Namrudisha Mke wangu kwao

Habari zenu waheshimiwa,nimeamua kumrudisha mke wangu kwao.
Sababu kuu ya kufanya uamuzi huu ni kwamba mie ni mtu wa wanawake wengi nje,kula nyumbani ni kwa mbinde kulala nako kwa week naweza nikalala nyumbani mara moja na yeye kutonifanya chochote,namuonea huruma huyu binti wa watu,nataka nimrudishe kwao naona kama nambania kwa kuwa nami bora nimrudishe kwao anaweza akapata mume muadilifu atakayefanana naye tabia.
Ila mpaka sasa sijamwambia kitu,nataka jumapili hii nimwambie twende kwao tukawatembelee wazazi na ndio hapo nitakapolilipua hili bomu.Nalog off

Nahisi kama MUNGU wako ni tofauti na wengine au na mkeo. Ulimuoa kwa ndoa au alijiuza kwako? Una unafananaje na avator yako? Huyo shangazi yako ana sura nzuri sana mpaka amwite mkeo bundi.

Wewe na shangazio kama hambadilishi hayo maneno yenu ya kifedhuri, nakuapia utakuja humu na neno la kumtafuta mkeo na hutamuona wenye sura za bundi watakuwa wamemchukua hapa ndiyo ukurasa wa maisha yako utakuwa umefunguka ki umaskini.

Usicheze na MUNGU wewe.
 
Ongea nae kwanza. Maybe anampenzi wake na yeye, anakuja kulala wewe ukiwa haupo. Sasa ukimpeleka kwa wazazi utakua umemkosea sababu hawataweza kuonana kwa muda (she will have to pretend kwanza kabla hajam-introduce). kwa hiyo we ongea nae tu, kama vipi umpeleke kwa boyfriend wake...
 
hongera sana kwa uamuzi huo mkuu. mwanaume lazima uwe na roho ya kaba, na ktk hili umeonyesha uanaume wako. wasiwasi wangu ni huyo uliyemfulia chupi ataishia kukukamata jumla jumla!
 
Hapana bi dada sijafuata maneno ya Shangazi ila mie namuonea huruma huyu binti wa watu kwa kweli,naomba unisamehe kama nimekukera Sweet lady,mie naona kama vile namzibia rizki na pia naogopa nisije nikamwambukiza nami nikiambukizwa huko nje ninakokwenda.Nalog off

kwenye rangi hapo siilikuwa jana tu mmeshauriwa au wewe haikuhusu..:target:
 
hongera sana kwa uamuzi huo mkuu. mwanaume lazima uwe na roho ya kaba, na ktk hili umeonyesha uanaume wako. wasiwasi wangu ni huyo uliyemfulia chupi ataishia kukukamata jumla jumla!
Usihofu mkuu ujue huyu ninakaa naye nyumba,nikisema niombe mzigo atakuja kunisumbua siku za usoni,kwahiyo huyu bi dada sintomgusa. Nalog off
 
Kweli kua uyaone! Si mchezo. Mambo ya Rais wa watu wasafi haya....yanatupa changamoto kwelikweli
 
kwani mkeo amekuambia kwmba anachukizwa na tabia zako.. kama kashazoea hiyo taabu ... kwanin umrudishe?
hajaniambia kama anachukizwa ila mie naona bora nimrudishe tu wajanja wasiwe wanamega kisela.Nalog off
 
kwani hao mabinti unaopiga nje naniliuu zao zina Gold...?? fafanua wapata nin nje ambacho mkeo hana
aisee ni vingi mno,ila kwa imani ya dini yangu sitakiwi kumfanyia hivyo mke wangu wa ndoa.Nalog off
 
Kumrudisha kwao ndo kumuonea sasa! Unadhani ile small house yake atakua anonana nayo vipi? Manake kwao babake atakuwepo kila siku, kwako ukiwepo hiyo siku moja kwa wiki unamkera kera tu anavumilia anajua kesho haurudi? Unadhani yeye hana akili kubaki hapo na visa unavyomfanyia!? Unanchekesha(FF, 2011)
mie nimeliwaza sana hilo suala na ndio maana nimeona bora nimtie chaka tu,maana isiwe small hausi anajimegea kisela,kwahiyo kama wanapendana basi wataoana mie siwezi kuubeba msalaba wa wengine.Nalog off
 
Back
Top Bottom