Nampenda sana, sipendi afanye kazi.

mitishamba

JF-Expert Member
Dec 21, 2011
697
111
Alikuwa na kazi yake nzuri.
Lakini nampenda sana kiasi kwamba nilikuwa namuonea huruma sasa nimemwachisha kazi ili asipate tabu.

Halafu kuna suala la wivu. Huko alikokuwa anafanyia kazi kuna majamaa kibao. Sikuwa na imani.
Nimemwachisha kazi sasa amepumzika nyumbani, nikirudi namkuta. Ndio furaha yangu.
 
Majamaa yakitaka na kutakwa hata kitandani kwako yatalala na chakula chako yatakula.
 
Mimi huo upendo hata siutaki kwa kweli!....Huo wivu mbaya kwa kweli...huyajui ya kesho....:(
 
  • Thanks
Reactions: BAK
jambo la ajabu sana hili
Yaani unamwachisha mkeo kazi kwa sababu ya wivu
Hiyo mijamaa ya ofcn kwake alikuwa na uhusiano nae
Je mchana kutwa unamlinda asitoke nje ya nyumba yako

hivi siku utamkuta na mtu ndani ya nyumba yako hiyo hiyo utasemaje
maamuzi mengine ya ajabu sana
 
  • Thanks
Reactions: LD
Hongera sana! katika maisha ya leo, majuku yalivyotele - kuliendeleza taifa na nyie wenyewe - halafu mpenzi wako asipofanya kazi - unataka afanye nini? Haishangazi kuona taifa linakuwa goigoi. Pili, kufanya kazi ni haki binafsi ya mtu, huwezi kumuachisha kazi tu mwenyewe, labda mtu mwenyewe awe mvivu, hajiamini, na unamkandamiza tu. Ni kosa la kiutu hilo na sheria pia
 
naomba nijue wivu ndio facilitating factor na pia huo uamuzi ni wako mwenyewe ukiwa sound mind kabisa
 
Alikuwa na kazi yake nzuri.
Lakini nampenda sana kiasi kwamba nilikuwa namuonea huruma sasa nimemwachisha kazi ili asipate tabu.

Halafu kuna suala la wivu. Huko alikokuwa anafanyia kazi kuna majamaa kibao. Sikuwa na imani.
Nimemwachisha kazi sasa amepumzika nyumbani, nikirudi namkuta. Ndio furaha yangu.
una fikra mgando weye mmh pole sana.
nikuambie tu kama ipo ipo na kama haipo mmh unajisumbua tu.
tafakari chukua hatua.
 
Alikuwa na kazi yake nzuri.
Lakini nampenda sana kiasi kwamba nilikuwa namuonea huruma sasa nimemwachisha kazi ili asipate tabu.

Halafu kuna suala la wivu. Huko alikokuwa anafanyia kazi kuna majamaa kibao. Sikuwa na imani.
Nimemwachisha kazi sasa amepumzika nyumbani, nikirudi namkuta. Ndio furaha yangu.

Namshukuru Mungu sikuja JF kutafuta umaarufu!!
 
Naona mnamlaumu na kumshtumu jaama,mwenyewe niko mbioni kumwachisha wa kwangu kazi!msicheze na hisia na mioyo ya watu.
 
jambo la ajabu sana hili
Yaani unamwachisha mkeo kazi kwa sababu ya wivu
Hiyo mijamaa ya ofcn kwake alikuwa na uhusiano nae
Je mchana kutwa unamlinda asitoke nje ya nyumba yako

hivi siku utamkuta na mtu ndani ya nyumba yako hiyo hiyo utasemaje
maamuzi mengine ya ajabu sana
highlighted, ndio siku atakayomtafutia kazi ya kufanya nje ya mkoa wanaoishi
 
Mimi huo upendo hata siutaki kwa kweli!....Huo wivu mbaya kwa kweli...huyajui ya kesho....:(

Sasa we angalia shida ya usafiri, asubuhi kudandia madaladala mtu anasimama kwenye gari masaa mawili, akifika kazini hoi. Wakati wa kurudi vivyo hivyo....yaani tabu tupu hata ukitaka kula akisema amechoka kukupakulia utasemaje?
 
jambo la ajabu sana hili
Yaani unamwachisha mkeo kazi kwa sababu ya wivu
Hiyo mijamaa ya ofcn kwake alikuwa na uhusiano nae
Je mchana kutwa unamlinda asitoke nje ya nyumba yako

hivi siku utamkuta na mtu ndani ya nyumba yako hiyo hiyo utasemaje
maamuzi mengine ya ajabu sana

Home kuna dada wa nyumbani pamoja na majirani, wataning'ata sikio tu.
 
highlighted, ndio siku atakayomtafutia kazi ya kufanya nje ya mkoa wanaoishi

Sasa huko si atapata ugonjwa wa moyo kabis akumuachia simba mwanambuzi alelee
Kama tu hapa mjini na anajua mkewe kaenda ofcn inakuwa issue ni akae mbali nae kwa miezi kadhaa si jamaa atakufa kwa wivu
Aise wivu mambo ingine bana
 
Hongera sana! katika maisha ya leo, majuku yalivyotele - kuliendeleza taifa na nyie wenyewe - halafu mpenzi wako asipofanya kazi - unataka afanye nini? Haishangazi kuona taifa linakuwa goigoi. Pili, kufanya kazi ni haki binafsi ya mtu, huwezi kumuachisha kazi tu mwenyewe, labda mtu mwenyewe awe mvivu, hajiamini, na unamkandamiza tu. Ni kosa la kiutu hilo na sheria pia

Lakini tuliongea na tukakubaliaana suala la yeye kuacha kazi. sikufanya ubabe.
 
Home kuna dada wa nyumbani pamoja na majirani, wataning'ata sikio tu.

Kalaghabaho
Wakati wewe unajua huku wenzako washajua kule
Eti msichana wa kazi na majirani
Duh mkuu funguka macho na masikio sikia la kuambiwa
Ni majirani haop hao watakaokuw awanashinda kwako na house gal huyo huyo atakayekuwa anawapikia chakula wale wapendwa mauncle wa mkeo
 
Back
Top Bottom