Nampenda lakini naogopa kumwambia nifanyeje?

upendo wa dhati huwa hauangalii hayo kwa mtazamo wangu...ukimpenda utamwamini, na kumheshimu. Kama dada atatokea kukupenda pia sidhani kuna kukwazwa kwa sababu ya mali.

Mbona wewe ulinipiga kibuti?
 
Kaka Kilimo Kwanza, na ukiona demu unamuona yuko serious ujue hajakupenda. Watu tuliwatokea walimu wetu ije kuwa huyo? unajua haya mambo huwa magumu naye hapo alipo kuna mtu kamfia anashindwa jinsi ya kumuingia. Lakini nakushauri akili nyingi peleka kwenye kilimo kwanza.
 
Sasa st roy unamshauri aendelee kuteseka? inawezekana hata huyo mdada hana mtu kwa kigezo cha kuogopwa na men so inaweza kuwa opportunity kwa idea.

Mateso ya kwenye mahusiano ni mabaya zaidi...
huwa tunamilikisha kila kitu tukishapenda....gari ataendesha, ndani atakaa kwenye kochi huku kafunga taulo, atm kadi atajua password.....mbona simple sana.....mwache kijana ajitose bana

Kuna mahusiano yasiyo na mikwaruzo ya hapa na pale?? Itokeapo mikwaruzo ndipo ataiona dunia mbaya....
 
kwenye umri sio tatizo sana kwa kuwa ukipenda umri sio issue kabisa na suala la elimu ni wewe tu kujipanga na kuhamua kujiendeleza baadae kielimu ili muwe sawa au uwe zaidi yake. Tatizo naloliona hapo ni kipato, hapo ndio kuna issue maana kinamama nao wakiwa na kipato cha juu sana kutuzidi uwa inaleta mushkeli kwa medula kila unachofanyia utaona kama unaonewa vile na sio wewe tu ni kila m/ume na ilo ni tatizo la kibaiolojia jiandae kabisa kuajiri mtu wa saikolojia awe anakusaidia ku-overcome hilo tatizo maana hata ukiambiwa "mpenzi shusha net basi tulale" utahisi anakupa hiyo kazi kwa kuwa ana hela. Hili lipo na alipingiki ni kila m/ume analo
 
Haiwezekani tumpigieeeeeeeeeeeeeeeeeeeee,weka loud spika tumsikieeeeeeeeeeeeeeeeeeeee,haiwezekani umuogope wakati yy ni binadam kama ww!
 
Mwambie ukweli toka moyoni mwako ukiwa na akili timamu kabisa na jinsi gani ungependa awe mke kipenzi chako! Usimtongoze na usitumie nguvu nyingi sana kukidhi std yake, be urself 100% ili akiamua afanye uamuzi ambao ni informative
 
kuna dada mmoja namfahamu toka siku nyingi lakini siku hizi nimetokea kumpenda lkn naogopa kumwambia. Dada mwenye ni msomi kiwango cha mwisho, mstaarab, 36 yrs old na ana uwezo wake lakini yuko serious sana na muda mwingi yuko busy kazini. Nikijiangalia mimi sina tatizo ila elimu, umri na kipato kanizidi. Wandugu nipe njia nitoke vipi?

We nawe vipi? mtokee tu achana na mawazo ya kufikiria sana mapenzi definition yake ni ngumu sana wala hutaweza kuielewa mpaka unaondoka duniani.. ukiona umeshindwa kabisa kwa njia zote kufikisha ujumbe tumia ile ya zamani MWAMBIE NAKUPENDA THEN TOKA MKUKU KAMA ZUZU :) atapata ujumbe..
 
kuna dada mmoja namfahamu toka siku nyingi lakini siku hizi nimetokea kumpenda lkn naogopa kumwambia. Dada mwenye ni msomi kiwango cha mwisho, mstaarab, 36 yrs old na ana uwezo wake lakini yuko serious sana na muda mwingi yuko busy kazini. Nikijiangalia mimi sina tatizo ila elimu, umri na kipato kanizidi. Wandugu nipe njia nitoke vipi?

Acha UDOMO ZEGE, wewe ni mto wa kiume, na siku zote mwanamme ndo kichwa cha familia.
Kuna wimbo unaitwa TOP QUEEN, wa zamani kidogo, ulipigwa na vijana jazi, ebu utafute na usikilize.
 
Je una mpango gani nae?, kama ni maisha nae hapo baadae nenda kamweleze wazo lako, ila kama ni kuzini nae tu mie nakuomba uachane na tamaa hizo, utatolewa nishai hadi uwe unamkimbia anapotokea.
 
kama huna nia nae mbaya,bora mwambie,maana kwa age aliyokuwa nayo,pengine na yeye anapenda apate mtu wake.ili baadae awe na familia yake{i mean mtoto au watoto}si unajua wanawake wana age limit ya kuzaa,lakini kama nia yako ni kumega,bora usimsogelee kabisa dada wa watu.
 
kuna dada mmoja namfahamu toka siku nyingi lakini siku hizi nimetokea kumpenda lkn naogopa kumwambia. Dada mwenye ni msomi kiwango cha mwisho, mstaarab, 36 yrs old na ana uwezo wake lakini yuko serious sana na muda mwingi yuko busy kazini. Nikijiangalia mimi sina tatizo ila elimu, umri na kipato kanizidi. Wandugu nipe njia nitoke vipi?

Pitia kwa sisi viongozi wa dini, tutamaliza kwa kumwambia mchungaji amepata maono kuwa kuna mpango wa Mungu kuwaunganisha!
 
kuna dada mmoja namfahamu toka siku nyingi lakini siku hizi nimetokea kumpenda lkn naogopa kumwambia. Dada mwenye ni msomi kiwango cha mwisho, mstaarab, 36 yrs old na ana uwezo wake lakini yuko serious sana na muda mwingi yuko busy kazini. Nikijiangalia mimi sina tatizo ila elimu, umri na kipato kanizidi. Wandugu nipe njia nitoke vipi?
.....! Pamoja na udhamini kutoka kwa watu wa Marekani umeshindwa...! Unadhani JF wana udhamini zaidi ya huo? Aidha, mimi nakushauri uvunje ukimya, kama ni kupigwa ngwara na upigwe....! Vinginevyo, kalie mbele yake, atakuonea huruma...!
 
Idea ukweli ni kuwa wewe ni mwoga na hata kama ukimpata bado utakuwa na uoga wa mambo mengine ambayo amekuzidi kitu ambacho si kizuri katika mahusiano.
Toa wazo la yeye kukuzidi chochote kati ya ulivyovitajana muone wa kawaida tu hna hapo ndipo utakuwa kwenye nafasi nzuri ya kuwa nae bila ya wewe kupata jakamoyo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom