pepekale
Member
- Nov 25, 2010
- 60
- 50
Nina mpenzi wangu nampenda sana , ila tatizo kubwa lililopo ni kwamba huko nyuma niliwahi kumsaliti na alinisamee tukaendelea na maisha, lakini toka amenisamee amekua ni mtu mwenye hasira na kuwahi kupaniki hata kwa sababu zisizo na msingi. Inafikia wakati ananiambia kama vipi tuachane coz mapenzi yameisha, ila akikaa siku mbili anakuja kwangu ananiomba msamaha huku akilia na kuniambia ananipenda sana. Kiukweli hali hii imekua ikijirudia mara kwa mara mpaka imekua kero kwangu hadi nahisi mapenzi yameanzakupungua na siku zinavyokwenda naweza kumwacha kabisa,ila sitaki tufike huko. Msaada tafadhari nini nifanye ili niweze kuweka mambo sawa .