Elections 2010 Namshauri JK amchague Dr Slaa kuwa Mbunge ili aburudishe Bunge

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Dec 26, 2006
4,184
671
kwa kua naamini bila ya shaka yeyote ile kua zimebaki siku chache dr slaa kujuta kwa kuacha kugombea ubunge na kuona jinsi gani wenziwe walivyomuuza

ningelimuomba mheshimiwa Rais JK katika kipindi chake cha pili, ktk zile nafasi zake kumi amteue ndugu yetu Dr slaa kurejea bungeni ili azidi kutuburudisha naomba hili nikithamini baadhi ya michango yake na kwa kujua kuwa Rais wetu mpendwa una upendo na wapinzani na ni njia ya kuwalea kama ilivyo kwenye ilani yetu kutoa fursa zaidi kwenye demokrasia

kama ulivyomchagua Mheshimiwa sanya naomba mara hii umpatie huyu jamaa pia ili asiadhirike maana atakua hana la kufanya na amepora mke wa mtu na amtelekeza familia yake
 
Wewe nawe unasahau haraka sana, Dr. slaa alishasema kuwa hakuna kulala na hawezi kujutia iwapo atashindwa kwa njia za haki.
Lakini sasa wewe na hiyo kura yako iliyopotea unaona itampeleka JK Ikulu tayari. Sivyo! Kuna watu kibao wanaojitambua na watampigia mtu Makini wa kutetea taifa lililokosa dira kama TZ
Hawezi juta ndugu yangu, yeye ni katibu wa Chadema, na ataendelea kuongoza TZ.
kwa kuwa JK ataboronga sana kipindi hiki atakachoiba hizi kura, basi hata 2015 Dr. lazima akanyage njia ya Magogoni!
 
Unajua maamuzi yaliyochukuliwa na baadi ya watu mpaka kuwaita mashujaa huwa kila siku ni magumu yakiwemo ya kupoteza uhai kwa ajiri ya jambo fulani. Mimi ni mwana CCM naamini leo hii mungu akiwaita Slaa na JK jina la slaa litabaki vizazi vingi kuliko la Kikwete. Labda nieleze ni kwa nini, Kwanza Slaa ametoa mchango mkubwa kwenye Kilimo kwanza kuliko mtu yeyote Tanzania kwa kuwa pesa zilizoingia huko ni yeye ndiye aliyezifichua bila yeye isingewezekana. Slaa hata asipopata Urais atabaki kuwa shujaa tu Tanzania na hatutamsahau nadhani baada ya baba wa Taifa Slaa ndiye anayefuata kwa kujari maslahi ya wananchi. Namwombea Mungu ampe faraja kuwa jina ameliandika duniani na watoto na wajukuu zetu watalikuta.
 
Nashukuru kuwa wewe ni Mtanzania wa ukweli kabisa.
Tatizo watu wengi washaona ukweli lakini wamebaki kushabikia tu kama wasiojua TZ iende wapi.
Naogopa kuwa hawaijui Tanzania na hawajui Mambo ya maendeleo
Dr. Slaa tayari ni rais hata kama kura wataiba atawakimbiza sana tu pamoja na wizi wao
 
Kwa maoni yako hayo moja kwa moja kura yako imepotea ila ukumbuke kuwa katika historia ya nchi hii mtu kama dr slaa hatasaulika na kuna wengi watamwiiga na kuja kuleta badiliko ya kweli,hivyo kuondoa mfumo wa utawala wa kifalme na wanao jiona mungu watu,
 
Kwa kweli mimi naamini hapa Tanzania tuna watu hawana chochote kinachowasukuma klitetea taifa letu liondokane na ufisadi uliokithiri. Huyu aliyeandika hivi ni msaliti mkubwa na asiye na tija katika mjadala huu. Slaa, potelea mbali asipate urais yeye bado atakuwa shujaa maana kazi aliofanya haiwezi kulinganishwa na upupu aliofanya huyu ndugu yenu.
 
nnamuomba afanye hivyo kwa kuamini mchango wake kule bungeni unahitajika

mara nyengine kubalance watu wenye kihere here cha mambo ambao ni maprovoker kama slaa wanahitajika

na kwa ubunge nnamkubali ila sio urais kwa vile urais atakosa 100% NAMUOMBA RAIS KWA HESHIMA ZOTE ATUREJESHEE BURUDANI YETU BUNGENI
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom