Nampenda sana, ila tabia inanishinda... Nisaidieni

hamic mussa

JF-Expert Member
May 1, 2012
227
19
Jamani mimi nina mpenzi wangu ambaye tunapendana sana lakini tatizo yeye huwa na hasira za karibu sana. Yaani naweza nikamkosea kitu kidogo halafu yeye akaninunia siku nzima,kuna wakati mpk inafkia wakati namwambia ni bora tuachane but ye anadai kuwa ananipenda sana na hawezi kuniacha.... Nimejitahidi kila njia kumfanya asiwe anakasirika na kununa nuna lakini nimeshindwa, nilikua naomba mnishauri nimfanyie kitu/vitu gani ili asiwe na tabia hii coz mm binafsi siipendi hlf ukizingatia yeye nampenda sana. Naomba msaada wenu jamani.
 
Kama ulishawahi mwambia muachane akasema hapana kwa sababu anakupenda sana ujue alimaanisha, kwa hiyo you just relax,she is looking for the way to control you! na akisha ku control hakutakuwa na shida coz atakuendesha atakavyo na wewe hutojali utaona sawa! and THAT IS LOVE!
 
ngoja mm nipite tu maana mapenzi yenyewe kwangu mm yako kushoto.
 
Kama ulishawahi mwambia muachane akasema hapana kwa sababu anakupenda sana ujue alimaanisha, kwa hiyo you just relax,she is looking for the way to control you! na akisha ku control hakutakuwa na shida coz atakuendesha atakavyo na wewe hutojali utaona sawa! and THAT IS LOVE!

kwa hiyo nikubali tu yy anicontrol?
 
Mapenzi kama mchezo wa kiduku......unaweza kufikiri ni rahisi kucheza kumbe yahiitaji moyo na roho
 
labda ni mkurya,bila kupigwa anaona hapendwa,siku nyingine akinuna mnasue kibao....:nerd::yawn:
 
labda ni mkurya,bila kupigwa anaona hapendwa,siku nyingine akinuna mnasue kibao....:nerd::yawn:

Huyo ni kama demu wangu anahasira na kununa nuna na anatamaa za pesa kwelikweli lol! Hawa wadada wa sikuhizi ni vimeo kweli

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Kama kweli unampenda, mchukulie jaribu kumuelewa zaid jaribu kujua nini anapenda na nini hapendi!
 
Kama kweli unampenda, mchukulie jaribu kumuelewa zaid jaribu kujua nini anapenda na nini hapendi!

Yeah! Wakati wa amani kaa naye muulize nini kinamsumbua, tabia yako asiyoipenda. Akisema kinachomkwaza jitahidi kujirekebisha kadri uwezavyo. Pia mwambie kuwa unampenda na hukusudii kumuudhi hivyo naye ajitahidi kudhibiti hasira zake asikate mawasiliano. Mkae msuluhishe kila tatizo linapotokea. Kufurahi muda mwingi zaidi ni kwa manufaa ya uhusiano wenu na kwa afya yako na yake.
 
Jaribu kuona ni kawaida na usioneshe kukerwa na hiyo hali na dhani utamzoea sababu ina wezekana ana kupenda kweli lakini ndiyo alivyo.
 
Yeah! Wakati wa amani kaa naye muulize nini kinamsumbua, tabia yako asiyoipenda. Akisema kinachomkwaza jitahidi kujirekebisha kadri uwezavyo. Pia mwambie kuwa unampenda na hukusudii kumuudhi hivyo naye ajitahidi kudhibiti hasira zake asikate mawasiliano. Mkae msuluhishe kila tatizo linapotokea. Kufurahi muda mwingi zaidi ni kwa manufaa ya uhusiano wenu na kwa afya yako na yake.

thanx braza nimekuelewa 100%
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom