Namshukuru mungu sikusoma UDSM

2010 UNIVERSITY RANKINGS​
The Minister of Education and Vocational Training Hon. Prof. Jumanne
Maghembe (MP) and the Ministry in general congratulate the University of Dar es
Salaam (UDSM) for achieving the top 100 in 2010 University ranking and
recognize UDSM contributions to quality higher education in Tanzania.
In his appreciation to the Hon. Minister, the Vice Chancellor of the University of
Dar es Salaam Prof. Rwekaza Mukandala said that UDSM shall continue with the
effort to uphold quality in the implementation of its mission, goals and
objectives, also to ensure that the achievements made from time to time are
visible internationally through the web.
According to the recent Web Popularity Ranking, University of Dar es Salaam is
ranked 10​
th while Sokoine University of Agriculture is ranked 45th out of the top
100 Universities in Africa. In terms of East and Central Africa, University of Dar
es Salaam is ranked 2
nd while SUA is ranked 6th position.
As stipulated in the recently developed Higher Education Development
Programme (HEDP), it is expected that by 2015, about 20-30% of Tanzania
Universities shall be ranked amongst the top 100 Universities in Africa. "This
indeed is a challenge to other Universities and University Colleges in the
country", said the Hon. Minister.
ISSUED BY THE DIRECTORATE OF PUBLIC SERVICE

6
TH MAY 2010



inapatikana kwenye
www.udsm.ac.tz/.../2010-5-6-16-44-53_2010%20university_rankings.pdf
 
kwa kuangalia haraka haraka tuu, kama watu wengi wa humu ndiyo wamesoma udsm, kweli kazi ipo huko nyumbani.

Hawa ndo wale waliokosa admission pale UDSM, na wakaenda kusoma nje katika college za ajabu ajabu mpaka anashindwa kuandika story katika mtiririko mzuri na unaoeleweka kwa wasomaji.

Poor Nancy!!
 
kwa kuangalia haraka haraka tuu, kama watu wengi wa humu ndiyo wamesoma udsm, kweli kazi ipo huko nyumbani.
binti Nancy Tweed, please come back ufafanue what did you mean, mbona humu jf tuko wengi ambao elimu zetu sio za kihivyo, usije ukawa unakihukumu UD kwa posti zetu ambao sio wa univesity level?.

Unavyoonyesha wewe uko nje ya nchi, ukijifanya unasoma reputable univesity kumbe unachofanya haswa ile ile oldest profession hapo ulipo na kuja humu kwa posti yako ya kwanza ukijifanya, kushaangaa bila kukisema kikushangazacho.

Welcome jf.
 
serikari ndio inayotuangusha bwana!kuna mifano mingi sana kama kina Prof Baregu kuona kwamba hawana maana na wakati huohuo wanafunzi wanasema wameridhika na ufundishaji wake,pia Udsm inashuka hadhi kutokana na ongezeko la vyuo vikuu kuwa vingi wewe huoni hata zamani kulikuwa na shule za sekondari zilizokuwa zinatamba sana lakini miaka hii hazisikiki kabisa kutokana na ila kata kuwa na sekondari na kata nyingine kuwa na sekondari zaidi ya 6 so wasomi wameongezeka na hili soko huria nalo linachangia wanafunzi wengi wanasoma nje ya nchi hasa wenye vipaji maalum ndio maana UDSM kwa sasa haitoi matunda kama yale ya zamani ila ukiangalia kwenye world ranking ya vyuo vikuu Africa na Kidunia bado utakuta UDSM ipo juu kwa nchi za ukanda wa africa mashariki kwa kifupi tembelea linki hii hapa!!Ranking Web of World universities: Top 12000 World Ranking na nyingine pia hii hapa 4 International Colleges & Universities | World Universities Web Ranking
 
Nancy, first post unaanza na UDSM, ok tell us where have you studied..? baba yako ana chuo? halafu nidhamu yako is too low, in general unawadhalilisha wote waliopo na waliomaliza UD, unatoka DOM no dought, this shows u have babish, kiddish, childish mind, kama umefika chuo nitashangaa, don't expose ur ignorance here, best way kuficha ujinga wako keep quite, nikwambie hivi, ungesoma UD usingekuwa na ubongo unaotamka haya madudu, u join JF kusema haya?

Hana lolote, utamu na ubaya wa Ngoma uingie Ucheze, Hajsoma Udsm atajuaje ya Udsm, au anatafuta Umaarufu Kupitia JF. Kwa taarifa yako kwa East Africa nzima Udsm is Still in Chart. Nambie chuo gani chenye Ubora Kuliko Udsm. Pole kwa kutosoma Udsm.. Umenikumbusha Msemo mmoja "Virginity is not a dignity but lack of opportunity" Kwa hiyo kutosoma Udsm si swala la kujisifia but ulikosa Opportunity.
 
Kwa ujumla Elimu ya Tanzania katika vyuo vyote haiendani sambamba na changamoto za karne ya 21 iliyotawaliwa na technolijia na ubunifu wa hali ya juu,wote unakuta tunamaliza vyuo huku tukifocus kuajiriwa katika maofisi flani flan na sio kuwa wajasiria mali.Swala la ujasiriamalia mali limekuwa ni kitendawili ambacho wengi wetu tumeshindwa kukitegua kwa kusema hatuna mitaji maana yake tunashindwa kuwa wabunifu wa kubuni namna ya kujikwamua kutokea chini.Ningeomba tujadili namna ya kujikwamua kutokana na mfumo mbaya wa Elimu isiyokuwa na tija kuliko kuanza kurushiana makombora ya chuo na chuo hatujengi tunabomoa
 
Unaweza kuwa specific Dada Nancy ?

UDSM pamechoka, tulishawahi kuchambua maandishi kutoka tovuti yao hata mtoto anayeenda hizi English Medium schools na kurudi nyumbani kufuatilia CNN kwa makini hawezi kuandika vile.
Unaposema chuo kikuu unamaanisha udsm. Chaguo lako la kwanza enzi uliyosoma lilikua hapo ulipokosa ndo ukaangukia ulikosomea hicho cheti chako. Kwa ujumla wote mnaonyesha inferiority katika hili
 
Watu wa UDSM naona mmo kwa nguvu humu kutetea shule yenu....pigeni harambee basi walau mpate hela za kuifanyia ukarabati.....
 
The topic seems to be hot!!! First of all I should admit that UDSM, though lagging behind a bit, it's not as worse as other Tanzanian Universities. Until recently, UDSM has highest ratio of Lecturers with PhD qualification compared to other Universities in Tanzania.

As for other educational facilities, it's true that it's a serious setback to professional excellence not only to UDSM but also to other PUBLIC UNIVERSITIES in TZ. Ni kweli majengo yamechakaa sana UDSM(ingawa baadhi ya vitengo vinafanya maboresho makubwa mfano UDBS). Vile vile student enrollment iko juu sana kulinganisha na available facilities, Serikali haifanyii maboresho maslahi ya Wakufunzi kitu ambacho kinashusha morali yao ya kazi(Hili tatizo la vyuo vyote vya serikali), Public funding on higher education imeshuka sana kitu kinachoathiri si tu mambo ya kiutawala ya chuo bali pia na maendeleo ya mwanafunzi mmoja mmoja(rejea tatizo la mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu). Sasa hivi baadhi ya maprofesa wa vyuo vyetu wameamua kuacha taaluma zao na kukimbilia siasa kwa sababu za kimaslahi. Ajabu ni kwamba serikali haionyeshi kuguswa na tatizo hili.

Ni ukweli usiopingika kuwa UDSM ilikuwa Harvard ya Tanzania lakini sasa inaporomoka kwa kasi ajabu. Ikiwa jitihada za makusudi hazitafanywa, huenda muda si mrefu ujao UDSM ikawa ni chuo cha kawaida. Serikali inatakiwa kubuni mkakati mahsusi wa kuokoa elimu ya juu Tanzania, la sivyo, wahitimu wa vyuo vyetu hawataweza kushindana katika soko la ajira Afrika Mashariki na duniani kwa ujumla.


According to rankings released by British Times Higher Education in 2010 kwa sasa ranking ya UDSM katika Africa ni 22nd and in East Africa, this is the ranking:

  1. Makerere University(No. 13)
Followed by:
2. University of Dar Es Salaam (No. 22)

And Finally:
3. University of Nairobi (No. 26)
 
Nakubaliana nawe kwa kiasi fulani, hata mie sipafagirii sana mlimani kutokana na ubabaishaji, jamaa wako kinadharia zaidi katika kufundisha kuliko kivitendo.
Lakini inategemea umemaliza kitivo kipi kwani baadhi ya vitivo vinatoa wachapa kazi hodari na vitivo vingine hutoa vihiyo. Naomba niongolee mifano michache inayohusu vitivo vya sayansi na injiniaring.
Nlipata kusikia kuwa kuna injinia mmoja wa umeme alikufa kwa kupigwa shot na high voltage, kisa alitumia tochi kumulika katika chanzo cha high voltage. Na haya majengo yanayoanguka wakati yakijengwa kwa mainjinia si wanatoka mlimani??? Kwa mtindo huu, kweli kazi ipo.
Mimi binafsi ni graduate wa DIT. Nlipokuwa field kipindi fulani tulikuwa na wanafunzi wa mwaka wa pili kutoka chuo kikuu fulani. Cha kushangaza wenzetu walikuwa hawajui hata kuandaa
1 Molar solution
.
Ha ha I can smell some Juche here!.
 
kwa kuangalia haraka haraka tuu, kama watu wengi wa humu ndiyo wamesoma udsm, kweli kazi ipo huko nyumbani.

Kwa kuangalia tu ....?...

...Amasing how you can conclude all that ...kwa kuangalia tu!!

..You must be a genius ... above ..UDSM!!!..so you r very right Nicy!
 
Kwa kuangalia tu ....?...

...Amasing how you can conclude all that ...kwa kuangalia tu!!

..You must be a genius .
.. above ..UDSM!!!..so you r very right Nicy!

Kwa mamlaka niliyopewa nakutunukia Nancy Tweed shahada ya uzamivu ya Chuo kikuu cha Dar es Salaam.
 
I have to declare before, I did my undergrad pale mlimani.

Hebu tujiulize, tunapima quality ya university kwa viwango vipi? Kwangu mimi naona UDSM inashuka kwa sababu zifuatazo. Walimu wengi siku hizi research imekuwa chini mno. Walimu hawapublish kabisa. Mfano nikiangalia hata department ninayoifahamu vyema kama sheria. Ukiangalia publication list kwa kweli ni wale wale tuu wa siku zote ndo wana-publish (here I mean Chris Peter, Majamba, Juma na wengine wachache). In fact kiukweli Prof. Peter ndo unaweza kusema ana-live ile ideal ya kuwa academician. Otherwise..research imekuwa zero kabisa. Yet, hawa hawa unakuta wanalalamika wanataka kuwa maprofesa! Na kinachouma zaidi ni walimu vijana pale sheria.....yaani hawaandiki kabisa! Now you wonder..kwanini waliomba kazi za kuwa walimu....to me..being academian..means you are being paid to think!

My views ni kwamba UDSM must reclaim its research niche. Inabidi deans waweke kanuni za walimu kupublish kila miezi miwili au mitatu! Honestly speaking ni aibu kwa hali ilivyo sasa (again hata hao deans hawapublish, sidhani kama watakuwa na audacity ya kuwaamuru wengine). Tusipime chuo kwa majengo (ingawa ni kigezo muhimu, lakini hilo liko mikononi mwa serikali ambao ndo wamiliki). Ila tuwapime kwa kigezo cha research (ambacho ndo kiko katika uwezo wao). Na in fact ndo kazi tunayowalipa kwa kodi zetu waifanye.

I am the living product of UDSM lakini nasikitika kusema kwamba...walimu wetu siku hizi wanakimbizana na consultancy zaidi kuliko kufanya kazi waliyoiomba ya kufundisha. Najua tuna justifications nyingi..maisha magumu, ukosefu wa facilities nk..yet ukweli unabaki..bila kufanya research na kupublish..huwezi ukajiita Profesa nikakuheshimu. Ndo maana mimi kwa pale kitivo cha sheria..zaidi ya Chris Peter na Shivji..wengine wote uprofesa wao nakuwa na some reservations maana najua kabisa....hata ukiwagoogle..huwezi pata zaidi ya publication tatu. Just try you will tell me.

Academicians need to publish their work in both national and international journals. Departments nyingine sijui hali ikoje.

So to me..hata kama ni UDOM au Mzumbe...kama wakiwa serious na research..I would still give them kudos! But I have had a chance kuangalia publication list ya Prof. Mmoja wa Mzumbe..duh..it was pathetic! Anyway twende hivyo hivyo tutafika...
 
serikari ndio inayotuangusha bwana!kuna mifano mingi sana kama kina Prof Baregu kuona kwamba hawana maana na wakati huohuo wanafunzi wanasema wameridhika na ufundishaji wake,pia Udsm inashuka hadhi kutokana na ongezeko la vyuo vikuu kuwa vingi wewe huoni hata zamani kulikuwa na shule za sekondari zilizokuwa zinatamba sana lakini miaka hii hazisikiki kabisa kutokana na ila kata kuwa na sekondari na kata nyingine kuwa na sekondari zaidi ya 6 so wasomi wameongezeka na hili soko huria nalo linachangia wanafunzi wengi wanasoma nje ya nchi hasa wenye vipaji maalum ndio maana UDSM kwa sasa haitoi matunda kama yale ya zamani ila ukiangalia kwenye world ranking ya vyuo vikuu Africa na Kidunia bado utakuta UDSM ipo juu kwa nchi za ukanda wa africa mashariki kwa kifupi tembelea linki hii hapa!!Ranking Web of World universities: Top 12000 World Ranking na nyingine pia hii hapa 4 International Colleges & Universities | World Universities Web Ranking


Kwa hii theory yako..siku hizi Cambridge ingekuwa ni ya mwisho UK au Oxford maana these are the oldest universities. Anyway the point is..bila research msitegemee kwamba UDSM au chuo chochote kita-improve. Hebu tembelea research page ya department mojawapo ya chuo kama Cambridge uone walimu wanavyofyatua vitabu kama kiwanda cha matofali! Tutasingizia facilities..lakini hawa hawa walimu ndo wanashinda wanakimbizana na consultancy za world bank nk...

We need to invest in education. Elimu siyo siasa.
 
Who are those great minds that are coming out of there? Name names sir!!

Unataka nikubali kuwa kuna vijengo vipya. Sawa nakubali. Lakini hivyo vijengo vipya ni asilimia ngapi ya campus? Vipi yale ya zamani? Mbona yametelekezwa? Hata ulinzi ni hafifu hadi ofisi za walimu zinawekewa magrill ya kuzuia wezi. Hii ni aibu!!! Au wewe unataka kuniambia hali ya chuo hicho ni nzuri tu na unaridhika nayo?

Karibu kwenye 50th Anivessary ya UDSM mwakani utawaona ustake kila kitu utajiwe'
 
I will always say, UDSM is still the best not only in Tanzania but in Africa and the world at large.. Nimesoma pale, nimemaliza nimefanya kazi nimerudi pale now. Hawa wanaongea kishabiki tu wanafkiri kufika Mlimani ni lelemama' Angalia ni watu wangapi wenye heshima duniani wanakuja na wanazidi kutaka kuja Mlimani, Thabo Mbekhi alikuja, Samir Amir alikuja achilia mbali wasomi wa nchi nyingine ambao kila siku wanakuja pale kwa either joint programs na mambo kama hayo. Wanakiamini UDSM na wanajua tu sio historia ila pia na idadi ya machapisho inayofanywa na watu walioko pale.

Lakini pia kuna nduigu zetu wamesoma pale hawataki kurudi, kila wakitaka kuongea wanaenda UDOM, wanajua UDSM ina utamaduni wake ni chuo cha kimapinduzi kihistoria na na kinatoa watu makini na walimu wake wengi ni watu makini na wanaoheshimika sana duniani' Na kama hawajui sidhani kama Dr. Asha Rose Migiro ana opinion sawa na wewe juu ya UDSM. Na kila siku anasema anatamani kurudi pale.

Ninachotaka kusema hapa ni kwamba UDSM si pahala pa vilaza, Watu makini wanapapenda na kila siku wanataka kurudi ili kuleta mawazo makini, ila vilaza na wababaishaji hawataki kuja wala kurudi maana si pahala pao pale'

UDSM is the best in the country na kwa kuangalia watu wengi waliopo pale najua itabaki kuwa hivyo, yatachoka majengo ila mawazo imara na utamaduni wa chuo kile utabaki imara pia!!
 
Back
Top Bottom