Namshukuru Mnyika kupeleka hoja ya katiba Bungeni-Sumaye

kapotolo

JF-Expert Member
Sep 19, 2010
3,727
2,213
waziri mkuu mstaafu F. Sumaye amezungumzia mambo mengi yanayoigusa jamii, mojawapo ni kumshukuru mnyika kwa kupeleka hoja ya katiba mpya bungeni, pia amezungumzia Dowans na kuwaunga mkono akina Sitta kwamba wana haki ya kuzungumzia hilo hadharani kwa kuwa halikupelekwa katika kikao cha baraza la mawaziri.

TBC1 Habari
 
Safi walioko nje ya serikali wakizidi kueleza ukweli, hapatatosha,na hadi ukweli wa nani aliyeko madarakani asiyetaka fahamika kuwa ndiye dowani original ajulikane, na kuwajibika.
 
Yaani bado kabisa, mpaka ukweli utakuwa peupe peeee; haijawahi mwanga kuzidiwa na giza hivyo ndivyo itakavyokuwa Tanzania. Hata kama wataendesha semina na makongamano ya kuhamasishana kusoma taratibu za bunge kwa lengo la kupinga kila kitu toka kwa washindani wa haki (wao wanawita wapinzani). Ukweli utabaki kuwa kweli na si vinginevyo. Aluta cont....... Mungu ni wa haki, na itapatikana ndani ya taifa hili.
 
Safi sana Mhe. Sumaye. Lazima uwaambie ukweli. Kwa sasa huna cha kupoteza. Hao mafisadi ndio waliokuchafua sana wakati ule ulipogombea kuteuliwa kuwa mgombea urais kupitia sisiem. Kumbe lengo lao lilikuwa ni kuwapa fursa mafisadi waitafune nchi yetu.
 
Hivi kuna watu bado wanamsikiliza sumaye?

Topical, katika hili wapo watakaomsikiliza. Wamemsikiliza. Kwa bahati mbaya hata wale wenye madoa watasamehewa kwa sababu tu hili la Dowans na Katiba linawagusa wananchi. Kipindi hiki wengi wataonekana mashujaa kwa kusema kile wananchi wanataka kusikia. Kwa hali ilivyo waliosahaulika kwenye siasa za Tanzania wamepata a new lease of life! Leo hii Lawrence Masha akitoa tamko kali (najua hatatoa) kuhusu Dowans na akasimama kuunga mkono Katiba mpya atasifiwa na kupongezwa na huenda akashinda ubunge akigombea jimbo litakalokuwa wazi Dar au Mwanza!!
 
Hongera Sumaye maana kama unaweza kusema hadharani....tunajua kuwa u msafi boss wako anaogopa hadi kivuli chake,sema baba wazalendo wameisha nchi hii hata waliofundwa uzalendo kwa miaka mingi JK na BWM wameshindwa kushika mafundisho hayo,...sema Sumaye sema...ungana na wazalendo wengine msaidie kurudisha maadili
 
Na bado.... Warioba, Salim, Msuya na Malecela mko wapi?? Go Sumaye go.
 
Dowans dowans dowans jamani inavikuna vichwa vyetu watanzania, ccm mmetuingiza makaburini humo.
 
Ila jamani tuwe makini sana na hawa wanaoongelea hii issue wengine ni kwa ajili ya kujirejesha katika masikio, mawazo na fikra za watanzania....
 
Walio karibu nae wanasema bado naye ana ndoto za kuwa Rais wa Tanzania na alishaanza kujipanga kichinichini muda mrefu tu
 
Hivi huko serikalini hakuna hata mtu mmoja liye bakiza akili hata kidogo ya kutafakari kuwa wa Tanzania wa leo si wale wa enzi zao! hivi utalipaje campuni ambayo mmiliki wake hajulikani! je nani alikuwa anaendesha keshi inayo semekana ameshinda na serikali inapaswa kuilipa DOWANS, Hata hawa wana intelejensia wanao weza kuota vurugu zinaweza kutokea sehemu fulani, watu wakiandamana wanashindwaje kututabiria wanimmiliki wa DOWANS!, Kweli hii nchi imepata viongozi wabishi, wanaopenda kufuata ndoto ya kuwa watanzania ni wajinga hawaelewi, wakati kitu kipo wazi kabisa, hivi ni kweli mmiliki wa dowans hajulikani!, mimi naomba mkurugenzi wa usajili wa makampuni brela, ajiuzulu, kazi yake maana hawajibiki ipasavyo,kampuni kama haijasajiliwa kinashikaje tenda, ya kusambasa umeme, nyie kweli mabwege niheri mungu angewapa viwiliwili tu bila vichwa wala ubongo, au akajaza matope huko minyoo wakaishi huko. maana havina issue. mnakesha angani kama popo mnakwenda ulaya hamjifunzi kwa wenzenu wazungu! wao kiongozi akishapata kashfa anajiuzulu, ninyi mnang'ang'ania nini huo ni urithi wa babazenu? mmnaniudhi kweli, yaani ninyi mtakufa vibaya kwa laana na jasho la walipa kodi wa Tanzania, mnachuma laana na kupeleka manyumbani kwenu kuwalisha watoto wenu, vizazi vyenu ni laana tupu! jamani wana jf samahani nina hasira sana.
 
Hivi kuna watu bado wanamsikiliza sumaye?

Kwani kuna tatizo gani kumsikiliza Sumaye? Sasa usipomsikiliza utajuaje kama ana hoja za msingi au laa? Au nyie ndo wale mnaohukumu watu kwa sababu ya majina, sura au historia zao? For your information maoni ya Sumaye kwenye TBC1 jana yalikuwa bomba sana!
 
Nilimsikia, na kweli alinikuna sana...kuanzia leo nimecha kumuita ZERO.
 
Back
Top Bottom