Namshukuru Mungu!

Masikini_Jeuri

JF-Expert Member
Jan 19, 2010
6,829
1,296
Wapendwa mabinamz na wapwaz!

Namshukuru Mungu kwa kuniokoa katika ajali iliyonipata juzi usiku nikielekea Iringa katika Hifadhi ya Taifa ya Mikumi umbali wa km 7 toka Mikumi mjini,

Kwenye gari tulikuwamo watu wa 5 na mmoja wetu hali yake si nzuri (tumuombee); alikimbizwa kwenye hospitali ya Kijeshi ya Lugalo baada ya kupitia Hospitali ya mt. kizito na baadaye hospitali ya serikali ya Morogoro..ni askari mwanafunzi wa kambi ya Mgambo Tanga.


Ukiachia kuchanika kidogo kidole cha mkono wa kushoto maumivu niliyo nayo ni ya msuli wa bega la kushoto na si makali sana. namshukuru Mungu.

Nilikuwa nikijitahidi kulipisha lori amablo lilionekana kujaa katikati ya barabara huku likwa limewasha taa zote; sikuwahi kusimama na kupunguza mwendo kiasi cha kutosha ndipo dereva wa lori alipotukwepa ghafla na kutuacha tukisemeza na body yake! impact ya kwanza ilikuwa ni kutoboka kwa tairi la mbele kulia upande wangu na gari kupinduka mara 3 kuelekea upande wa kulia na kutupwa porini mita 12 toka barabarani.
 
Oooph MJ pole sana na ajali hii lakini mungu ni mwema na ana makusudi na wewe kukuweka hai mpaka leo tuko JF pamoja Kumbe leo tungekuwa tunasema mengine ....
Mpe pole sana Rafiki yako mungu atamsaidia kupona haraka
 
Pole sana Muumba wetu akujalie upone haraka, akuepushe na majanga mengine na kukupa maisha marefu.
 
Pole sana rafiki,namshukuru Mungu kwa ajili yako na hao wengine pia.Wape pole wenzio,i pray for a quick recovery
 
Pole bro, Mshukuru Mungu kaktika yote, Mungu ndiye mwenye mamlaka yote na Ndiye Mwanzo na Mwisho, Kwa hiyo yeye ndiye anajua mwanzo wako na mwisho wako na hata kusudi la kukuleta Hapa Duniani, unatakiwa uelewe kusudi hasa la mungu katika Maisha yako.
Karibu tena JF.
 
Pole sana MJ........MUNGU apewe sifa maana yeye ni MWEMA kila wakati.....tunakuombea upone haraka maumivu..
 
Du! MJ pole sana naamini Mungu aliyekuponya na ajali atairejesha tena afya ya huyo ndugu mwingine, get well soon.
 
Pole sana MJ, mungu na akuponje mapema ili uendelee na shughuli zako kama kawaida.
 
Pole MJ....Mungu akuepushe na majanga ya aina yoyote....drive safely wherever you are dear..
 
Wakuu MJ kanitumia some of the snapshots za ajali yenyewe...Ni Kumshukuru Mungu kwamba kweli kuna watu wamepona....some more to come
 

Attachments

  • DSC00632.JPG
    DSC00632.JPG
    74.7 KB · Views: 195
  • DSC00590.JPG
    DSC00590.JPG
    66 KB · Views: 186
  • DSC00589.JPG
    DSC00589.JPG
    81 KB · Views: 195
Mungu Mkubwa.............awajaalie afya na uzima na kuwalinda na ajali na majanga mengine daima- amen
 
Too bad and devastating!Kweli Mungu ni wa ajabu sana!Mshukuru sana Mungu, na ninaamini ana mpango maalum na wewe, ndio maana kakunusuru!Nasi tunakuombea sana wewe pamoja na jamaa zako wote, mpone haraka, mengineyo yatajirekebisha taratibu!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom