Nampenda sana waziri Magufuli, ni waziri ambaye hana mfano

Ni kweli hana mfano mkuu.
Sii unakumbuka alivyouza nyumba zetu kishabiki tena kwa demu wake na nduguze?kisha akatuambia ss wananchi wa kigamboni ambao hatuna ongezeko la nauri ya kivuko tupige mbizi?sasa ww ktk maisha yako uliwahi kusikia kauli chafu kama hiyo???????

Hivi unajua kauli chafu wewe? au umepandikizwa na maadui wa Magufuli hivi kupiga mbizi ni kauli chafu je angesema HUNA AKILI WEWE NA WOTE MLOTAKA KUANDAMANA KUPINGA NAULI YA MIA TATU ingekuwa ni kauli nzuri kwenu na wabunge wenu wachovu? Siyo kila kitu uchangie kama huwezi kuheshimu kazi nzuri za wenzako mbiga mbizi.
 
Mimi natoka kanda ya ziwa anakotoka Magufuli.
Nadhani utakubaliana na mimi kuwa ni kweli mawaziri wanastahili kuadabishwa.
Je Magufuri alisaini kuunga azimio la kumung'oa PM?

Wewe kweli kanda ya ziwa la binadamu wala siyo ziwa Victoria, huko hakuna watu mbumbumbu kama wewe, hivi ni waziri gani na wa dunia gani atasaini kuindoa serikali yake madarakani? Au umelewa kaka yangu basi kama hivyo pombe ikiukutoka utagundua kosa lako.
 
Kazi kwelikweli

Binafsi namkubali Pombe Magufuli.

  1. Yupo straight kwenye maamuzi yake
  2. Ana waadabisha vizuri tu watendaji wake wabovu na legelege haangalii cheo chako
  3. Ana uwezo mkubwa wa kusimamia vipaumbele vya wizara kama vilivyo kwenye mipango na sera
  4. Anashiriki kikamilifu katika shughuli za wizara kwa kusoma na kukosoa mipango na bajeti za wizara
  5. Hana ubaguzi kwa wafanyakazi wake ukabila, dini wala cheo, anasikiliza mawazo ya hata ya wafanyakazi wa chini.
  6. Hakumbatii wawekezaji wala kushobokea rushwa zao au 10% percent zao (nina ushahidi)
  7. Amezuia huuzwaji au ukopaji wa magari ya serikali kwa wafanyakazi (hususan magari ambayo bado yapo poa tu). Viongozi wengi walikuwa wanatumia mwanya wa kujifanya magari mabovu angali mazima ili wajikopeshe

Mapungufu

  1. Alishindwa kuzuia uuzwaji wa nyumba za serikali
  2. Maneno yake makali hata mahali pasipo

Changamoto kwake

  1. Ukosefu wa fedha hadhina kunamfanya ashindwe kutimiza malengo ya wizara yake
  2. Udhaifu wa chama chake

Note: Magufuli na serikali ya Ben walikuwa na mpango wa kuuza nyumba za serikali chache ili wajenge nyumba za wafanyakazi katika wilaya mbalimbali nchini na fedha hizi zilikuwepo mpaka Ben alipokuwa anamaliza muda wake na miradi ilianza lakini awamu ya JK hawakuendeleza. Hapa walishindwa kusimamia vema huuzwaji wa hizo nyumba ila naona mipango yao ilikuwa na nia njema.

Kuwaongelea mawaziri wenzake hadharani: Miaka yote katika wizara alizozunguka Magufuli amekuwa na kawaida ya kwenda kwa rais na kablasha lake la bajeti ili apatiwe fedha za kuendeleza shughuli za wizara na hupewa go ahead na kwenda kwa waziri wa fedha ili mipango itekelezwe (hutoa msukumo wa hali ya juu kufanikisha malengo ya wizara). Inawezekana amefanya hivyo tena akapewa miahadi na mkulo lakini hajatekelezewa ndio maana akatumia hiyo mbinu
ingawa sio nzuri. Kumbuka pia hakuwa kambi ya JK huyu.

Hitimisho: Kwa mimi Magufuli ni waziri makini, bora na mchapakazi ukilinganisha na wengine.

Naomba nikuweke sawa kwenye mapungufu ya Magufuli nilipotia red na kubold kuna vitu vinakupiga chenga kwenye maamuzi anayofanya Waziri WAZIRI HAWEZI KUAMUA/KUFANYA KITU CHOCHOTE ISIPOKUWA KWA BARAKA ZA BOSS WAKE. JUU YA NYUMBA HAKUWA NA MAAMUZI BALI KUKUBALI BOSS ALICHOTAKA NA HIYO NDIYO NIDHAMU PEKEE ALIYO NAYO BROTHER MAGUFULI TOFAUTI NA MAWAZIRI WOTE AKIWEMO PM. KAULI ZA UKALI NI LAZIMA ZITUMIKE KWAKUWA ANAJUA FIKA KWAMBA MKIAMBIWA KWA KUBEMBELEZWA MNAFIKIRI NI UTANI KWA MAGUFULI HILO HALIPO NA NDIYO MAANA ANAOGOPWA KULIKO ........... JAZIA MWENYEWE
 
Wazir bora 1995- 2005 mngesema nani kama si JK,ishu ni kutembea na vyombo vya habari,eti miaka 3 ya wizara ya uvuv kakamata meli ya wavuvi haram,wizara ya Ardhi kafanya nn?,jamaa katumia stail ya Dr.Love wa nyumba nyeupe kutumia makanjanja kumuoshea nyota!

Wewe ujinga na wivu unakusumbua tu katika mawaziri wanaosemwa bungeni umesikia Dr. John anatajwa hata na wabunge wa upinzani kwamba hafai? kabla ya Magufuli ni nani mwingine aliyekamata hata mtumbwi wa kutoka nje ya nchi? Muwe na shukrani basi kwa kazi nzuri wanazofanya wenzenu kama hulitambui hilo muulize mbunge wako atakuambia JDr. John anafanyaje kazi zake. Nasema tena John atarudi kwenye baraza la mawaziri hata likivunjwa mara mia na huo ni uthibitisho kwako na wajinga wengine kwamba Magufuli anafaa.
 
:biggrin1:

kweli mtoto wa mjini haujui kitu wewe ila tukiuliza bekham ana watoto wangapi utajua kila kitu mpaka tarehe waliyozaliwa na hospitali walikozaliwa lakini ya ndani ya nchi yako hujui kabisa kama hujui magufuli nanafanya nini hutajua kitu chochote tena na utotu wako. Kama unajua niambie waziri mkuu wa kwanza tz alikuwa nani?
 
Chukua wanafunzi hamsini wa walioshika nafasi za mwisho katika mtihani wa kata darasa la nne, kisha wape mtihani uleule waufanye tena! Ni dhahiri shahiri kuwa kutakuwa na wa kwanza hadi wa mwisho. Magufuli ni mjanja wa waliofeli! Siwalazimishi kukubali!

Katabia ketu huwa hakajifichi,- kuwa critical kwa kila kitu ili hali uwenda ukipewa wewe hata robo ya aliyoyafanya JP hutafikia.

Penye sifa tusifie kuwapa ari ya kufanya vizuri!JP si Mtakatifu na wala hatutapata mtu Mtakatifu toka popote, ila kwa challenges tulizonazo na viongozi tulio nao, he is outstanding!

Bila ya hivyo asingekuwa waziri wa 4-phase hadi sasa mana huyu si mwana mtandao!!
 
kumpenda magufuli ni sawa na kumpenda mzee wa nji hii kutoka kiraracha marangu kilimanjaro. kwani aliyenunua boti mbovu ya kuvutia panton za kigamboni iitwayo rescue ni nani? je boti hiyo imewahi kufanya kazi yoyote tangu inunuliwe? mbona iko juu ya mchanga pale feri na bado magufuli hajawajibika? au nalo hili kafanya naibu wake kama kwa nundu?
kwani aliyenunua mitambo ya kukatia tikiti za kuvukia kivukoni kigamboni mitambo ambayo tangu inunuliwe miaka mitano iliyopita hadi leo haijafanya kazi ni nani? siyo magufuli na mpaka leo hataki kuwajibika? a na hili nalo kalifanya naibu wake kama kwa nundu? kwani aliyetuingiza mkenge kwa kuvunja kituo cha mafuta mwanza eti kiko road reserve tukalipa mabilioni ya pesa ni nani kama siyo magufuli? magufuli magufuli, kama hujui kuwa katika kapu la takataka hakuna embe zuri nenda kumlambe miguu basi magufuli wako. tangu lini pipa la taka likawa na usafi - rundo lote la mawaziri wa magamba ni taka fulstop.:wave::kev:
 
Magufuli kwa kudanganywa na Mkapa na Sumaye aliuza nyumba za serikali, alifanya kosa,na yeye anajua hilo, lakini hilo litarekebishwa na CDM, nina hakika nyumba zitarudishwa. Ila kwa sasahivi, magufuli anafaa kuwa waziri asiyekuwa na wizara maalum ( wakati wa Mwl Nyerere alifanya hivyo) ndo atapata kazi ya kumtosha. ataenda ujenzi aanzishe miradi ya barabara na viwanja vya ndege, aende fedha ahimize upatikanaji wa pesa, aende madini apate data zote ze uzalishaji migodini, aende sheria na katiba afumue mikataba mibovu, aende mawasiliano na uchukuzi ajenge reli ya gauge kubwa, aende ulinzi asimamie ununuzi wa rada za bei nafuu, aende elimu akamate wote wanaoiba mitihani aende maliasili atupe idadi ya swala na nyani wote aende mifigo na samaki atupe idadi ya kuku na samaki aende mambo ya ndani asukume kesi zote za uchaguzi, aende afya atupe taarifa ya maradhi ya Mwakyembe na Mwandosya. Wengine wote hawana uthubutu wa kutupa hali halisi ya mambo.
 
Mkuu wewe ni maarufu wa kuchambua maovu ya wenzako, nasikitika maana swala la kuuza nyumba lilikuwa ni amri ya Raisi, sasa Magufuli ni nani agomee amri!!! Swala la kuuza nyumba kwa ndugu yake sio isue saana kulinganisha na maghorofa yanayoibuka eti ya wakubwa na watoto wao!!!!

Kwahiyo wewe unaona swala la kuhonga nyumba vimada wake na kuuzia nyumba za serikali ndugu zake na rafiki zake unaliona jambo dogo?

Yeye kama waziri hata kama aliamrishwa nyumba ziuzwe mwisho wa siku utaratibu mzima wa kuziuza hizo nyumba aliutengeneza yeye na watendaji wake. Hizo nyumba zingeuzwa kwa thamani halisi hata haya makelele yasingekuwepo. Tatizo ni kujiuzia nyumba ya Oysterbay milioni 20 wakati kiwanja peke yake milioni 500!
 
Kamhonga nani nani wewe unadanganywa na maadui wa Magufuli unadanganyika swali kwako na wenzako wote kama hafai kwa nini anarudi kila mara kwenye baraza la mawaziri ili hali si mwana mtandao? Walioko juu wana mkubali wakiwemo wabunge wa upinzani umeona analaumiwa mjengoni kama mawaziri wengine? Kama halaumiwi jua anafaa kwa asilimia 1000 utake usitake shauri yako
 
Jamani ndugu zangu watanzania. Waziri Magufuli ni the best Minister ever, ukimuacha marehem Sokoine. Huyu waziri anafanya kazi na kazi imo ktk damu yake. Mimi ni mchaga sina undugu wala hanifahamu. Ila jaman huyu waziri anatisha. Nadhani tuwanzishe award kwa mawaziri. Tuweze kupata maziri weng kama Magufuli. Mim nakuombea afya,nguvu na ulinzi toka kwa Mungu.

misifa tu hana jipya, sitotoa siri za baraza la mawazir maana yake nini? magufuli ayafanyayo sio utaratibu alitakiwa afuatilie tatizo la vifaa kuchelewa sio kutuambia atamchongea kwa rais.Hii inatia shaka ina maana hakuna utendaji wa pamoja bali kila wazir kupeleka umbeya kwa alomteua. je huo ndo uwajibikaji wa baraza pia mawazir kufanya kazi kwa vitisho?
 
Naomba nikuweke sawa kwenye mapungufu ya Magufuli nilipotia red na kubold kuna vitu vinakupiga chenga kwenye maamuzi anayofanya Waziri WAZIRI HAWEZI KUAMUA/KUFANYA KITU CHOCHOTE ISIPOKUWA KWA BARAKA ZA BOSS WAKE. JUU YA NYUMBA HAKUWA NA MAAMUZI BALI KUKUBALI BOSS ALICHOTAKA NA HIYO NDIYO NIDHAMU PEKEE ALIYO NAYO BROTHER MAGUFULI TOFAUTI NA MAWAZIRI WOTE AKIWEMO PM. KAULI ZA UKALI NI LAZIMA ZITUMIKE KWAKUWA ANAJUA FIKA KWAMBA MKIAMBIWA KWA KUBEMBELEZWA MNAFIKIRI NI UTANI KWA MAGUFULI HILO HALIPO NA NDIYO MAANA ANAOGOPWA KULIKO ........... JAZIA MWENYEWE

Mkuu, waziri ni mshauri wa rais kwa masuala ya wizara husika hivyo tulitegemea angemshauri vema juu ya taratibu za uuzwaji wa nyumba hizo. Kwenye changamoto ya pili ndio maana nikasema katika sehemu isiyo (sikupenda kuweka lugha anazotumia wakati wa mikutano na wafanyakazi wake) na sikumaanisha kuwa asiwe mkali katika utendaji ndio maana katika mazuri yake nimesema yupo straight na anawaadabisha wazembe na kusimamia shughuli zake vizuri.

Kwahyo umenielewa vibaya mkuu. Kama kiswahili changu hakijakaa vzr tusamehane. Tupo pamoja mkuu
 
jamani ndugu zangu watanzania. Waziri magufuli ni the best minister ever, ukimuacha marehem sokoine. Huyu waziri anafanya kazi na kazi imo ktk damu yake. Mimi ni mchaga sina undugu wala hanifahamu. Ila jaman huyu waziri anatisha. Nadhani tuwanzishe award kwa mawaziri. Tuweze kupata maziri weng kama magufuli. Mim nakuombea afya,nguvu na ulinzi toka kwa mungu.
ndugu elewa kuwa mawazo yako ndiyo serikali yako hivyo usigeneralized mawazo yako kwa watu wote
 
Jamani ndugu zangu watanzania. Waziri Magufuli ni the best Minister ever, ukimuacha marehem Sokoine. Huyu waziri anafanya kazi na kazi imo ktk damu yake. Mimi ni mchaga sina undugu wala hanifahamu. Ila jaman huyu waziri anatisha. Nadhani tuwanzishe award kwa mawaziri. Tuweze kupata maziri weng kama Magufuli. Mim nakuombea afya,nguvu na ulinzi toka kwa Mungu.

Kama unampenda sana kamtafute mnywe naye chai.
 
Kwahiyo wewe unaona swala la kuhonga nyumba vimada wake na kuuzia nyumba za serikali ndugu zake na rafiki zake unaliona jambo dogo?

Yeye kama waziri hata kama aliamrishwa nyumba ziuzwe mwisho wa siku utaratibu mzima wa kuziuza hizo nyumba aliutengeneza yeye na watendaji wake. Hizo nyumba zingeuzwa kwa thamani halisi hata haya makelele yasingekuwepo. Tatizo ni kujiuzia nyumba ya Oysterbay milioni 20 wakati kiwanja peke yake milioni 500!

Angemuhonga binti yako ungelalamika humu?
 
Mkuu, waziri ni mshauri wa rais kwa masuala ya wizara husika hivyo tulitegemea angemshauri vema juu ya taratibu za uuzwaji wa nyumba hizo. Kwenye changamoto ya pili ndio maana nikasema katika sehemu isiyo (sikupenda kuweka lugha anazotumia wakati wa mikutano na wafanyakazi wake) na sikumaanisha kuwa asiwe mkali katika utendaji ndio maana katika mazuri yake nimesema yupo straight na anawaadabisha wazembe na kusimamia shughuli zake vizuri.

Kwahyo umenielewa vibaya mkuu. Kama kiswahili changu hakijakaa vzr tusamehane. Tupo pamoja mkuu

Sijakuelewa vibaya ninaongezea tena kuwa ushauri ni hiyari ya mtu anayeshauriwa kuukubali au kuukataa sasa hapo kama BM alikataa Dr. John angefanyaje? Pia Kumbuka urais unakuwa ni ushirika wakati wa Kampeni akishaingia Ikulu kaka anaweza kufanya yale ambayo hayakutegemewa kabisa, kwa kusema hivyo nawaomba tumuombe Mungu amsaidie kufanya kazi zake vizuri kwani anafanya kazi katika mazingira ya hatari na magumu sana, pia tumuunge mkono Magufuli badala ya kumkatisha tamaa kwa lawama nyingi zisizo na sababu.
 
Ni kweli hana mfano mkuu.
Sii unakumbuka alivyouza nyumba zetu kishabiki tena kwa demu wake na nduguze?kisha akatuambia ss wananchi wa kigamboni ambao hatuna ongezeko la nauri ya kivuko tupige mbizi?sasa ww ktk maisha yako uliwahi kusikia kauli chafu kama hiyo???????
Teh teh teh lol:becky:!!!
 
hana lolote la ajabu alilofanya zaidi ya unafiki tu mpaka leo nyumba zipo mpaka barabarani pale ubungo jengo la tanesco lipo palepale tumemchoka kabisa.

limbukeni wewe umemchoka wakati jk anamkubali huna adabu mjinga wewe unafikiri ni waziri wa fedha huyo anayefanya kazi za ubabaishaji magufuli ni mbuzi wa shughuli kawaambie na waliokutuma nani kama magufuli?
 
Magufuli anapenda tv utafikiri mcheza maigizo

Jamani tuwe wakweli let we call a spade as a spade and not a big spoon Magufuri kwa kweli ni tofauti na wengine. Swala la kigamboni mbona nauli za daladala zilipanda nani alisema kitu? Gharama za kuhudumia kivuko nazo zimepanda jamani.
 
Back
Top Bottom