Yawezekana na wao (ndugu zako) na mama yako wana duku duku nyingi sana

kuhusu wewe lakini wanaona kuna namna flani ya ukuta kati yenu,....UVUNJE UKUTA HUO SASA!

All the best

UNAJUA MAGONJWA MENGINE YA WAGANGA YANAITAJI KUTATULIWA NA WANGA WENYEWE KWA ULICHOANDIKAHATA WAKUPELEKE MISIKITI KUMI NA MAKANISA 40 UGONJWA WAKO
NI HATARI ANAUTIBU ALIEKUGAWIA PEKE YAKE

umeona sasa
hili ambalo hutaki kulizungumzia
ndio chanzo cha yote hayo.....
I was right....
Wewe machoni mwa mama yako
umem replace baba yako...
Kuna kitu hapo...

Mimi ninachokiona ni kwamba enzi za uhai wa baba yake episode alikuwa ameegemea upande wa baba yake ie hakuwa akifurahishwa na aliyokuwa akitendewa baba yake...............na taratibu akajikuta akijenga chuki na mama yake na kucreate distance kati yao.

Baada ya baba kufariki..........hana tena rafiki katika familia kwani nduguze walikuwa upande wa mama yao.........hivyo anajiona katengwa.
Suluhisho hapa si yeye kupata pesa nyingi au kuongeza utajiri.............ni ushauri nasaha/mazungumzo ya ana kwa ana kati yake yeye na mama yake mzazi kwani mama ni mama na atabaki kuwa mama.

Kila mmoja atakuwa na dukuduku na mwenzake na kwa kuwa hawawezi kukaa zaidi ya dk10 na kuongea..........hakuna muafaka utakaopatikana..........mama anaona anadharauliwa..........mtoto anaona hathaminiwi.......UFA MKUBWA SANA NA WA HATARI!

Ushauri wangu apige moyo konde,akae chini na mama yake na kujaribu kuongelea kwa upendo jinsi mahusiano yao yanavyomkwaza.

Hongera sana kwa kuendelea kumuheshimu mama yako japo unahisi yeye hakuheshimu. Nakushauri ukae naye mzungumze nini hasa unaona unakikosa kwake hiyo itasaidia sana kujua nini kimesababisha hii hali. Inawezekana pia kuwa huwa hueshimu maamuzi yake au unatabia ambazo mama hazmfurahishi. Radhi ya mama ni muhimu sana hivyo kama una wazo la kutojihusisha tena na mama yako unaweza kukutwa na mambo mengi mabaya.

lakini kwa kadri tulivyokuwa tunaendelea na maisha niligundua mama yangu mzazi anamthamini mtoto mwenye mali peke yake'
baada ya kugundua hilo niliamua kunyamaza kimya japo nilikuwa na uchungu moyoni'

nawakilisha.

Mkuu kwahiyo ameweza kukulea vizuri na kwa upendo mpaka umeweza kukua na kupata uwezo wa kuwa na mali (yaani umekuwa mtu mzima)

Mkuu shukuru Mungu na Mama yako kwa kukulea na mpaka umekuwa mtu mzima (dont expect appreciate) na kumbuka umri unavyokwenda na akili zetu zinabadilika msamehe kama amezeeka lakini mpende kwa kukulea mpaka umefikia umri huu

What more do you want? Una:
1. Mke
2. Watoto
3. Nyumba
4. Gari
5. Kazi

Mbona una basic necessities in life? Menigine ya upendo na amani ktk familia yako sivihesabu.

Wewe ni kaka mkubwa, claim your right and be who you are. Mafanikio ya wadogo zako yasikutishe. Kuwa dynamic kaka!

Usipoangalia utaidumbukiza familia yako kwenye matatizo kwa mambo madogo eti kisa unahisi mama yako hakuheshimu.

Kaka, respect is earned. Kuwa mtulivu, utakuwa mtu wa ajabu sana ukianza kufikiri humpendi mama yako. Mawazo mabaya sana hao.

mwanzoni nilihisi labda hana kazi na bado hajajitegemea na hivyo anaonekana mzigo nyumbani. lakini hata mimi nilishtuka sana wakati thread inaendelea kugundua kuwa ana vyote hivyo ulivyoorodhesha na bado anajiita masikini, analialia mbele ya mama yake na (labda) hata mbele ya wadogo zake! sijui Mungu ampe nini tena ili ajiamini na kurejesha tena furaha maishani mwake?

kwa kweli huyu kaka ni wa kumuombea zaidi Mungu ampe amani yake kwa kadiri ya wingi wa rehema zake
Jina la Bwana libarikiwe

Hiyo sio point nzuri unapoanza kumshauri mtu (usimfanye aone anavo hisi yeye ni sahihi),...
Back to the point,...

Mkuu,pole sana kwanza kwa yaliyo kukuta,..
Lakini mara nyingi ili hata Mungu akubariki inabidi ujifunze kuchukua "msalaba" wa mwenzio!
Hata kama unahisi una mchukia mama yako kwa sababu uliyo eleza,jaribu kujifanya mjinga kidogo,...

Assume kwamba wewe ndio tatizo la yeye kua hivo,yawezekana sababu ulizotoa kwamba
anapenda "wenye mali" ni mtazamo wako tu na sio kweli kwamba anapenda wenye mali,..

kwa mfano,mdogo wangu alikua hapendi sana kusoma,mimi nilikua napenda kusoma sana
na mara nyingi nilifanya vizuri,mdogo wangu alinionea wivu maana siku zote "nilikua mfano kwake kila
mama anapo ongea nae",....

Kwa mfano ungesikia "mbona kaka yako **** anafanya hivi na anafaulu,me sitaki watu wasio jituma
na wazembe kama wewe",......kama huyu dogo asingejituma na kuanza kuniiga katika kusoma,..
na kama "asingeongea na mama kwamba hapendi kila anapo ongea nae anitolee mimi mfano"
basi leo hii huyu dogo angekua ana lalamika kwamba mama hampendi.

Point yangu ni kwamba,kaa chini,hata kama hujisikii kuongea nae jitahidi tu,....ongea na mama yako
kuhusu unavo jisikia juu yake,kua muwazi kabisa na utaondoa hasira zote ulizo nazo juu yake
(kwa kuongea nae tu kwanza),...then sikia atasemaje!

mwambie ukweli,mama nakupenda sana lakini mara nyingi sijisikii kuongea na wewe maana naona
kama hunipendi na unapenda watoto wako wenye mali tu

believe me,ni maneno magumu sana kuyatamka,lakini impact yake ni kubwa sana katika kujenga mahusiano
mapya na ya kudumu na mzazi wako,...

nakumbuka niliwahi kuongea kitu na mama kilicho kua kina nitatiza (kama mdogo wangu alivo ona napendelewa
nami kuna vitu niliona anapendelewa),niliongea nae kwa hasira kweli kiasi kwamba nikawa nalia wakati naongea,...
nilivomaliza nilienda kulala,mama alikaa kimya na kila nilipo msalimia alikaa kimya,.....
baadaye nilikuja kumuomba msamaha kwamba nimekosa kwa kuongea nawe kwa hasira,...this time ilikua
zamu yake kulia na kuniomba msamaha pia,....since then,life has never been the same!!!!!!

Kama ni ngumu sana kuongea na mama yako,basi kaa chini na ndugu yako mmoja unae mwamini,
mwambie kwa uwazi kabisa duku duku lako,then yeye ataongea na mama yako na mtajua chanzo cha tatizo ni nini,

yawezekana kabisa wewe ndio tatizo,ila hutajua kama wewe ni tatizo hadi muongee kwa
kina kujua chanzo cha yote hayo

Option za kuwa muwazi na kuongea ni ngumu sana nakuhakikishia,lakini option
nyingine ya kukaa kimya ni ngumu zaidi maana "una mpa shetani nafasi ya kukudanganya kuhusu nini ufanye
juu ya hali iliyopo
",.....trust me,shetani hata kushawishi kufanya mazuri,....

Matokeo yake ndo tutasikia oooh,kamuua ndugu yake,mdogo wake,mama yake (God forbid in Jesus name)!!!!

Njia pekee ni kuomba,then kaongee nao!
Yawezekana na wao (ndugu zako) na mama yako wana duku duku nyingi sana
kuhusu wewe lakini wanaona kuna namna flani ya ukuta kati yenu,....UVUNJE UKUTA HUO SASA!

All the best

nimeupenda sana usauri wako kwa huyu ndugu yetu. namshauri auzingatie sana sambamba na ushauri wa wengine

Mungu akubariki sana mpendwa

Glory to God!

Episodes,
nadhani umegundua baada ya kusoma mawaidha yote haya kuwa wewe ndiye chanzo cha kujiweka mbali na mama yako. Hakuna anayeona mawazo yako kuwa na tija.
Kama ulivyosema kuwa wewe ni mtu mzima, basi unafahamu unachotakiwa kukifanya hapa. Kamwombe mama yako msamaha kwa kujitenga kwako na yeye pili jaribu kuwa karibu naye. Tatu iweke familia yako karibu na yeye pia. Mara nyingi huwa inatokea kwa mtu kama wewe pia na familia yako inakuwa mbali na huyo mtu. Sitashangaa ukisema na mkeo na watoto hawako karibu na mama yako. Unaua ukoo wako!
Pengine una mawazo ya zamani kuwa mtoto wa kwanza lazima awe tajiri kuliko wadogo zake. Hayo yamepitwa na wakati.
Utakuja kushangaa sana ukisikia kuwa mama yako pia anahangaika juu yako na haelewi tatizo lako ni nini.
Kusema kuwa mama yako ni mmachame siyo hoja. Kumbuka na wewe damu yako ni nusu mmachame pia.
Mwombe mungu akuongoze ufanye jambo la hekima. Kujitenga kwako kusije kukakosesha watoto wako baraka na upendo wa bibi na ndugu zako wengine.

Huyo mama ni wa hajabu. SIsi mama yetu anampendelea zaidi asiye na uwezo na sisi hatusikii vibaya kwani tunaona ni huruma ya mama kwa mtoto. Yani tulikuwa na kaka yetu mama alikuwa anampendelea sana kwa kuwa alikuwa hana mbele wala nyuma; aliamua kwenda shule kwa sasa ana kazi yake na yuko mbali; ila those days alipokuwa arosto ndio alikuwa kipenzi na ukimsema vibaya kwa mama tegemea kununiwa.

Hiyo ndio "nature" tuijuayo, mama huwa karibu zaidi na yule asiye na bahati, yule aliyepotea, yule asiyependwa na jamii, yule mnyonge. Mama huwa ni mlezi wa maisha na ni nani wa kumlea? mwenye mali au asie na mali au mwenye mapungufu yoyote yawayo? Mama huwapenda wanawe wote bila kipimo ila hujitahid sana kwa yule mwenye mapungufu ili asimzidishie unyonge na pia kuonesha mfano kuwa wenzake pia wasimtenge kwa mapungufu yake tu.

Nadhani huyo mama anaependa mwanawe mwenye mkwanja tu ana matatizo ya kichwa. Ananshangaza.

Eeh Mwenyeezi Mungu tuondoshee haya majaribu ya dunia, tuwapende wenye nacho na wasio nacho, wawe wetu au sio wetu. Na tuliojaaliwa kuwa navyo tuvi "share" na waliopungukiwa na wao wasijihisi kuwa wana mapungufu. Ni nani ajuwae kuwa alichonacho leo kesho anaweza kuwa hanacho tena? Na yule asiye nacho kesho ndio akawa anacho?

ndugu zangu wana jf member mliochangia hapa mmenibadilisha mawazo yangu
naanza kufikiria tofauti japo naona kama ni ngumu sana
ni ngumu sana lakini nitajitahidi sana kufanyia kazi mawazo yenu wote hapa
napenda kuwaeleza wazi ya kwamba mkasa huu ni wa kweli na mungu ni shahidi
sijui niseme nini lakini naona kama nina safari ndefu kufanyia kazi hilo

Pole sana Episodes kwa kufikiria hivyo..Labda kweli na kwa asilimia kubwa labda si kweli.

Michango mizuri imetolewa hapo juu na utakuwa umemsoma "Boss, na pia wengine. Kwanza kabla hujamuhukumu mama yako tafakari vigezo unavyochukua kumuhukumu mama yako. Kuna uwezekano wewe ndiye tatizo au jamii inakufanya uamini mama yako ni tatizo.

Asilimia 98% bila kujali kabila, utaifa, rangi, au unatoka machame upendo wa mama ni wa pekee. Kumbuka moyo wa mama unauwezo wa kutoa machozi ndani kwa ndani kwa miaka mingi..Asilimia kubwa ya kina mama wanashindwa kuwahukumu hata wale watoto wao waliowasaliti..wanawakubatia.lakini mioyo yao inaendelea kulia kwa kushindwa kuwapa furaha. Asilimia kubwa ya kina wanishia kubeba machungu ya maisha ya watoto wao.."mtoto hakuwi kwa mama" kina mama wanajiona wao ndio tatizo kwa jinsi watoto wao wanavyoteseka.

Kuna nafasi kubwa kubwa mama yako anasikitika sana na maisha yako kiasi cha kutoweza kukwambia. Kuna uwezekano mkubwa mama yako hapati usingizi kwa ajili yako akiona wadogo zao wana maisha mazuri..Je wewe unawezaje kujua hili? Kwa kumwangalia jinsi anavyotabasamu wakija wadogo zako?

Kabla hujakata tamaa na kumuhukumu mama yako..Jaribu kujirudi..Mpende mama yako hata kama unajihisi yeye akupendi..ukiweza kujishusha kwa hilo utaweza kusikia kilio cha moyoni cha mama yako na siyo kile kinachotoka mdomoni kwake.

ndugu zangu wana jf member mliochangia hapa mmenibadilisha mawazo yangu

naanza kufikiria tofauti japo naona kama ni ngumu sana

ni ngumu sana lakini nitajitahidi sana kufanyia kazi mawazo yenu wote hapa

napenda kuwaeleza wazi ya kwamba mkasa huu ni wa kweli na mungu ni shahidi

sijui niseme nini lakini naona kama nina safari ndefu kufanyia kazi hilo

Asante sana ndugu yangu. Safari ni ndefu sana. Sikujui jina ila nitakuombea kila siku ili mambo yawe mazuri.
Mungu ni mwema na tukumbuke sisi binadamu tuna mapungufu mengi sana. Tupeane moyo.
Utayashinda yote haya. A problem shared is a problem solved. Kuna kitabu kinaitwa 'the love challenge'. Ni kwa ajili ya watu waliopo kwenye ndoa ila mafundisho yake ni mazuri sana kwa majaribu ya aina yoyote. Jaribu kukitafuta.

Kwa haya uliyosema umeshafikia kutafuta suluhisho.

Kwanza pole sana, inapofikia hapo tatizo ni kubwa sana. Ni vema unamuheshimu mama yako na endelea hivyo maisha yote. Mama ni sehemu yako na ana uchungu na wewe kama ulivyo nae. Nakuhakikishia una uchungu sana na mama yako kinachojitokeza ni kuwa lipo lingine limeweka ukungu wa juu juu tu.

Kuna tatizo la kisaikolojia kuwa ukiwa wa kwanza ulitarajia kipaumbele ikiwa ni pamoja na majukumu. Unapoona mama anatoa kipaumbele kwingine unahisi dharau kutokana na hali yako. Yaweza kuwa mama anaelewa kuwa wewe unauwezo mdogo na anataka kukulinda(nature) lakini unatafsiri tofauti. Inaweza kuwa ni inferiority complex inayotokana na tofauti za vipato, na inaweza kuchangiwa na mwenye kipato kutotambua nafasi yake na nafasi ya heshima katika familia n.k

Njia nzuri ya kumpenda mama yako ni kujiuliza, wakati ukiwa hujijui nani alikuwa anakubadilisha nguo, nani aliyekuwa anajua una njaa. Kuna wakati mama alikuwa mgonjwa yawezekana au kulikuwa na dhiki kama njaa, lakini ni mama huyo huyo alitoa titi lake unyonye pengine ni damu tu. Fikiria ni misuko suko mingapi mama yako alipambana nayo wakati wa kukulea akiwa anakesha kuangalia homa isipande, na asubuhi akiwa na usingizi anakuwahisha hospitali, akirudi apike uji na kuhakikisha umeshiba. Ukifika hapo jiulize je yote hayo si upendo uliozidi manyanyaso ya uwezo?Kwanini achukue dhamana ya yote hayo kama hukupendi? na wewe utamlipa nini chenye thamani hapa duniani kama si upendo na mapenzi yasiyo na uzani.

Ondoa kabisa hisia za chuki na kama anakufanyia isivyo wewe unatakiwa umlipe upendo na mapenzi. Ninakuhakikishia ni upendo tu ndio utambadili mama yako, na hicho ndio uwezo mkubwa mungu amekupa bila gharama. Mpe upendo wa dhati na jiulize unamwita mama leo talaa(mungu apishilie mbali) inakuwa vinginevyo nani utamwita mama?

Wewe ndiye utambadili mama, na ondoa chuki kwa kufikiria yale milioni 1 ya hatari aliyokunusuru nayo dhidi ya 1 la uwezo. Akikuambia wewe huna uwezo tabasamu na mwambie yote ni majaliwa, mama ninakupenda sana na nakufikiria kila mara.Mzawadie kidogo ulicho nacho akitupa mwambie hicho ndicho ulicho nacho na umehangaika ili apate kwasababu unampenda sana.

Hakuna unachoweza kufanya zaidi ya kuapa kuwa wewe hutawafanyia hivyo wanao. Msamehe mama yako...

Chamsingi achukulie swala hilo kama changamoto, ajitume zaid katika kusaka mafanikio kwan yaweza kuwa ufunuo wa Mungu kwake kupitia swala hili. Amsamehe mzazi wake na kuchukulia kama madhaifu yake. Na yeye asijitenge na ndugu zake!

wewe utakuwa hupendi kufanya kazi, na huwenda umekwisha bagua kazi kibao wakati huna ujuzi wowote....vitabu vya dini vinasema mama ndio kila kitu kwenye maisha kwani huwezi kusingiziwa mama...na huenda hizo zote ni laana ndio maana hufanikiwi. jitahidi kujishughulisha na usiridhike na umasikini.

Mkuu chukua hiyo kama changamoto fight for life na nadhani ndo njia MUNGU aliyokuwekea ya kutokea na umwombe MUNGU Ampe uzima ili utakapofanikiwa ajiazibu mwenyewe kwa kujuta alichofanya

Nemo andika kiswahili jamaa aelewe. Narudi kwako Ep...nina experience kama yako and I know vile inauma nakuelewa sana mie sipendwi na wote na ninapuuza na kuwasaidia pale napoweza sijali kabisa na maisha yanakwenda hapo jipe moyo tu usijali

Similar Discussions

Back
Top Bottom