Nampenda lakini naogopa kumwambia nifanyeje?

idea

Senior Member
Apr 3, 2009
123
16
kuna dada mmoja namfahamu toka siku nyingi lakini siku hizi nimetokea kumpenda lkn naogopa kumwambia. Dada mwenye ni msomi kiwango cha mwisho, mstaarab, 36 yrs old na ana uwezo wake lakini yuko serious sana na muda mwingi yuko busy kazini. Nikijiangalia mimi sina tatizo ila elimu, umri na kipato kanizidi. Wandugu nipe njia nitoke vipi?
 
Sema nae tuu sasa unasubiri nn kama vipi pata beer ya kutoa nishai halafu nenda kampe darasa atakubali tuuu:biggrin1::biggrin1::biggrin1::biggrin1:
 
Love has no count,,,songa mbele ili uridhishe moyo wako, usiendelee kuteseka.
 
we mtokee tuu, mapenzi hayajali hayo yote....kaza moyo

Preta hebu kuwa realistic....unazungumzia mapenzi peke yake bila maisha??
Simshauri idea kujitafutia presha za kudumu katika maisha yake...
 
kuna dada mmoja namfahamu toka siku nyingi lakini siku hizi nimetokea kumpenda lkn naogopa kumwambia. Dada mwenye ni msomi kiwango cha mwisho, mstaarab, 36 yrs old na ana uwezo wake lakini yuko serious sana na muda mwingi yuko busy kazini. Nikijiangalia mimi sina tatizo ila elimu, umri na kipato kanizidi. Wandugu nipe njia nitoke vipi?
kakuzidi kwa miaka mingapi? napata wasi2 kama umempenda au umetamani kile alichonacho ndugu
 
Preta hebu kuwa realistic....unazungumzia mapenzi peke yake bila maisha??
Simshauri idea kujitafutia presha za kudumu katika maisha yake...

Sasa st roy unamshauri aendelee kuteseka? inawezekana hata huyo mdada hana mtu kwa kigezo cha kuogopwa na men so inaweza kuwa opportunity kwa idea.
 
Preta hebu kuwa realistic....unazungumzia mapenzi peke yake bila maisha??
Simshauri idea kujitafutia presha za kudumu katika maisha yake...

huwa tunamilikisha kila kitu tukishapenda....gari ataendesha, ndani atakaa kwenye kochi huku kafunga taulo, atm kadi atajua password.....mbona simple sana.....mwache kijana ajitose bana
 
Mpigie nyeto tu maana kiukweli hamwendani.. naomba nikuulize unaundugu na wallet? yule aliemzimia hausigeli wa mshikaji wake?
 
kweli nampenda na hajaolewa wasiwasi wangu ilikuwa ni vile atanichukulia vipi! Maana naona noma kukataliwa. Kanizidi miaka 4. Ehee wandugu imekaaje hii?
 
Unampenda au unamtamani? Kama unampenda nenda kamwambie kwani hujawahi kutongoza mwanamke katika maisha yako? mbona huyu unamuogopa au unamheshimu ?. Kama unaona ugumu ngoja nikupe mbinu anza kuwa karibu naye tu kujenga mazoea kama ulikuwa hujawahi kumsalimia anza kuwa unamsalimia, ukisha msalimia angalia atarespond vipi atasmile au atanuna? peleleza ujue anapendelea kutembelea sehemu gani na wewe uwe unaenda sehemu hizo anakula wapi mchana, anasali wapi anajipumzisha wapi. Usiogope kwani ukiwa mwoga atakupa wakati mgumu sana. Ukishakuwa karibu na yeye mwalike siku moja kupata naye lunch ili muendelee kufahamiana naye zaidi . Usiwe na haraka ya kuuza sera siku ya kwanza ongelea general issues ukitaka kufahamiana naye tu, mkishazoeana ndiyo umwage sera zako.
 
kweli nampenda na hajaolewa wasiwasi wangu ilikuwa ni vile atanichukulia vipi! Maana naona noma kukataliwa. Kanizidi miaka 4. Ehee wandugu imekaaje hii?
kila kitu kakuzidi my dia, mbele ya safari lazima mtakwazana tuuu!
 
upendo wa dhati huwa hauangalii hayo kwa mtazamo wangu...ukimpenda utamwamini, na kumheshimu. Kama dada atatokea kukupenda pia sidhani kuna kukwazwa kwa sababu ya mali.
 
Songa nae mbele mkuu, akijlengesha kula mzingo hayo mambo ya baadae kitelewka kwa sasa ni mapema kutabiri, lakini kwa kuanzia piga ball mbele
 
kuna dada mmoja namfahamu toka siku nyingi lakini siku hizi nimetokea kumpenda lkn naogopa kumwambia. Dada mwenye ni msomi kiwango cha mwisho, mstaarab, 36 yrs old na ana uwezo wake lakini yuko serious sana na muda mwingi yuko busy kazini. Nikijiangalia mimi sina tatizo ila elimu, umri na kipato kanizidi. Wandugu nipe njia nitoke vipi?

Kweli unampenda au unamtamani? Utaweza kumvumilia hata mkizaa watoto watatu maumbili ya kimwili yakibadilika na gapi lilipo kati yako na yeye ki-umri? Kwa upande wangu huwa napendelea mtu naye mzidi umri kidogo, shule tukiwa sawa siyo Issue kwangu. Kipato huwezi kutabiri maana bado wote mnapambana katika maisha japo huwa napenda mie ndo niwe mhangaikaji zaidi kwa ajiri ya familia, Huwa hainipi picha kumuomba mama watoto pesa ya matumizi wakati mimi ndo natakiwa niyotowe.

Kama unampenda kweli, Inabidi uhangaike zaidi kama baba wa Nyumba na kichwa cha familia Ili aku-appreciate kwa juhudi zako na kukuona kuwe ni baba kweli wa familia na siyo tegemezi maana bila hivyo inaleta dharau japo hata kwambia.

Ushauri Wangu, tafuta lika yako au unayemzidi kidogo ki-umri japo watu wengine wanasema mapenzi hayachagui umri kwangu huwa ni issue ukizingatia wenzetu wakipata watoto wengi wao miili inachoka mapema. Inapaswa ukiingia kwenye ndoa basi umpende mkeo siku zote za maisha yako na siyo kuanza kuangalia mabinti wanaopita na kumuona mkeo mzee. Kama ni maendeleo ya huyo dada, yasikuumize kichwa alihangaika kufika hapo alipo, na yawezekana kafanya sacrifice nyingi, Inawezekana pia ukamtafuta wa umri wako au unayemzidi mkayatengenezaa maisha kwa kadili mpendavyo wenyewe. Usitake ready made sana kijana.
 
Mtokee Mkuu, tena inabidi uanze mazoea ya kumkaribisha diner na kumpa Vizawadi vidogo vidogo ambavyo havitamshtua, Kama mko nae ofisi moja ukienda Lunch ukirudi unamletea hata Bublish, pipi ukiona unakuwa naye karibu na uoga unaanza kukutoka unamuomba muambatane naye kwenye Lunch na vitu kama hivyo, vile vile sio mbaya kuanza hata kumsifia kidogo juu ya Mavazi au aina ya Msuko, Vitu kama dada leo Umependeza naona shemeji anajali kweli kweli, hapo kama hakuna shemeji lazima utamsikia tu " a wapi hakuna cha shemeji wala nini". Cha msingi usiwe mwingi wa maneno kwa siku za mwanzo usije uka expose ujinga wako na ukambore mapema. Ila cha msingi usiwe na nia ya kumchezea tu

Hii Technique inaitwa " Boiling the frog technique" Nikipata nafasi nitaielezea vizuri
 
wee idea just follow your heart mwambie tu unaongopa kuwa atakuchapa viboko, wenzio usituone hivi wapo waliotukataa na walikubali pia.
 
UNAMPENDA
UNAMUOGOPA
UNAMUHESHIMU
UNAMTAMANI

Hebu kati ya hivyo ni kipi kinachukua nafasi yake kwako kwa penzi ulionalo kwake
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom